Mkutano wa Contractors, Karimjee Hall Dar es Salaam!

Mkutano kwa leo umehitimishwa, utaendelea kesho kuanzia saa mbili kamili asubuhi!
 

Mkuu ni imani yangu hata kesho utatupa updates, kwani tungependa sana kuwepo hapo lkn kwasababu zilizo nje ya uwezo wangu nimeshindwa.
 
Mkuu ni imani yangu hata kesho utatupa updates, kwani tungependa sana kuwepo hapo lkn kwasababu zilizo nje ya uwezo wangu nimeshindwa.
Ondoa shaka mkuu, timu ya YECCO (T) LTD itakuwa eneo la tukio kuanzia saa mbili asubuhi kukupa yanayojiri hatua kwa hatua,


Kwa mahitaji ya:

Building & Civil Works Contractor, Electrical Contractor, Electrical Plan, ICT & Clearing & Forwarding

Wasiliana nasi kwa:
+255 715865544
+255 755865544
Barua pepe ni:
yeccotltd@yahoo.com

Au fika katika Ofisi zetu zilizopo Mtaa wa Samora,Posta,DSM
Coronation House gorofa ya Pili, Chumba na 12 kulia! Jirani na BAKITA!


Kwapamoja tutalijenga Taifa!
 
Habari za asubuhi wapendwa wateja wetu na watanzania wote, mkutano wetu wa CRB unaendelea leo ikiwa ndio hitimisho, endelea kufuatilia hapa!
 
Mabadiliko ya Ukumbi, leo tutakuwa makumbusho ya taifa jirani na chuo cha usimamizi wa Fedha (IFM)

Mkutano umeanza kwa salaam,

Hehee Eng Magesa ameanza kusalimia kisha akatania kwa kusema Kidumu chama Cha mapinduzi! Watu wakazomea hooooooo!
 
Hivi MECCO bado ipo? Kama ipo inafanya nini? Naona kila mradi mkubwa wa ujenzi unafanywa kwa asilimia 100 na makampuni ya nje. Kama nchi ingekuwa busara kuwa na kampuni kadhaa kubwa ambazo zitahusishwa na ujenzi wa maeneo nyeti. Mfano haitakuwa busara kama kampuni ya nje itajenga daraja la kigamboni kwa asilimia 100. Tungeweza kuwalazimisha kufanya kwa ubia na kampuni kama MECCO kama ingelikuwa hai.
 
Sasa anaanza kutoa mada mwakilishi wa benki ya biasha ya Afrika ACB Bibi Fatuma Abdala,

ACB hatuhitaji dhamana kumkopesha mkandarasi,

Utaratibu ni:
1)Class 1 atakopeshwa hadi milioni 700

2)Class 2 atakopeshwa hadi milioni 500

3)Class 3 atakopeshwa hadi milioni 300

4)Class 4-7 atakopeshwa hadi milioni watapewa kulingana na class limit zao!

Hii haiko ktk benki yoyote!

Pia mkandarasi akihitaji kununua mitambo takopeshwa bila riba wala dhamana yani ile mitambo itakuwa ndio dhamani halisi, itatolewa leseni ya majina mawili ya ni Mkandarasi na Benki ya ACB
 
UPDATES:

Mwakilishi wa NBC ndugu. Dastan Kolimba anaanza kutoa mada:

Sisi maranyingi tumejikita ktk ushauri wa kitaalam wa kifedha na malipo yenu kuko kwenye sekta yenu!

Mtaji uutafutao uwe mahususi kwa mradi uliokusudiwa,

Makandarasi muondokane na utamaduni wa zamani,
Benki yetu ya NBC itakusaidia kupata fedha ikiwa umelipwa pesa lakini bado huja ishika mkononi yani pesa hiyo bado ipo kwenye mchakato wa kibenki, mfano umelipwa cheki yenye kuchukua siku 4 ndipo ikufikie basi NBC watakupa hela hiyo siku hiyohiyo ukienda na cheki hiyo hata kama ni ya benki nyingine!

Naam sasa ni nyakati za maswali na majibu

Swali: Pamoja na maneno mazuri ya CBA lakini maranyingi vitengo vyenu vya biashara na mikopo vimekuwa kikwazo kwa sisi makandarasi hasa kwenye dhamana na mengine, je unatuahidi nini kwa hilo?

Swali 2: Kwakuwa mabenki karibu yote yana hadithi zinazofanana, mnatuhakikishiaje utimizwaji wa ahadi hizo?

Swali 3 Limekataliwa baada ya muuliza swali kuingiza uchama kwa kusema, "mimi ni mkandarasi na mwenyekiti wa ccm Tarime" hapa makandarasi wamecharuka kwa kupiga mayowe na kuzomea ndipo mwenyekiti wa mkutano huu kulikataa swali hilo na kumtaka mwenyekiti huyo kukaa chini!

Sasa ni nyakati za majibu!

Jibu: CBA tunawaahidi kuwa ukija kwetu tutakuhudumia kwa mda wa mwezi mmoja tu!

Jibu: CBA itatoa mkopo hata kama huna akaunti ila tutahitaji maelezo ya benki ya akaunti zako, (bank statements)

Pia tumeingia makubaliano (MoU) na Tanroads ili sisi CBA tuweze kuwadhamini na kuwalipa madeni yenu na kuondokana kwa ucheleweshaji wa malipo yenu!

Interest rate ya mikopo yetu itaendana na aina ya mkopo wa mkandarasi
Hatuwezi kuweka uwiano sawa kati ya class 1 na 7


Asante sasa ni mapumziko tutarejea baadae!
 
UPDATES:

Baada ya mapumziko, sasa tunaendelea na msemaji ni Eng Stella Manyanya mkandarasi, mbunge, na mkuu wa mkoa!

Eng Manyanya:
Mimi nikiwa kama mkuu wa mkoa na mkandarasi ninawakaribisha mje kuwekeza mkoani Rukwa, tenda zipo na nitawasimamia ipasavyo makandarasi wa ndani,

Rukwa kuna fursa nyingi za uwekezaji katika ujenzi na utalii hasa maporomoko yaliyopo huko!

Nimefrahi kukutana na makandarasi wenzangu hasa ktk makutano mazuri kama haya!

Asanteni sana kwa kunisikiliza!
 
UPDATES:

Maadhimio ya Makandarasi:

Tunaomba CRB na OSHA wasimamie na kutoa elimu juu ya uzingatiaji wa sheria za ukandarasi kwa ujumla,

Makandarasi tufungue benki yetu itakayotusaidia kupata mikopo kirahisi na kwa riba ndogo zaidi!

Kwenye evaluation wawepo watu wa ppra ili haki ziwe zinatendeka kumpata mshindi halisi!

Sub Contractor nao waingie kwenye mfumo wa ppra ili washindane kupata tenda kuliko ilivyo sasa man contractors kujichagulia sub wa kufanya nae kazi!

CRB itengeneze vitabu vya sheria na kanuni za utekelezaji wa sheria ya OSHA, lakini ziwepo za jumla na sheria zile zitakazohusu mradi husika na mkandarasi apewe kitabu hicho kila akisajili mradi!

CRB itoe kwanza mafunzo kwa makandarasi kabla ya kusajiliwa

CRB waongeze idadi ya wafanyakazi ili waweze kuifikia miradi yote hata iliyopembezoni mwa miji, na ikiwezekana waweke mawakala wa kusimamia!

Tovuti ya CRB iwe updates mda wote na iweke haya mafunzo yote kwenye tovuti hiyo

Idadi ya taasisi zinazotoa vibali vya ujenzi ni nyingi tunaiomba serikali ipunguzi taasisi hizi na ikiwezekana mambo yasimamiwe na CRB na ERB tu, mfano upataji wa vibali vya ujenzi kwenye halmashauri zetu ni ngumu sana hivyo humpotezea mda mwingi mkandarasi kufuatilia vibali hivyo!

Makandarasi tuhakikishe tunakuwa na wafanyakazi wakudumu na kepuka kasumba ya kumuajiri mtu pindi uwapo na mradi tu!

Kila mkandarasi azingatie kuweka uzio kila sehemu anayokuwa na project ili kuweka usalama wa site yake!

Makandarasi tuwe makini kwenye kutenda tenda zetu ili kuepuka kupata hasara na kufilisika
 
Eng Muhegi:

Kuanzia sasa ilikusajili mradi sio lazima uwe na kibali cha ujenzi,

Kibali utakileta ikiwa eneo unalojenga limepimwa na unacho,

Kila mradi unaoufanya njooni muusajili ili serikali ipate takwimu na itawasaidia nyinyi mkitaka kupanda madaraja yenu!
 
UPDATES:

Mgeni rasmi ndio anaingia ni Naibu Waziri wa Ujenzi Eng: Gerson Lwenge

Msajili wa CRB anamkaribisha Naibu Waziri

N.Waziri:

Kwa kazi zinazogarimiwa na fedha ya ndani hasa za mfuko wa barabara serikali imeamua zifanywe na makandarasi wa ndani (wazalendo)

Zingatieni kuwa mkibebwa bebekeni, msiwe kama kinyonga

Tunatambua kuwa nchi haiwezi kuendelea bila ninyi!

Tunasikitika sana kuona kazi nyingi kubwa zikifanywa na wageni, hivyo tunaomba mjiandae kufanya kazi za kiwango bora sawa na wageni au hata kuwazidi!

Tunataka kondoa suala la turn over lisiwe kikwazo kwenu kupata miradi mikubwa!

Tunataka kuona leo mkandarasi wa ndani akifanya mradi wa bilioni 300 au zaidi na hili litawezekana kwa kurekebisha sheria zetu na nyinyi wenyewe kuwa tayari!

Ninaimani bodi pamoja na nyinyi wenyewe ikiwa mtayatekeleza mliyokubaliana, malengo mtayafikia

Na ninawaomba makandarasi muungane (JV) ili muweze kufanya miradi mikubwa zaidi inayofanywa na wageni na itakuwa rahisi kwenu kupata mikopo!

Mwisho nawaomba makandarasi muache kutoa rushwa ktk kazi zenu!

Natangaza kuufunga rasmi mkutano huu

Asanteni sana niwatakie mafanikio meme kulijenga taifa letu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…