Mkuu wa polisi, tusaidie wakazi wa uwanja wa ndege Karakata majambazi wametawala

GPTZ

Member
Sep 27, 2015
84
24
Afande shikamoo,

Yaani huu mtaa umefululiza kwa matukio ya ujambazi wa kutumia silaha.Walianzia kwa mtu mmoja (simjui jina) wakamkosa kosa kumuua, wakavamia kwa bwana mmoja anaitwa Mazongera karibu kabisa na kituo kidogo cha polisi Karakata, sasa Mungu saidia hawakumkuta wakaitesa familia yake.

Juzi wamekuja kuvamia gesti moja hapa mtaani matukio yote ni mfululizo na haipiti wiki.Hofu imetanda hata kulala ndani ya nyumba zetu tunaogopa Ukisikia mpasuko hata wa tairi ya gari unajua ni hao.

Hawa jamaa waovu kwa maana hata wanamvamia mtu bila kuwa hakika kama anazopesa hama lah.Nikuombe mkuu wa polisi; Nakujua wewe kwamba nimchapa kazi tuma kikosi maalumu kukibaini kikundi hiki kiovu nakikamatwe haraka sana.

Mpaka sasa naandika huu uzi nasikia kitu kama risasi mtaani..
 
Jipangeni kwa sungusungu wekeni mtego mkikamata watatu au wawili mnachoma na tairi basi mtakaa kwa amani walau kwa mwaka
 
Muwe mnatumia ajili jaoi kudogi basi! Kila kitu kifanyww na Polisi, hii itawezekana vipi? Polisi wetu ni 'wachache sana' na wote sasa hivi wamepelekwa kuoambana na upunzani. Hilo suala la majambazu sudhani kama linaweza kuwashindeni, hivyo jipangeni namna ya kulimaliza ili mlisaidie jeshi la Polisi nalo angalau liendelee kudhubiti wapinzani kwa amani.
 
Mkuu hao jamaa wao wako Busy na UKAWA.
Hiyo kwao ndio imekuwa Main Job Description.
Labda Mumuombe Mh Halima Mdee ahamie mtaani kwenu watakuwa wanakuja kufanya Patrol na Doria
Kama hao majambazi wanatumwa na ukawa lazima polisi wawashughulikie ukawa kwanza kwa kuwa ndiyo chanzo.
 
Afande shikamoo, yaani huu mtaa umefululiza kwa matukio ya Ujambazi wa kutumia silaha .

Walianzia kwa mtu mmoja (simjui jina)wakamkosa kosa kumuua, wakavamia kwa Bwana mmoja anaitwa Mazongera Karibu kabisa na kituo kidogo cha polisi karakata sasa Mungu saidia hawakumkuta wakaitesa familia yake...

Juzi wamekuja kuvamia gesti moja hapa mtaani Matukio yote ni mfululizo na haipiti wiki.

Hofu Imetanda hata kulala ndani ya nyumba zetu tunaogopa .Ukisikia mpasuko hata wa tairi ya gari unajua ni hao...

Inaonekana Vijana wako wameshindwa kuwakabili hawa jamaa waovu kwa maana hata wanamvamia mtu bila kuwa hakika kama anazopesa hama lah.

Nikuombe mkuu Wa Polisi; Nakujua wewe kwamba nimchapa kazi Tuma kikosi maalumu kukibaini kikundi hiki kiovu nakikamatwe haraka sana.

Mpaka sasa naandika huu Uzi nasikia kitu kama lisasi mtaani..
Hadi uchaguzi wa Meya ukamilike
 
Mkuu hao jamaa wao wako Busy na UKAWA.
Hiyo kwao ndio imekuwa Main Job Description.
Labda Mumuombe Mh Halima Mdee ahamie mtaani kwenu watakuwa wanakuja kufanya Patrol na Doria
Aisee upo njema mkuu salute
 
Dah, unaweza kuta na wewe ni kijana mwenye nguvu tu, sasa unalialia nini badala ya kupambana?
Nimeishi maeneo hayo miaka ya 2003 nakumbuka mchezo huo ulikuwa miaka hiyo lakini tulianzisha doria tulikua na jamaa 1 hivi ni PM wa JWTZ alikua anafanya kazi kambi ya Airwing, kiukweli tulitembeza mkon'goto mpaka adabu ikarudi kitaa!!!
Sasa wewe nakushangaa kulialia tuuuuuuuuu!!!!
 
2003 sasa hivi ni 2016.... unachosema ni sawa lakini sasa hivi hao vibaka sio wa mwaka ule..ukitaka kujua nguvu yao njoo wasalimie jamaa zako huku ikifika saa tano usiku waage we uondoke kwa miguu utakuja kutuambia kwa nini jamaa analalamika.....
 
Mkuu kipindi kile ilikua kuna vijana wanaishi kipawa kabla haijavunjwa, so saa 2 tu wanakua mitaa ya relini kufanya yao, walikua wanavamia viduka saa 2-3, pia walikua wanavunja mageti na kuiba mafriji na TV na vyombo vya maana, ukiamka asubuhi unakuta mlango upo wazi. Na kukata madirisha ndio ilikua fasheni mkuu, nakumbuka niliwahi kutega shoti dirishani na ilimpiga mmoja, but tulivyo anzisha doria mambo yalikua byeeeee sana!!!
 
Dah poleni Sana aisee inabidi jesh la polis lifanye operesheni yake kabla madhara makubwa hayajatokea
 
Mkuu kipindi kile ilikua kuna vijana wanaishi kipawa kabla haijavunjwa, so saa 2 tu wanakua mitaa ya relini kufanya yao, walikua wanavamia viduka saa 2-3, pia walikua wanavunja mageti na kuiba mafriji na TV na vyombo vya maana, ukiamka asubuhi unakuta mlango upo wazi. Na kukata madirisha ndio ilikua fasheni mkuu, nakumbuka niliwahi kutega shoti dirishani na ilimpiga mmoja, but tulivyo anzisha doria mambo yalikua byeeeee sana!!!

kaka mimi sijabisha ila hawa watoto wa miaka hii hapana aisee.....hivi unajua kwa sasa hivi watu bila polisi wakaamua kufanya doria wakaviua kama viwili au vitatu siku ya kwenda kuvizika hivyo vijambazi kuna uwezekano karakata watu hawatalala na kuna uwezekano hata polisi mkawapigia simu na wasije acha ndugu...
 
Back
Top Bottom