Mkutano wa CHADEMA Wafana CHALINZE.

Mkutano wa CHADEMA Wafana CHALINZE.

Richard Robert

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2012
Posts
632
Reaction score
340
Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Pwani Bwana Said ukwezi ameongoza jopo la viongozi wa mkoa, wilaya na majimbo ya Pwani kuhutubia wanachama na wakazi wa CHALINZE waliojitokeza kwa wingi kusikiliza hotuba za viongozi wao.

Mkutano huo umefanyika katika viwanja vya TANESCO opposite na njia panda ya Tanga. Lengo la mkutano huo lilikuwa kuwaandaa wananchi kuzipokea harakati za M4C kwa mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.

Awali baadhi ya vijana, wanawake na wazee waliwaomba baadhi ya viongozi wa CHADEMA wasikilize kero zao ambazo wao kama wapiga kura wanataka CDM izipigie kelele na baadaye 2015 izitatue baada ya kuingia madarakani, kama vile:
1. Migogoro ya ardhi - hali ambayo inatishia usalama wa taifa siku za usoni;
2. Huduma za afya - hazipo na ndogo zilizopo hazitunzwi vizuri.
3. Taaluma mbovu mashuleni - hali mbaya ya matokeo ya kidato cha nne.
4. Vitisho vya CCM hadi kuwafanya waishi kinafiki kwa kuweka bendera za CCM ktk biashara zao.
5. Kukosa soko, stendi na mpangilio mbovu wa mji.
6. Michango mingi shule za msingi hasa shule ya msingi pera ambako wazazi hutozwa laki 2. P1010477.JPGP1010451.JPGP1010458.JPG
 
Richard Robert

Hakika umesomeka! Je? Mkutano itakuwa ni lini?
Viongozi wa chama watakaokuwepo ni akina nani?
Hebu funguka kidogo Kamanda wetu Richard Robert

Viva Chama makini kwa wananchi wake

CHADEMA
 
Last edited by a moderator:
Richard Robert

Hakika umesomeka! Je? Mkutano itakuwa ni lini?
Viongozi wa chama watakaokuwepo ni akina nani?
Hebu funguka kidogo Kamanda wetu Richard Robert

Viva Chama makini kwa wananchi wake

CHADEMA

Mkuu mkutano huu umefanyika leo. Hapa nilipo leo (Msata) mtandao unasumbua picha za mkutano nashindwa kuwaleteeni.
Mikutano ya vijiji kwa vijiji inaendelea wiki nzima. Mikutano mikubwa itakuwa jumamosi tarehe 23/3/2013 - Magomeni, Bagamoyo na tarehe 3/4/2013 To top, Bagamoyo.

M/kiti CDM (w) Bagamoyo).
 
hakika tutashinda zaidi yA UHURU
 
Back
Top Bottom