Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma na watendaji wengine wasimamishwa kazi

Michael Amon

JF-Expert Member
Dec 22, 2008
8,768
3,621
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora Angella Kairuki amemsimamisha kazi Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Said Nassoro kwa kushindwa kusimamia watendaji wake pamoja na watumishi wengine wawili Silvanus Ngata mtumishi wa makao makuu na bwana Joseph Mbwilo mkuu wa chuo cha Kampasi ya Dar es Salaam.

 
Utumbuajiiii. Kwani alishampa mafunzo jinsi ya kuinua utendaji kazi wake ili asimamie wengine? Serikali ya Magu haijui kama kuna sheria.

Unachekesha kweli, mtu ukianza kazi kwani hapewi duties zake au kujua job description?
 
Waziri wa nchi, ofisi ya rais-utumishi na utawala bora Mhe. Angella Kairuki amemsimamisha kazi mkuu wa chuo cha utumishi wa umma Said Nassoro kwa kushindwa kusimamia watendaji wake pamoja na watumishi wengine wawili Silvanus ngata mtumishi wa makao makuu na bwana Joseph Mbwilo mkuu wa chuo cha Kampasi ya Dar es Salaam.

Angellah-Kariuki.jpg
Hivi aliyewaweka hao watumishi wanaotumbuliwa jipu hakuyaona hayo?na kama aliyanyamanzia kwa nini wasianze na yeye?
 
Nina hamu ya kufahamu huyo Mkuu wa Chuo, hicho kinachosemwa "kushindwa kusimamia watendaji wake" kuna maanisha nini, manake penye maeneo ya kazi yapo mengi sana.....ubadhirifu, uzembe, na hata baadhi ya waalimu kutembea na wanafunzi wao!
 
Ninavyojua kuna promotion and demotion

Promotion ni kwa wafanyakazi waliofanya vizuri kazini ambapo. Wanapewa motisha ili. Waweze fanya vizuri zaidi

Demotion ni kwa wafanyakazi ambao. Utendaji kazi wao sio mzuri

Sasa kwenye hii serikali naona demotion tu sijaona mtu ka promotiwa kwa kazi nzuri sasa maana yake ni kwamba wafanyakazi wote hawafanyi kazi kwenye utendaji unaoridhisha? nadhani kama kungekua na promotion kungeamsha hata hari ya wengine kufanya kazi than hii demotion ambayo mwisho wasiku itafanya watu wafanye kazi kwa uoga
 
Kutumbua ndio sera yao wakati wananchi mtaani hali ni mbaya wangejikita kuboresha huduma za jamii kwanza wamesahau mambo ya muhimu wao ni majipu tu.
 
Dah, yani vitoto vidogo na bachelor zao wamsimamisha hadi prof?
Kweli mamlaka si mchezoo!!!
 
Enzi zetu tulikuaga na Second Master yaani ikitokea Headmaster kasafiri hata siku mbili tu akirudi anakuta nusu ya shule mmepigwa suspension.... headmaster anaanza kuhangaika kuwarudisha...yule ticha angefaa sana kwenye hii serikali ya Magu...full kusimamishana kazi
 
Back
Top Bottom