Uongozi ni kuonesha njia.
Makonda kwa ubora wake amewezesha kujenga wodi za kisasa za wazazi na vifaa vyake kwenye manispaa zote za Dar es salaam.
Makonda alikaa na wataalamu wake wa elimu wa mkoa wa DSM,wakati huo mlikua mnabeza kuwajibisha maofisa elimu,moja ya changamoto ilikua waalimu hawana ofisi za kutayarisha vipindi na kusahihisha mitihani,waalimu wanafanya kazi chini ya miembe.
Makonda kwa upeo wake,akahamasisha kamati ya ulinzi na usalama mkoani kwake impe wataalam,JKT na polisi wakatoa wataalam,Magereza wakatoa wafungwa kama nguvu kazi-hapo utaona 50% za gharama zimekatawa.
Dar es salaam ni jiji la kibiashara,makampuni makubwa huwa yanatenga kiasi fulani kwa ajili ya social responsibility,Makonda kwa maarifa yake akayata hayo makampuni yatoe cement na na mabati,hapo utaona 90% ya mradi umeshawezeshwa.
Wakati mwingine kuongoza Dar es salaam hakuihitaji maguvu meengi tumpe hongera na kumuunga mkono Makonda ili watoto wetu wapate elimu bora,badala ya kusubiri kila kitu tufanyiwe na serikali
Watumishi wa umma hawajaongezewa mishahara wala kupandishwa Madaraja mwaka wa pili sasa hata ukijenga wodi nzuri kiasi gani hazitasaidi.
Mmeanzisha elimu bure bila maandalizi matokeo yake unampa mwalimu mkuu laki mbili huku wengine ukiwaacha solemba mnadhani mikwara itawasaidia kuinua elimu au afya? Juzi wikimoja kabla ya mey mosi raisi aliwaita viongozi wa vyama vya wafanyakazi ikulu kwenda kuwaweka sawa! Wapo waliopewa pesa, nyumba, magari na kusomeshewa watto wao nje ili wawasaliti watumishi ambao ndio waliowachagua huyo Bashite hata ukijenga ofisi zitasaidia nn?
Watumishi wamefukuzwa kazi kwa vyeti feki huku makonda akilindwa wewe bado unamsifia ama kwa kutumwa au kujikomba kwake!
Watumishi wengine wamesingiziwa kuwa wanavyeti fake lakini ati wanarudishwa kwa awamu kwenye payroll mbona hawakutolewa kwa awamu.
We endelea kumsifia bashite lakini ukweli unajua kuwa mambo hayaendi na raisi amejawa na kibur, visasi, udini, ukanda na kila aina ya upendeleo