MKUTANO MKUU WA KIDEMOKRASIA NI WA WOTE!

ACT Wazalendo

JF-Expert Member
May 5, 2014
620
1,543
MKUTANO MKUU WA KIDEMOKRASIA NI WA WOTE!
Kwenye vyama vya siasa duniani, kuna Mkutano Mkuu na Mkutano Mkuu wa Kidemokrasia. Hapa nchini, mbali na ACT Wazalendo, vyama vingine vina Mkutano Mkuu pekee, havina Mkutano Mkuu wa Kidemokrasia.
Mkutano Mkuu huwaleta wanachama kujadili mambo ya Chama, tena una wajumbe maalum (Wajumbe wa Mkutano Mkuu). Kinyume chake, Mkutano Mkuu wa Kidemokrasia ni wa wote, wanachama na wasio wanachama; hauna wajumbe mahsusi! Mkutano Mkuu wa Kidemokrasia haujikiti kwenye kujadili Chama. Badala yake, mijadala kwenye Mkutano Mkuu wa Kidemokrasia huangazia masuala ya maendeleo ya nchi na dunia. Hata watu wasio wanachama hupata nafasi ya kutoa mada na kuchangia. Ndiyo maana kwenye Mkutano Mkuu wa Kidemokrasia wa Mwaka 2016 uliofanyika Makumbusho ya Taifa, Dar es salaam watu kama akina Deus Kibamba wa Jukwaa la Katiba waliwasilisha mada. Pia, wawakilishi wa Taasisi mbalimbali za ndani na nje ya nchi ambao si Wana-ACT walishiriki na kuchangia mjadala.
Tarehe 25 Machi 2017, ACT Wazalendo itafanya Mkutano wake Mkuu wa Kidemokrasia ambao kama ilivyo ada unawapa fursa watu wote kushiriki.
Mkutano utafanyika kwenye Hoteli ya Corridor Springs, Arusha kuadhimisha miaka 50 ya Azimio la Arusha
Wananchi wote wanaopenda kushiriki kwenye Mkutano Mkuu wa Kidemokrasia watume majina yao kwa baruapepe: actwazalendo15@gmail.com au Kwa namba zifuatazo:
1. 0719847032
2. 0717047574

Wenu, Ndugu Ado Shaibu
Katibu wa Itikadi na Uenezi-ACT Wazalendo
05973d73e800f117d45c72e6923f6255.jpg
 
Back
Top Bottom