Mkuu wa wilaya akamata kilo 180 meno ya tembo

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
MKUU wa Wilaya ya Masasi, mkoani Mtwara, Nape Nnauye kwa kushirikiana na polisi wilayani humo amefanikiwa kukamata meno ya tembo yenye uzito wa kilo 180.3 yaliyokuwa yakisafirishwa katika basi la abiria la Buffalo.

Basi hilo linafanya safari zake kutoka Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma kwenda Dar es Salaam kupitia barabara ya Masasi Lindi na kwamba walikamata nyara hizo zikiwa kwenye sanduku dogo la bati juu ya dari ndani ya basi.

Hata hivyo mwenye sanduku hakujitokeza jambo ambalo liliwafanya polisi kuwachukua wafanyakazi wa basi husika.

“Tumeamua kuwashikilia wafanyakazi wanne wa gari hilo, kwa sababu si rahisi kwa mzigo kama huo uingie kwenye gari bila wao kujua, kulikuwa na abiria 24 tu kwenye gari ambao walitafutiwa utaratibu mwingine wa kusafiri,”alisema.

Alisema baada ya uchunguzi wa polisi kukamilika watuhumiwa hao watafirikishwa mahakamani kujibu tuhuma za kukamatwa na nyara za serikali kinyume cha sheria

Akizungumza na Mwananchi ofisini kwake jana, mkuu huyo wa wilaya alisema basi hilo la Buffalo Express, lilikamatwa saa 6 mchana wa Januari, 13 mwaka huu katika eneo la Masasi mjini.

Alisema kuwa kabla ya tukio hilo, polisi walipata taarifa kutoka kwa raia wema juu ya usafirishaji huo wa nyara za serikali na kuweka kizuizi kilichofanikiwa kunasa mzigo huo.

“Baada ya ukaguzi tulifanikiwa kukamata kilo 180.3 za meno ya tembo zikiwa zimehifadhiwa katika dari ndani ya basi, walikata vipande vidogo 67 na kuvihifadhi katika sanduku ndogo la bati, hata hivyo hatukufanikiwa kumkamata mwenye mzigo,” alisema Nape na kuongeza

Nape alitoa wito kwa wananchi wilayani humo kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi pindi wanapobaini vitendo vya uvunjifu wa sheria ili waweze kushughulikiwa
 
tatizo huko tunduru hakuna vyanzo vya habari na huo mzigo utashangaa umepotea katika mazingira ya kutatanisha!kama mmiliki haeleweki jamaa wakiwekewa dhamana!chama tawala kitauchukua kulipia fedha za uchaguzi kwa mafisadi!
 
Back
Top Bottom