Mkutano wa G7 utafanyika kupitia video

Mkutano wa G7 utafanyika kupitia video

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,286
Reaction score
10,831
Rais wa Marekani Donald Trump amefuta Mkutano wa viongozi wa mataifa 7 tajiri dunaini G7 na badala yake watazungumza kwa njia ya vidio kutoa fursa kwa viongozi kushughulikia mpripuko wa maambukizi ya virusi vya corona katika nchi zao.Mkutano huo uliokuwa uwakutanishe viongozi wa mataifa ya Canada, Ufaransa, Ujerumani, Japan, Italia, Uingereza na Marekani ulikuwa ufanyike mnamo mwezi Juni katika jimbo la Marekani la Maryland.

Trump pia atakutana na viongozi wa mataifa hayo saba kwa njia ya video mnamo mwezi Aprili na Mei baada ya viongozi hao kufanya mkutano kuhusu mripuko wa virusi vya corona wiki hii.Kwa hali inavyoendelea, serikali ya Trump inaamini mripuko wa virusi vya corona utaendelea kuwa na athari ulimwenguni hadi majira ya joto

DW Swahili
 
Ata ule wa secretariate ya mawaziti wa Sadeki umefanyika hivi hivi majuzi. Waziri mkuu wetu ndiye alifungua.
 
Ivi Italy na Russia Nani Yuko juu ya mwenzie.....????? Huu umoja Ni mfu ..uundwe mwingine kutokana na mazingira ya sasa
 
Ivi Italy na Russia Nani Yuko juu ya mwenzie.....????? Huu umoja Ni mfu ..uundwe mwingine kutokana na mazingira ya sasa
Italy ipo juu kiuchumi.

Russia alifukuzwa uanachama (wakati huo ikiitwa G 8) baada ya kuitwaa Crimea kutoka Ukraine kwa nguvu.

Upo Umoja wa G 20 ambao kuna nchi hizo tajiri na zinazoinukia kwa Kasi huenda huo ndio mbadala.

Pia Kuna ule wa mataifa yanayoinukia kwa Kasi (Bricks) unaongozwa na China, Brazil,India, Russia, Africa Kusini sema bado haujawa na nguvu za kuitwa mbadala wa G 7 japo wanajitutumua.
 
Back
Top Bottom