ACT Wazalendo
JF-Expert Member
- May 5, 2014
- 620
- 1,543
MKUTANO MKUU WA KIDEMOKRASIA WA MIAKA 50 YA AZIMIO LA ARUSHA.
Chama cha ACT Wazalendo kinakukaribisha Ndugu mwananchi kushiriki katika Mkutano Mkuu Maalumu wa Kidemokrasia utakaofanyika Jumamosi 25/03/2017 katika ukumbi wa Corridor Springs Hotel jijini Arusha.
Mkutano huu ni wa kikatiba na unahudhuriwa na wanachama, wasiowanachama, wadau wa siasa, asasi za kijamii na wananchi wa kawaida.
Miaka 50 tangu kupitishwa Azimio la Arusha ni kipindi muafaka cha kujitathmini kama Taifa.
Pamoja na changamoto zake Azimio la Arusha lilikuwa na mema yake ikiwemo misingi ambayo liliipanda ili kuipa nchi uelekeo sahihi.
Utu, Uwazi, Uwajibikaji, Haki, Uadilifu, Uzalendo, Udugu, Umoja na Mshikamano ni baadhi ya misingi hiyo.
Kupitia Mkutano Mkuu Maalumu wa Kidemokrasia wajumbe watapata fursa ya kujadili, kutathmini na kuangazia kwa undani hatua tulizopitia kama Taifa kwa kipindi hiki cha miaka 50 wapi tulifanikiwa, wapi tulikosea, nini kilisahaulika, kipi kiongezwe ili tuweze kutatua changamoto anuwai zinazotukabili kama Taifa katika zama za sasa za Siasa za Kidemokrasia.
Ni fursa pia kupitia Mkutano huu Maalumu watanzania kuchambua hali ya kisiasa, kiuchumi na kijamii ya nchi na kutoa mapendekezo sahihi ya namna bora ya uendeshaji wa Nchi na ushirikishwaji wa wananchi kufikia malengo tunayokusudia.
Mkutano huu utarushwa mubashara kupitia kituo cha Luninga cha Azam Tv.
Thibitisha leo ushiriki wako kupitia namba zifuatazo:-
+255 715 800927
+255 719 847032
Nyote Mnakaribishwa.
ACT Wazalendo, Taifa Kwanza!