Brigedia Chan-ocha
JF-Expert Member
- Mar 7, 2014
- 1,353
- 2,851
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mlongo ametangaza kuwa, Lazima majimbo ya Ilemela na Nyamagana yarudi CCM wawe wameshinda au hawakushinda, alikuwa akizungumza na polisi watakaosimamia Uchaguzi siku hiyo, amewaambia kuwa, matokeo yote ya ilemela na Nyamagana yatajumlishiwa na kutangazwa katika halmashauri ya Ilemela iliyopo Busweru na amewaagiza polisi siku hiyo kujipanga mita 100-150 kutoka katika halmashauri hiyo ili kuzuia wafuasi na wananchi kuyafikia majengo ya halmashauri hiyo, amesema kuwa, punde baada ya matokeo anayoyataka yeye kutangazwa, polisi wapige mabomu ya kutosha ili kutawanya wananchi.
Note: Mkuu wa mkoa, hivi ICC unaitaka kwa nguvu, familia yako na wewe mtasakwa kwa udi na uvumba.
Usiwaingize Polisi wetu kwenye matatizo yasiyo ya lazima.
Note: Mkuu wa mkoa, hivi ICC unaitaka kwa nguvu, familia yako na wewe mtasakwa kwa udi na uvumba.
Usiwaingize Polisi wetu kwenye matatizo yasiyo ya lazima.