Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,487
Mkuu wa mkoa Arusha,Felix Ntibenda kesho anatarajiwa kuwatangaza idadi ya watumishi hewa katika wilaya sita za mkoa wa Arusha.
Akizungumza na Mwananchi, Ntibenda alisema kamati maalum aliyounda imekamilisha kazi na kubaini watumishi hewa.
"Kesho nitaweka hadharani idadi ya watumishi hewa waliobanika na hatua za kuchukua"alisema
Alisema awali alitoa siku saba kwa wakuu wa wilaya na wakurugenzi kumpatia idadi ya watumishi hewa na pia akaunda kamati maalum kufatilia.
Akizungumza na Mwananchi, Mwenyekiti wa kamati iliyoundwa na mkuu wa Mkoa, Richard Kwitega alisema wamekamilisha kazi ya kusaka watumishi hewa.
Kwitega ambaye ni Afisa utumishi secretarieti ya mkoa hata hivyo hakuwa tayari kutaja idadi ya watumishi hewa.
"Msemaji ni mkuu wa mkoa ila sisi tumekamilisha hatua ya awali ya uchunguzi na taarifa tumempatia"alisema.
Mkoa wa Arusha wenye wilaya za Arusha, Monduli ,Arumeru,Ngorongoro,Karatu na Longido umeendesha zoezi la wafanyakazi hewa kutekeleza agizo la Rais John Magufuli kwa wakuu wa mikoa yote kuwabaini wafanyakazi hewa.
source: Mwananchi.
Jiandaeni kulia kama watoto