mmaranguoriginal.
JF-Expert Member
- Jan 1, 2014
- 4,060
- 460
Wanabodi,
Habari zilizotapakaa leo toka asubuhi ni kutoka Manyara ambako Vijana wa CCM Mkoa huo kupitia Vikao vyao walifikia maamuzi ya kumfukuza Katibu wao Bwana Ezekiel kutokana na kutelekeza ofisi.
Hata hivyo habari zilizopatikana jioni hii inasemekana kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha kapokea maelekezo kutoka kwa Catherine Magige mjini Dodoma akimwomba RC wa Arusha ambaye naye pia ameshawasili Dodoma ili kutafuta wasaa wa kukutana na Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Kinana ili waweze kumsaidia Ezekiel katika kunusuru ajira yake.
Uchunguzi umebainisha kuwa Ezekiel anaombewa apelekwe Wilaya ya Monduli na hii ni kutokana na hali ya kisiasa inayiendelea Mkoani Arusha. Ezekiel amewahi kuwa Katibu wa Vijana Wilaya hiyo na aliacha makandokando mengi jambo ambalo bado linaonekana kuwa mtihani mkubwa kwake.
Hata hivyo baadhi ya Vijana Wilayani hapo wamekiri kusikia tetesi hizo na wamesema wanamsubiri huyo bwana kwa hamu kubwa.
Hata hivyo Makao Makuu ya CCM wamesema hawajapata habari hizo ila waliweka walakini wakikiri kuwa Katibu Mkuu kumpandisha huyo bwana haitawezekana manake wana habari nyingi chafu zinazomuhusu Ezekiel.
Huyo Bwana kwanza alikimbia kituo cha kazi sasa hiyo haiwezi kuwa sifa ya mtumishi lakini la pili tuna habari kuwa angefanikiwa kupitishwa na CHADEMA basi angegombea udiwani kwenye mojawapo ya Kata huko Arusha. Hivyo baada ya kushindwa na kukataliwa na CHADEMA akarudi huku ghafla. Hivyo tuna taarifa zake nyingi sana ni kati ya wasaliti wa Chama huyo. Kilieleza chanzo kimoja kutoka Makao Makuu ya CCM.
Chanzo hiki kilipoulizwa inakuaje RC amsaidie msaliti wa Chama huyu naye alionekana kushangazwa. "Unajua hapa ndipo tunapochoka manake wakati wa Mwalimu hawa MaRC ndio waliokuwa wanatusaidia kutupasha habari mbaya na nzuri za watumishi lakini enzi hizi zimebadilika sana wale watumishi wenye sifa nzuri wanapewa mbaya na wale wenye mbaya basi wanapewa nzuri ndo mana tunaamua kwenda wenyewe field.
Tumesikia kuna Vikao vinakaa hapa Dodoma ili kumsaidia huyo kijana ila nikueleze Kinana hawezi ruhusu hilo litokee na navyomjua Katibu Mkuu huyo RC atapata majibu ambayo hakuwahi kuyapata toka kuzaliwa"
Kiliongeza chanzo hicho. Mwaka huu tuna mengi mno ya kuyashuhudia ndani ya Chama kinachotawala manake kila kukicha kuna jipya.
Mytake: Viongozi Wangu Wa CCM okoeni jahazi lisizame.