Mkurungenzi Wa shule Ya Mus'ab,Tanga akiuka maagizo ya Wizara

Kikwajuni One

JF-Expert Member
Mar 18, 2013
13,149
6,993
Mkurugenzi wa Shule ya Mus'ab English Medium,akiuka maagizo ya Wizara ya Elimu,ya kutorudisha wanafunzi waliopata wastani chini ya 50,wa darasa la sita kwenda la saba,pamoja na madarasa mengine.

Wazazi wengi waliomfuata kuhusiana na kurudishwa darasa,hataki kuwasikiliza,mkurugenzi huyu ambaye sio mtanzania,anaitumia nafasi yake kuwakomoa wazazi,baada ya kupandisha ya ada kwa kiwango ambacho wazazi wengi hawakimudu,na wakati shule hiyo iko chini ya shirika,la African Muslim Agency,ambalo limeandikishwa Tanzania,likiwa kama shirika la misaada.

Twaomba Wizara ya Elimu,iwasaidie wazazi hawa,wanaohusika tunawaomba wafuatilie suala husika.
 
Hii shule sio Yake,hili ni shirika limeandikishwa Africa Muslim Agency,anatakiwa afuate sheria ya nchi,kama hafuati akafunguwe shule hewani sio kwenye nchi,ambayo hataki kufuata sheria ya nchi husika.
 
Wizar iwasaidie nini hzo n taratbu zao ,muandkshe serikaln wanaofata taratbu kml za wizar ya elimu
 
Mimi nimesoma hzo shule ,usipofikia wastani una takiwa Ku Repeat au kuhama

Hao waamue hayo mawili
Lazima wafuate utaratibu wa wizara,kama hafuati utaratibu wa wizara kwa nini shule aliiandikisha wizara ya Elimu.
 
Acha siasa kwenye elimu fisi wewe muache huyo mkurugezi afanye kazi yake hawezi kupitisha makapi hiyo siyo shule ya kata mtoto wako umemuona akili hana mpeleke magufuli secondary school
 
Kila mzazi achague pa kumpeleka mwanae, hutaki mwanao achujwe mpeleke pasipochuka.

Kwa hili serilali itarudi nyuma kama ada elekezi
 
Acha siasa kwenye elimu fisi wewe muache huyo mkurugezi afanye kazi yake hawezi kupitisha makapi hiyo siyo shule ya kata mtoto wako umemuona akili hana mpeleke magufuli secondary school
Acha ujinga,ikiwa yeye Mkurugenzi,ameshindwa kuwasimamia waalimu wake mpaka,wanafunzi kuwenza kufikia huo wastani.
 
Kwa nini mzigo abebeshwe mzazi,ikiwa kama mkurugenzi,hakusimamia waalimu,kufundisha kiwango kinachotakiwa,au kama ameajiri waalimu ambao hawana sifa.
Hili pia linatakiwa lichunguzwe,itakuwaje iwe upande wake kwa kujipa faida ya ada.
Wakati wanafunzi hawa walianza toka chekechea shule hii,iweje leo kutoka la sita kwenda la saba,wanguke,liko tatizo kwenye uongozi,sio kwa wanafunzi.
 
Kuna shule hazina smile kwa watoto vilaza. Shule za serikali watoto wengi humaliza shule ya msingi bila kujua kusoma, kuandika wala kuhesabu na hilo wanaona sawa. Shule binafsi hazitaki kuzalisha vilaza. Uliza wazazi waliokua wanalalamika kuhusu Al-Muntazir schools wameishia wapi.
 
Kuna shule hazina smile kwa watoto vilaza. Shule za serikali watoto wengi humaliza shule ya msingi bila kujua kusoma, kuandika wala kuhesabu na hilo wanaona sawa. Shule binafsi hazitaki kuzalisha vilaza. Uliza wazazi waliokua wanalalamika kuhusu Al-Muntazir schools wameishia wapi.
Itakuwaje watoto wawe kilaza,wakati walianza shule hii hii,kwa kufanya mitihani toka darasa la chekechea,na kote huko anapasi,leo kutoka la sita kwenda la saba,ndio watoto hawa wawe vilaza,kwa ukilaza ni wa shule sio wa wanafunzi.Wizara zifuatilie shule hizi.
 
Back
Top Bottom