Sexer
JF-Expert Member
- Oct 22, 2014
- 8,369
- 8,072
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo amewasimamisha kazi maofisa wawili wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha kwa kukiuka agizo la Rais John Magufuli la kusafiri nje ya nchi bila kibali maalumu cha Ikulu.
Maofisa hao ni pamoja na kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Leah Lwanji na Ofisa Utamaduni wa halmashauri, Abdul Haufi ambao wamekwenda Sweden.
Inadaiwa pia, maofisa hao hawakuwa na kibali kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa.
Ndikilo pia amemvua cheo cha ualimu mkuu wa Shule ya Msingi Maili moja, Sedekia Fanuel kwa makosa ya kuwaruhusu wanafunzi kufanya kazi binafsi za walimu katika muda wa masomo na kosa la kuchelewa kufika kazini.
Itakumbukwa mwishoni mwa mwaka jana, Rais Mgufuli aliagiza kusimamishwa kazi mara moja watumishi waandamizi wanne wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) waliosafiri nje ya nchi licha ya kupiga marufuku safari hizo kwa watumishi wa umma.
Watumishi hao ni Mary Mosha, Ekwabi Mujungu, Doreen Kapwani na Rukia Nikitas ambao walisafiri nje ya nchi licha ya kunyimwa kibali cha safari kutoka kwa Rais ama Katibu Mkuu Kiongozi.