Mkuu wa Mkoa wa Dar amtaka Meya wa Kinondoni aache malumbano afanye kazi

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,735
22,433
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiki, amemtaka Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Boniphace Jacob, kuacha malumbano ya kisiasa na badala yake ajikite kufanya kazi.

Onyo hilo Sadiki limekuja baada ya Meya Jacob kukaririwa akisema manispaa hiyo ina uwezo wa kukabiliana na uamuzi wa serikali wa kutoa elimu ya bure bila kuhitaji fedha zinazotolewa na utawala wa Rais John Magufuli.

Halmashauri ya wilaya ya Kinondoni inaongozwa na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) ambao ni mwamvuli unaojumuisha wabunge na madiwani kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Chama cha Wananchi (CUF).

Sadiki alisema hahitaji malumbano na kiongozi huyo ambayo hayana tija.

"Mimi sipendi malumbano yasiyo na tija baina ya viongozi," alisema Mkuu wa Mkoa na kuongeza; "unapokataa msaada kama huo wa kupunguza mapungufu katika sekta ya elimu, wanaoathirika ni watu waliowachagua."

Serikali imepanga kutumia Sh. Bilioni 137 kugharamia elimu bure katika miezi sita ya kwanza ya Rais wa tano, Magufuli.

Kiasi cha Sh. bilioni 18.77 kilitumwa kwenye akaunti za shule za Msingi na Sekondari za halmashauri zote hapa nchini na vyombo vya usimamizi wa mitihani kwa kila mwezi wa Januari na Februari, kwa ajili ya wanafunzi kusoma bure.

Pesa zilizogawanywa kwenye akaunti za shule za Msingi na Sekondari katika halmashauri zote ni Sh. bilioni 15.7 kila mwezi na Sh. bilioni 3 kila mwezi kwenye akaunti vyombo vya usimamizi wa mitihani katika Halmashauri zote hapa nchini.

Mkuu wa Mkoa alisema fedha hizo zitapelekwa katika Manispaa zote na ametoa agizo kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni kutumia fedha hizo katika matumizi yaliyokusudiwa na si vinginevyo.

Sadiki alisema kwa sababu Rais Magufuli ni kiongozi wa wote, ana haki ya kutoa kwa wote bila kuzuia wala mipango yake kukataliwa.

"Yule ni mkuu wa nchi, hata kama wanakusanya fedha za kutosha, zipo taratibu za matumizi ya fedha hizo,"alisema Sadiki.

Kwa mujibu wa Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mipango wakati akitoa taarifa ya kuanza kwa utumaji wa fedha za elimu bure Januari 6, mwaka huu, walimu wakuu wa shule zote za Msingi na Sekondari katika halmashauri zote hapa nchini wanatakiwa kuweka wazi matumizi ya fedha hizo katika mbao za matangazo kwa kila shule, ili kila mzazi aweze kujua kiasi gani kimetumika.

Sadiki alikuwa akizungumza wakati akipokea msaada wa ahadi ya ujenzi wa madarasa 12 katika mkoa wa Dar es Salaam kutoka kwa Wamiliki wa Malori Tanzaznia(Tatoa), yenye thamani ya Sh. milioni 300.

Mkoa wa Dar es Salaam, alisema Sadiki, una upungufu wa vyumba vya madarasa 7,223, lakini pia uhitaji wa madawati 66,000.

"Yapo maeneo mengi ya kujenga shule, nawaomba wadau wetu muendelee kuhamasisha kupata shule nzima kwani shule nzima inahitaji madarasa kuanzia 22,"alisema.
 
Daaa mayor jaribu kuwa na haiba flani ya kutoropoka...kaa utulie piga kazi malumbano yasiyo na tija tupa kule..cpendi mtu anaelalama bila kuwa na 7bu za msingi...umekuja juzi tu nawe unatafuta kick...fanya kama makonda watu wana appreciate uwepo wake...sasa ww kama utajifanya unajua sana kuliko kuhudumia wananchi itakuwa sio poa
 
Huyu meyor ni mtu wa kutumia msuli sana kwanzia anapongea sijawahi kuvutiwa naye haa kidogo
 
Ulevi Wa madaraka huoo hats wachukue umeyaWadar bila serikali awawesifanyakitu
 
Meya Jacob ni kama Godbess Lema.Tulishawahi kusema inabidi Lema apigwe 'pini' na chama chake.Meya Jacob ni kijana Mwanaharakati. Inabidi CHADEMA imu-'reign in' mapema kabla hajaharibu..
 
Tatizo la kuchaguliwa bila kujiandaa, pia huyu anatumika na walioko nyuma yake kina Mbowe na genge lake Ili tu kutafuta migogoro isiyo na tija kwa wananchi zaidi ya kuendeleza Chuki za machungu ya wakosa ikulu wa UKAWA.
Hakuna lingine hapo. Si wamuige mwenzao zitto kule kigoma kaanzisha mfumo wa kusomesha watoto bure jimboni kwa mfuko wa maendeleo wa halmashauri na wala hapigi kelele.
 
Sijaona mbaya aliloongea huyo Meya.Amesema ukweli kwamba kwa mapato ya Halmashauri tu bila kusubiri pesa za Rais bado wanaweza kuweka lengo la Elimu bure.Kwa maana hiyo badala ya pesa kupeleka Kinondoni ni bora zipelekwe kwenye halmashauri zisizojiweza.Hivi Hata hili nalo jamani??Au sababu siyo CCM??? Anheyasema hayo CCM mngepiga makofi mpaka mchanike mikono kayasema mpinzani imekuwa nongwa!!Nadhani Mkuu wa Mkoa hakumuelewa tu.Mie nilichomuelewa ni kwamba badala ya kwenda kuomba Momba kwa rais wakusanye mapato ambayo Kuna uhakika hata wa kuvuka lengo.
Angesema Makonda mngempigia makofi na sifa nyiiiingi.
Kama la walimu kupanga bure duh.

Meya kufanya kodi achana na bwa CCM wanaobagua viongozi sababu ya itikadi zao
 
Hii ndo inawapunguzia vijana kuaminika katika nafasi kubwa kubwa! Kila siku wao wanawaza uanaharakati tu hata kama hauhitajiki! Sasa kuna ubaya gani serikali kupeleka fedha kwenye halmashauri ya Kino? Ili kesho na keshokutwa uje useme hatukutumia fedha za serikali? Aache ujinga apige kazi bwana! Kwani kuna ubaya gani hiyo hela ambayo wangeitumia kwenye elimu wakaipeleka kwenye maeneo mengine na hiyo ya Magufuli ndo wakaitumia kwenye elimu?
 
Hajui kuwa kampeni zimeisha. Sasa ni mayor wa watu wote bila kujali vyama vyao.
Pesa hazitoki kwa watu wa chama chake pekee. Magufuli keshasema ni Rais wa watanzania wote.
Mayor fanya kazi iliyoko mbele yako. Wakati huu wananchi wanahitaji huduma sio malumbano. Umepewa uongozi, boresha maisha ya wananchi wako.
 
Mambo mengine ni mjinga tu anaweza kuyatetea.

Kama hawahitaji pesa sababu wanayo sasa mbona hawajengi hizo shule?

Mkurugenzi wa hiyo halmashauri alidai kunahitajika shule saba na bado kuna uhaba wa vyumba vya madarasa kwenye shule zilizopo pamoja na madawati na tatizo ni pesa lakini meya anasema hawana shida na pesa sababu wanazo za kutosha wanazokusanya kwenye mabango.

Kinondoni bado chafu na sababu hakuna magari ya kutosha kuzolea taka pamoja rasilimali watu ilhali meya anadai pesa wanazo.

Hata huyo meya wa jiji la Dar akiwa na akili kama za huyu basi tegemeeni malumbano kwenye media tu.

Wenye magovi ya kisiasa na uchama kwenye ubongo hawafai hizi kazi wabaki kwenye majukwaa ya kisiasa tu.
 
Mambo mengine ni mjinga tu anaweza kuyatetea.

Kama hawahitaji pesa sababu wanayo sasa mbona hawajengi hizo shule?

Mkurugenzi wa hiyo halmashauri alidai kunahitajika shule saba na bado kuna uhaba wa vyumba vya madarasa kwenye shule zilizopo pamoja na madawati na tatizo ni pesa lakini meya anasema hawana shida na pesa sababu wanazo za kutosha wanazokusanya kwenye mabango.

Kinondoni bado chafu na sababu hakuna magari ya kutosha kuzolea taka pamoja rasilimali watu ilhali meya anadai pesa wanazo.

Hata huyo meya wa jiji la Dar akiwa na akili kama za huyu Jacob basi tegemeeni malumbano kwenye media tu.

Wenye magovi ya kisiasa na uchama kwenye ubongo hawafai hizi kazi wabaki kwenye majukwaa ya kisiasa tu.
Ni vyema aanze kutumia pesa kutatua matatizo ya wilaya yake.
Lakini akumbuke kuwa hata akusanye vipi, fedha za umma zina utaratibu wake. Hawezi kwa mfano kuamua kuwapa nauli walimu wa wilaya yake bila kufuata taratibu. Hawezi kujenga shule bila kuweka hizo fedha kwenye budget.
Ingekuwa kila mtu anakurupuka na fedha za umma ingekuwa chaos!
 
Lakini nchi yetu inawatu wa aina nyingi kweli hivi viongozi kama jacob wakazi gani sasa kwenye maendeleo watu wanashikamana wala siyo kuleta siasa vijana wengine shida sana maana wanaaminiwa wanaleta vituko.
 
Hawezi kujenga shule bila kuweka hizo fedha kwenye budget.
Ingekuwa kila mtu anakurupuka na fedha za umma ingekuwa chaos!

Hapa sijakupata hasa unamaanisha nini.

Anyway,hili suala la uhaba wa vyumba vya madarasa ni emergency case iliyotokana na hamasa ya elimu bure mfano kuna shule zimeandikisha mpaka wanafunzi 800 kwa std 1.

Sasa basi huwezi kuikataa pesa ya wadau waliojitokeza ilhali unajua pesa yako inapitia mlolongo mrefu mpaka kufika site maanake huyu mayor kaponda mpaka saruji aliyokusanya DC.

Na kama ana nia ya dhati kwa nini asiitishe baraza lake wakapitisha hiyo budget kwa dharula ili ku-solve hizi emergency cases?maanake wanafunzi wanakaa chini huku hataki hisani.

Hii issue Ni sawa na mayor wa huko iliko Pawaga kukataa misaada kwa wahanga wa mafuriko mpaka baraza lake lipitishe budget yake litakapo kaa tarehe isiyojulikana.

Sasa hiyo ni akili au tope?

Wanafunzi waendelee kukaa chini tena nje mpaka mayor atakapojisikia kukaa na baraza lake na hao wanaojitolea ku-solve anadai wanaingilia majukumu yake.
 
Hapa sijakupata hasa unamaanisha nini.

Anyway,hili suala la uhaba wa vyumba vya madarasa ni emergency case iliyotokana na hamasa ya elimu bure mfano kuna shule zimeandikisha mpaka wanafunzi 800 kwa std 1.

Sasa basi huwezi kuikataa pesa ya wadau waliojitokeza ilhali unajua pesa yako inapitia mlolongo mrefu mpaka kufika site maanake huyu mayor kaponda mpaka saruji aliyokusanya DC.

Na kama ana nia ya dhati kwa nini asiitishe baraza lake wakapitisha hiyo budget kwa dharula ili ku-solve hizi emergency cases?maanake wanafunzi wanakaa chini huku hataki hisani.

Hii issue Ni sawa na mayor wa huko iliko Pawaga kukataa misaada kwa wahanga wa mafuriko mpaka baraza lake lipitishe budget yake litakapo kaa tarehe isiyojulikana.

Sasa hiyo ni akili au tope?

Wanafunzi waendelee kukaa chini tena nje mpaka mayor atakapojisikia kukaa na baraza lake na hao wanaojitolea ku-solve anadai wanaingilia majukumu yake.
Kama kuna pesa na imetokea emergency ya aina yoyote, sheria inaruhusu emergency budget as well. Tatizo mayor huyo na wafuasi wake akili ni matope. Badala ya malumbano, angekuwa anandaa mchakato wa budget ya dharura maana ina utaratibu wake kisheria.
Ni mwendawazimu atapinga hilo maana manufaa yake hayatajali chama cha mtu.
Najua anakabiliwa na ugeni katika kazi. Aelekeze nguvu kujifunza ikibidi hata kwa hao mahasimu wake kisiasa. Hilo huwa halikwepeki unless mtu ana akili za mbu.
 
Zama za ndiyo kwa kila analosema mkubwa lishapita lazima tuzooe kusikia ya upande wa pili japo hatutaki kuskia,meya yupo jikoni anaona mzigo unaokusanywa matumizi anayajua sasa asiseme?tuvumiliane ndo demokrasia.
 
Back
Top Bottom