Elections 2010 Mkutano wa dr w slaa arusha

Tuwe macho sana na mbinu za CCM za kuvuruga amani. Mliona jinsi vibaraka wa Chenge walivyojaribu kuvuruga mkutano wa CHADEMA.

CCM wakiona wanazidiwa, wataanza Plan B yao ambyo ni VURUGU. Wamezoea kuhodhi madaraka. Na kati yao wapo mafisadi wengi sana ambao wanaogopa CHADEMA ikishinda Urais wanaweza kuajibishwa. Tuwe macho nao. Kati yao kuna waliopata shinikizo la damu kwa kuangalia mambo yalivyokuwa Arusha. Na wanajua hakuna HONGO iliyotumika kufanya watu waje.


Tumechoka utawala usio na ahueni wa CCM. Sasa tunataka mabadiliko.
 
Amesema akiwa rais atahakikisha bei ya bati na cementi inachuka mpaka chini ya 5000 iliwatu waweze kujenga nyumba za kudumu, serikali yake haitakuwa na anasa kama ya ccm, na wafujaji wa mali za serikali hatacheka nao ni kuwakamata na kuwapeleka mahamani....

Mungu amjaalie huyu mkombozi wa taifa hili linalotafunwa na mchwa walafi, hakika nguvu ya umma itathibitika..inshaallah
 
Dr. anasema kuwa zinatakiwa kujengwa ofisi za wabunge na makadirio ya ujenzi ni kati ya milioni 40 na 50. LAKINI KWA KUWA SITTA ALIKUWA SPIKA YEYE AKAENDA KUJENGA OFISI YA SPIKA KWA MILIONI 500. INA MAANA MWAKANI AKIJA SPIKA MWINGINE TUSEME AKATOKA JIMBO LA KIGAMBONI BASI NAYE ATAJENGA OFISI YAKE YA SPIKA KIGAMBONI. na huu ni UFISADI (ubadhirifu) kwa kuwa-
1. Aijawahi kutangazwa tenda kwa ajili ya huo ujenzi.
2. Fenicha ni za milioni 150( nazani zitakuwa za marumaru toka ITALY)
3. Milioni 500 zinatosha kujenga zahanati 10 au madarasa 70, Embufikiria wana Urambo leo wangejengewa hizo zahanati 10 au hayo madarasa 70( ambayo ni sawa na shule kumi za msingi, sekondari za kidato cha nne 27) embu fikiria vijiji vingapi vinge nufaika na hizo hela?

Kweli tuhitaji wahisani kutuambia hili au kutambua hili?
 
Back
Top Bottom