Mkutano wa Umoja wa Afrika wavunjika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkutano wa Umoja wa Afrika wavunjika

Discussion in 'International Forum' started by Saint Ivuga, Jul 2, 2011.

 1. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #1
  Jul 2, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,276
  Likes Received: 19,427
  Trophy Points: 280
  Mkutano wa Umoja wa Afrika wavunjika
  [​IMG] Großansicht des Bildes mit der Bildunterschrift: Waasi nchini Libya

  Mazungumzo ya Umoja wa Afrika ya mpango wa kumalizia mgogoro nchini Libya yamevunjika mapema leo nchini Guinea ya Ikweta baada ya kutofikiwa makubaliano kuhushu hatima ya Muamar Gaddafi.

  Viongozi wa Afrika waliunga mkono mpango wao wa upatanishi wa mgogoro wa Libya katika siku ya kwanza kabisa ya mkutano huo hapo jana, ambao unafanyika katika mji mkuu wa Guinea ya Ikweta, Malabo.

  Mkutano huo wa vuta n'kuvute pia umehudhuriwa na pande zote hasimu nchini Libya, yaani utawala wa Gaddafi na Waasi. Hata hivyo, maafisa wanasema ungendelea tena baadae.

  Mpango huo wa upatanishi wa Umoja wa Afrika unajumuisha kusimamisha mapigano, misaada ya kiutu, kipindi cha mpito, mabadiliko kulekea demekrasia na uchaguzi, lakini ufafanuzi na nafasi ya Gaddafi katika masuala hayo haijawa wazi.

  Mwakilishi wa Baraza la Mpito la Waasi, Mansour Safy Al-Nasr, aliwaambia waandishi wa habari kwa upande wao bado unashinikiza kwamba Gaddafi aliyekuwa madarakani kwa zaidi ya miaka 40 aondoke.

  Mwakilishi hiyo wa waasi aliongeza kwa kusema kwamba Gaddafi mwenyewe anafikiri mgogoro huo utamalizika kisiasa au kijeshi, basi wao wako
  tayari kwa namna yeyote ile. Na kwamba Waasi hawatosalimu amri kwa wakati huu.

  Al-Nasr alisema kama operesheni za kijeshi zikisonga mbele na kuzunguka mji wa Tripoli, Gaddafi atakubali kuondoka madarakani. Hivi sasa amejitenga. na kudai yupo katika handaki lake, hana maisha, hawezi kwenda kokote.

  Nae mwenyekiti wa Baraza la Waasi, Mahmud Jibrir, ambae kwa hivi sasa yupo mjini Vienna, alisema anangoja msimamo wa wazi kutoka kwa Umoja wa Afrika kwama wanamuunga mkono au wanamlaani Gaddafi.

  Jibril aligusia kutolewa kwa waranti wa kukamatwa Gaddafi, akisema unaashiria kwamba mauwaji yamefanyika, kwa hivyo Umoja wa Afrika unapaswa kuwa wazi katika suala hilo.

  Umoja wa Afrika, kwa upande wao, umesema waranti huo uliotolewa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu unafanya mambo yawe magumu katika kufikia suluhisho la mgogoro wa Libya.

  Großansicht des Bildes mit der Bildunterschrift: Uwanja wa vita nchini Libya

  Pia umesema hali imekuwa tete na hasa Ufaransa ilipoanza kutoa silaha kwa waasi, ukiachilia mbali malalamiko ya mwanzoni kuhusu mashambulizi ya ndege za Umoja wa Kujihami.

  Wakati huo huo, mapambano yanaendelea nchini Libya. Taarifa za hivi punde zinaeleza kwamba waasi nchini humo wamejiondoa katika eneo la karibu na mji wa Bir al-Ghanam, huko kusini mwa Tripoli, baada ya kuvurumishiwa makombora ya mareketi na wanajeshi watiifu kwa Gaddafi
   
 2. T

  The Infamous JF-Expert Member

  #2
  Jul 2, 2011
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 719
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  umoja wa afrika unatapatapa kama mwanamke anaetafuta bwana...hauna maamuzi
   
 3. Somoche

  Somoche JF-Expert Member

  #3
  Jul 2, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 3,823
  Likes Received: 922
  Trophy Points: 280
  Mimi wananikera hawa viongozi wa Afrika ni waoga na wanafiki wakubwa kila mtu anajifunika kama kifaranga kisa haya mabeberu wanayaogopa...lakini wangekua na umoja hawa wazungu wangeogopa...ama kweli naamini bora masikini wa mali kuliko akili
   
 4. Ami

  Ami JF-Expert Member

  #4
  Jul 2, 2011
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 1,858
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Tatizo vyombo vya kikachero vya nchi za magharibi zipo katika kila mimoja.Hivyo si rahisi kupatikana mwafaka katika mikutano hii.Hawa jamaa wamo ndani ya OIC,ndani ya Umoja wa nchi za kiarabu na kila kitu.Ukiangalia rasimu ya OIC imejaa mambo ya kijinga ambayo uislamu hauyatambui.
  Nakumbuka katika mkutano fulani Iblisi alijipeleka bila kualikwa.Akavaa kanzu na kilemba saafi kabisa sawa na wajumbe waalikwa.Agenda ikielekea huku anairudisha kule.Ikionekana kuungwa mkono anaibeza,hivyo hivyo mpaka mwisho.Wajumbe wakashindwa kupata muafaka kwa vile walipoteza muda mwingi kumsikiliza Iblisi kutokana na utanashati wake.
   
 5. POSHO MAVYEO

  POSHO MAVYEO JF-Expert Member

  #5
  Jul 2, 2011
  Joined: Jun 28, 2011
  Messages: 377
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Udini utawamaliza walibya wao wanashinda porini /jangwani wakipigania haki zao nyie mnaleta udini na laptop zenu
   
Loading...