Mkutano wa CHADEMA na Waandishi wa Habari katika ofisi za Makao Makuu ya chama, Kinondoni

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
C7q2_GMU8AEU3PX.jpg






Mnyika: Mwenyekiti, Freeman Mbowe, alifanya kikao cha Halimashauri Kuu maalum juzi na jana. Bahati mbaya Leo kaenda Tanga.


Mkutano ulikuwa na agenda mbili, kwanza kuhusu wagombea ubunge wa Bunge la Afrika mashariki kupitia CHADEMA.

Agenda ya pili ya Mkutano ni kuhusu yanayoendelea katika taifa letu likiwemo la uvamizi Clouds na kutenguliwa kwa Nnape

J. Mnyika: Uvamizi wa Clouds Media na Kutenguliwa kwa Nnauye Nape ni matumizi mabaya ya Rais na Jeshi la Polisi.

J. mnyika: Kama Chama, tunamtaka Rais Magufuli ahakikishe anamchukulia Makonda hatua kwa sababu ya vyeti feki na kuvamia Clouds Media.

J. mnyika: Chadema tunamtaka Rais Magufuli atoe sababu halisi za kumtengua uwaziri Mh. Nnape

 

Attachments

  • VID-20170324-WA0044[1].mp4
    13.4 MB · Views: 62
Mkuu hii ni kama kulogwa hivi kwa watanzania, kuanzia taifa halina dira yani ni mzobemzobe tu ni kama gari limekatika break vile mnafikiri hayo maendeleo yatatoka wapi!?
Sasa na vyama tena chakuskitisha zaidi hata upinzani hakuna agenda!
Hivi upinzani una agenda gani kwa sasa?
Yani ni kwenda na matukio tu leo hili badaye limepotea litakuja tukio lingine, kesho tena hii haitotufikisha popote.
Pasipo kuwa na dira/agenda kuanzia taifa na hata kwenye hivyo vyama vya siasa ni kazi bure.

Dr. Martin Luther King Jr. alikuwa akisema ni lazima uwe na kitu ambacho unakiamini, unakisimamia na kupigania na ukubali hata kufa hapa siyo kwa maneno tu na yaga yaga, ni kwa vitendo na hii inaanzia kwa mtu mmoja mmoja na hata taasisi zinajengeka kwa misingi hii.

“A man who does not have something for which he is willing to die is not fit to live.”
 
C7q2_GMU8AEU3PX.jpg






Mnyika: Mwenyekiti, Freeman Mbowe, alifanya kikao cha Halimashauri Kuu maalum juzi na jana. Bahati mbaya Leo kaenda Tanga.


Mkutano ulikuwa na agenda mbili, kwanza kuhusu wagombea ubunge wa Bunge la Afrika mashariki kupitia CHADEMA.

Agenda ya pili ya Mkutano ni kuhusu yanayoendelea katika taifa letu likiwemo la uvamizi Clouds na kutenguliwa kwa Nnape

J. Mnyika: Uvamizi wa Clouds Media na Kutenguliwa kwa Nnauye Nape ni matumizi mabaya ya Rais na Jeshi la Polisi.

J. mnyika: Kama Chama, tunamtaka Rais Magufuli ahakikishe anamchukulia Makonda hatua kwa sababu ya vyeti feki na kuvamia Clouds Media.

J. mnyika: Chadema tunamtaka Rais Magufuli atoe sababu halisi za kumtengua uwaziri Mh. Nnape

Wewe huwezi kuleta habari kama hii itakuwa account yako imedukuliwa sio wewe huyu..
 
Daaah...mnasikitisha HIVI nyie kinawauma VIpi NAPE kuondolewa UWAZIRI?????......
Why not KITWANGA povu halikuwatoka?????.....Ebu kwenye hivyo vikao vyenu muwe mnajadili mambo ya MAAANA.....yapo mengi mno...msikalie kula ruzuku ya chama kupitia hivi vikao...
MBNA WAKATI ana mchagua HAMKUULIZA kwanini AMEMCHAGUA NAPE???????
Hapa semeni ajenda yenu ni KUJIKOMBA KWA NAPE ili aje upande wa PILI na hilo msahau NAPE atapigana humo humo ndani ya CCM kamwe hawezi HAMA CHAMA.....na kusema mnaamnisha mnachokisema HAPA huo ni UZUZU.......mnashindwa kuhoji ALIPO SAANANE mnakuja KUTOA matamko yasikuwa na AFYA KWENYE CHAMA CHENU.......
 
C7q2_GMU8AEU3PX.jpg






Mnyika: Mwenyekiti, Freeman Mbowe, alifanya kikao cha Halimashauri Kuu maalum juzi na jana. Bahati mbaya Leo kaenda Tanga.


Mkutano ulikuwa na agenda mbili, kwanza kuhusu wagombea ubunge wa Bunge la Afrika mashariki kupitia CHADEMA.

Agenda ya pili ya Mkutano ni kuhusu yanayoendelea katika taifa letu likiwemo la uvamizi Clouds na kutenguliwa kwa Nnape

J. Mnyika: Uvamizi wa Clouds Media na Kutenguliwa kwa Nnauye Nape ni matumizi mabaya ya Rais na Jeshi la Polisi.

J. mnyika: Kama Chama, tunamtaka Rais Magufuli ahakikishe anamchukulia Makonda hatua kwa sababu ya vyeti feki na kuvamia Clouds Media.

J. mnyika: Chadema tunamtaka Rais Magufuli atoe sababu halisi za kumtengua uwaziri Mh. Nnape

Kweli Chadema mmechoka. Hivi teuzi za Rais tena siyo wa chama chenu zawawashia nini.

Kama kachemsha si ndo mlo kwenu?

Tangia lini mmekuwa washauri wake?

Hivi ya Nape mmeyasahau au tuwakumbushe?

Anaandika Dr.Christopher Cyrilo (MD).
____________________
Pongezi kiduchu zimfikie Nape Nnauye kwa kuonesha kuwa kinyume na ufedhuli, lakini pongezi hizo kiduchu na hatua yake ya kuwa kinyume na ufedhuli, havifuti ufedhuli wake. (Nape ni fedhuli anayevuna alichopanda).

Kwa maneno machache tu;

1. Nape na vijana wenzake wa CCM ndio waliozunguka nchi nzima kumtukana Lowassa, ambaye wakati huo alikuwa moja kati ya watu muhimu ndani ya Chama chao. Lakini kwa sababu ya kutumikia makambi na makundi ya chama, wakazunguka kutukana na kupakaza uongo kwa manufaa ya kundi fulani.

2. Nape ndiye aliyetangaza ushindi wa CCM hata kwa goli la mkono, akijua kabisa ni kinyume cha demokrasia.

3. Nape ndiye aliyewatolea maneno machafu waangalizi wa kimataifa wa uchaguzi mkuu mwaka 2015, waliodai uchaguzi ulikua na mapungufu mengi.

4. Nape ndiye aliyetangaza kulifungia MILELE gazeti la Mawio, kwa madai ya uchochezi, kwa sababu tu liliandika habari zisizowafurahisha watawala.

5. Nae mdiye aliyelifungia gazeti la Mseto kwa miezi 36 (miaka mitatu) kwa madai ya kuandika habari zenye kumchafua Naibu waziri wa Ujenzi Edwin Ngonyani.

6. Nape ndiye aliyefungia Radio Magic Fm na Radio Five Arusha kwa madai ya uchochezi, kisa tu radio hizo zilikua zilitoa nafasi kwa viongozi wa upinzani kuongea na wananchi.

7. Nape ndiye aliyewasilisha hoja bungeni ya kufuta bunge Live, na kuwanyima wananchi haki yao ya msingi ya kufuatilia kazi za viongozi wao bungeni.

8. Nape ndiye anayedaiwa kuagiza Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Lindi Selemani Mathew afungwe gerezani kwa kufanya mkutano bila kibali, kwa sababu Mathew alimshinda kwenye kura za maoni jimbo la Mtama mwaka 2015 akakatwa, na kwenda Chadema.

9. Nape akiwa Katibu Mwenezi wa CCM ndiye aliyesema CCM haiwezi kuondolewa madarakani kwa vipande vya karatasi.

10. Nape ndiye aliyetengeneza propaganda ya kusema Lowassa ni mgonjwa na hafai kuwa Rais. Propaganda hiyo ilitumika na viongozi wa CCM kumchafua Lowassa na kumpunguzia kura.

11. Nape akiwa mkoani Ruvuma kwenye ksmpeni za uchaguzi, alimuita Magufuli Rais hata kabla ya uchaguzi. Yani alijiona kama Mwenyekiti wa Tume ya ucjaguzi mwenye uwezo wa kupanga matokeo na kuamua nani awe kiongozi.

12. Nape akiwa Katibu Mwenezi wa NEC na mjumbe wa Kamati Kuu ndiye aliyewasilisha azimio kwenye Kamati ya maadili la kumkata Lowassa katika hatua za awali za mchujo. Azimio hilo liliungwa mkono na wajumbe wengine na Lowassa hakupita hata kwenye 5 bora.

13. Nape ndiye aliyeshawishi wafuasi wa Lowassa waliobaki CCM watimuliwe akiwemo Mhe.Sophia Simba ambaye amevuliwa uanachama na kupoteza ubunge wake na uenyekiti wa UWT.

14. Nape ndiye aliyekuwa injinia wa kupitisha muswada wa sheria mbaya kuliko zote ya habari, ambao tofauti na lengo linaloelezwa, ukiisoma sheria ile na kuielewa, utagundua sio tu inaminya uhuru wa kupashana habari lakini pia inapingana na stratejia za kupambana na ufisadi, stratejia ya 'Whistle blower policy' inayotajwa kuwa bora kabisa katika kupamabana na ufisadi, inawekewa ukinzani na sheria ya Habari ambayo Nape alihusika moja kwa moja katika kuipitisha.

15. Nape ndiye aliyepigania sheria ya mitandao ipitishwe akiwa Katibu Mwenezi wa CCM ili kuzuia nguvu ya vijana wa upinzani kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

16. Nape ndiye ameongoza juhudi za waandishi kunyanyaswa, kupuuzwa na kudharauliwa. Hakuna kipindi waandishi wameishi kwenye mateso kama kipindi cha utawala wa Nape.

17. Nape ndiye aliyewasilisha hoja bungeni ya kutaka vyombo vyote vya habari (Radio na TV) vijiunge na TBC kila siku saa 2 usiku kwa ajili ya taarifa ya habari.

18. Nape ndiye aliyepitisha muswada wa habari (ambao kwa sasa ni sheria) ya kulazimisha waandishi wote wa habari kuwa na degree moja kabla ya mwaka 2021. Mwandishi ambaye hatakuwa na degree wakati huo HATATAMBULIKA kama mwandishi wa habari.

Huyo ndiye Nape Moses Nnauye ambaye leo kuna watu wanamuona shujaa, kwa sababu amevuliwa uwaziri. Hivi yeye ni mtu wa kwanza kuvuliwa uwaziri? Mgogoro wake na Makonda haumfanyi kuwa shujaa.

Kuna watu wanasema ni shujaa eti kwa sababu ya kuunda kamati ya Uchunguzi uvamizi wa Clouds. Lile ni jukumu lale kama Waziri. Na asingefanya hivyo umma ungemiwajibisha. Sasa mnamuonaje shujaa mtu aliyetimiza wajibu wake? Hivi housegirl wako akideki nyumbani utamuona shujaa wakati ametimiza wajibu wake?

Labda tumpongeze kwa ujasiri wa kujitokeza hadharani na kupinga udikteta wa Rais wake. Udikteta ambao Lissu ameupinga kwa muda mrefu. Wakati akina Lissu wanaongea akina Nape walidhani hawahusiki, kwa hiyo wakakaa kimya. Leo yamewakuta wanataka kufanya ni msiba wa kitaifa.

Yani wakati Lema anakamatwa na kudhalilishwa akina Nape walikaa kimya. Lissu kukamatwa na kudhalilishwa Nape kimya. Vijana wa upinzani kunyanyaswa, kupigwa (refer Mdude), kufungwa magerezani (refer Mwaifunga) na wengine kupotezwa (refer Ben Saanane) Nape na wenzie walikaa kimya kama vile hayawahusu, leo yamemkuta yeye anaonekana shujaa?

Ukweli ni kwamba Nape hajawahi kuwa mtu muhimu kwa taifa, bali amekuwa mtu muhimu sana kwa CCM. Ameisaidia CCM, ameipigania CCM alijitoa kwa ajili ya CCM. Alifanya kila aliloweza kuhakikisha CCM inabaki madarakani. Nape, January na Mwigulu ndio waliomuweka JPM madarakani kwa kutumia mbinu halali na haramu. Bila hawa watu watatu pengine tungekuwa tunsongea mengine kwa sasa.

Kwahiyo kinachomtokea Nape ni matokeo ya kile walichokitengeneza wenyewe. Anavuna matunda ya ufedhuli wake. Nape kafanya uovu mkubwa sana kwenye nchi hii ili kuisaidia CCM. Ni uovu wenye manufaa kwa CCM, sio kwa Taifa.

Kwa hivyo, ikiwa Nape anahitaji huruma, basi atahitaji zaidi kuonewa huruma na a wanaCCM wenzake kuliko watanzania aliowanyanyasa, kuwakebehi na kuwadharau kwa muda mrefu.

Ushauri wa bure: Nape kama mwanasiasa mwingine yeyote ana tamaa ya madaraka makubwa zaidi kuliko aliyowahi kushika. Kwahiyo ni veama akawa mkimya kwa kipindi hiki kuliko kipindi chochote kile. Akae kimya, arudi kuwatumikia watu wa Mtama. Asome kitabu cha Robert Green; 48 laws of power, aangalie amekosea wapi.

Zaidi ya hayo, amtafute mzee Lowassa amuombe msamaha na kuomba somo zaidi la siasa. Ajifunze kwa nini Lowassa bado ni mtu mwenye ushawishi mkubwa pengine kuliko aliyemteua na kumtumbua. Alamsiki.!

Dr.Chiss Cyrilo, 23/03/2017.
 
Daaah...mnasikitisha HIVI nyie kinawauma VIpi NAPE kuondolewa UWAZIRI?????......
Why not KITWANGA povu halikuwatoka?????.....Ebu kwenye hivyo vikao vyenu muwe mnajadili mambo ya MAAANA.....yapo mengi mno...msikalie kula ruzuku ya chama kupitia hivi vikao
Kwa hiyo alikuwa wa Waziri wa Habari.....wa Lumumba pekee!
 
Chadema siku hz wamekosa cha kufanya, yaani waziri wa ccm amefukuzwa na mwenyekt wa ccm lakini wanalalamika!
Kama Taifa Nape Alikuwa Waziri.
Waziri ni Kiongozi Mkubwa Anapotenguliwa Kwenye Nyadhifa yake Wanachi Lazima Tujue Sababu za Kutenguliwa Kwake ili Alina Itikadi Au Wewe Unajua Sababu ya Nape Kutenguliwa Uwaziri?
 
Back
Top Bottom