lendila
JF-Expert Member
- Sep 26, 2012
- 5,806
- 4,370
Mkuu wa Mkoa na mkuu wa Wilaya ya Kinondoni tuko chini ya miguu yenu. Sisi wafanyabiashara wa Mwenge tunawaomba sana sana tuko chini ya miguu yenu tunaomba mtusaidie kero ya magari, ili tuweze kupaki magari yetu kwa amani kama ilivyokuwa mwanzoni.
Waheshimiwa sisi tunatekeleza sera za Serikali ya awamu ya tano kwa vitendo, tumejiajiri, tumeajiri na tunalipa kodi. Tunalipia leseni na tunaheshimu Serikali yetu.
Hali ni ngumu sana toka kumetokea katazo la kutokupaki magari kwenye barabara ya Mwenge. Biashara zetu zinazidi kudorora.
Waheshimiwa sana, sisi ni watanzania tunaowaheshimu sana, tunawaombeni sana mtusaidie tuweze kufanya biashara. Kama kuna kosa tulilowafanyia, tunaomba mtusamehe!