Mkuu wa Mkoa Dar, Jipime kuhusu Taka zilizorundikana Barabarani

Hii dhana haipo dar peke yake hata arusha nalo ni tatizo hawa wakuu waliitikia wito wa rais bila kujipanga haiwezekan wananchi tumefanya usafi tokea tarehe 09-12 hadi leo uchafu ulipokusanywa upo wala hawaba dalili za kuutoa tumekusanya mafungu ya uchafu ili kuhararisha mlipuko wa kupindupindu? Jiji la arusha angalien hili
 

Umeongea cha maana sana mkuu
 
sasa kwanini usingejitolea kwenda mamlaka usika ku report wakautoe..? umekuja ku report JF ?
 
Ukistaajabu ya Musa hujayaona ya Firauni, sio huko Dar na Arusha tu jijini kwetu ndiyo usiseme mpaka dakika hii kuna vifusi vya uchafu eti magari ya kuzoa taka ni mabovu. Hivi kumbe hamkuwa na maandalizi?
 

Attachments

  • 1449990529353.jpg
    102.3 KB · Views: 310
Ukistaajabu ya Musa hujayaona ya Firauni, sio huko Dar na Arusha tu jijini kwetu ndiyo usiseme mpaka dakika hii kuna vifusi vya uchafu eti magari ya kuzoa taka ni mabovu. Hivi kumbe hamkuwa na maandalizi?
 
Mawaziri husika wameshateuliwa wachukue hatua sasa mm nadhani kwa Dsm naunga mkono hoja
 
Hii slogan ya "Hapa kazi tu" iongezewe na "tumia akili" peke yake haitoshi
 
Kwa hali hii TUWATUMIE JESHI LETU LA ULINZI MAGARI YAO YAFANYE OPERESHENI UZOAJI WA TAKA.HILI PIA LITAKUWA ONYO KWA WANANCHI WANAOTUPA UCHAFU OVYO OVYO WAKIWAHOFIA WANAJESHI WETU IWE KWA MUDA HUU TU KWANI HALMASHAURI WAMEZIDIWA NA HAO WAKANDARASI UCHWALA WA UZOAJI WA TAKATAKA WALIOLAMBA TENDA TUTAFAKARI TUSILAUMU TU TUTOE PLAN B
 
Kwenye nyekundu: Unaonyesha ulivyo na akili finyu ya kimanamba! Jaribu kufikiria tena na kwa kina!
 

Nchi hii haihitaji kibabe na kuwatisha wananchi, kutumia jeshi ni sawa ila serikali iweke vifaa vya kuweka taka kila mita 100

Hapo ndio unaweza kumlaumu mwanachi kama watatuoa taka ovyo.

Mm naamini Watz ni wasikivu sana na mifano tunaiona kwenye muitikio huu wa uzoaji taka.
 
Hili halina mana ya kuwatisha raia ila basi uchafu huo ukiachwa muda mrefu ni mlipuko wa maradhi.na hili la maradhi ni vita mimi binafsi siuoni ubaya wo wote magari ya jeshi yakawamobilized kusaidia jambo hili ni sawa tu na mafuriko yanapotokea.tusianze kulaumu ooh serikali haikujipanga!la muhimu hapa ni vipi uchafu huu utaondolewa wakosoaji kwa maslahi yao hawakosi leta wazo tusilaumu
 
ndo maana wananchi wamewapa ukawa nao wajaribu angalau watakuja na mbinu nyingine japo tayari kuna malalamiko watendaji wa ukawa wanaomba pesa watu wanaokwenda kupata huduma pasipo kutoa risiti.

Kwani huki ulikojaa uchafu si pengine serikali za mitaa ni ukawa ama wao wanahisi ni sawa ?
 


Kuna makampuni yaliyoshinda zabuni ya kufanya usafi wa mji wanalipwa mabilioni ya pesa. Cha kujiuliza ni kuwa, ikiwa wananchi wamewasaidia kazi ya usafi na kuwakusanyia uchafu wao waokote tu wakatupe na wameshindwa, wataweza kweli kufanya usafi wa jiji? Na baya zaidi, mpaka taasisi nyengine kama JWTZ zinasaidia katika hili zoezi la kuokota huu uchafu.

Kinachonishangaza mimi ni kwa nini viongozi husika hawalisimamii hili agizo la Mh Raisi mpaka likagikia lengo. Labda wanasubiri Mh Raisi afanye ziara ya kushtukizia tena aone huo uchafu. Nafikiri kuipa jina la uchafu wa Magufuli itasaidia zoezi likamilike haraka, kwa sababu wataogopa jina lisitapakae mpaka mwenyewe akalisikia. It's not fair on him, officials let him down big time!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…