Mkurugenzi wa Uchaguzi ajibu taarifa za Upotoshaji matokeo ya Dimani

Kinjekitile junior

JF-Expert Member
Apr 20, 2015
4,404
581
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeeleza kuwa Kura 234 ziliharibika katika Uchaguzi mdogo wa Ubunge katika jimbo la Dimani, Zanzibar Januari 22, 2017.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bw. Ramadhan Kailima amesema kuwa Wapiga Kura walioandikishwa katika jimbo la Dimani, Zanzibar ni 9,275.

Amesema kati ya hao wapiga Kura 6,406 walijitokeza kupiga Kura siku hiyo ambapo Kura halali zilikuwa 6,172 na Kura zilizoharibika zilikuwa 234.

“Napenda kuwafahamisha wananchi wote kuwa taarifa sahihi za matokeo ya Kura katika Uchaguzi mdogo wa Ubunge Jimbo la Dimani ni kama ifuatavyo; Wapiga Kura walioandikishwa jimbo la Dimani ni 9,275, Waliopiga Kura walikuwa 6,406, Kura halali 6,172 na Kura zilizoharibika ni 234” Amesisitiza.

Mkurugenzi Kailima ameeleza kuwa katika Uchaguzi huo vyama 11 vilikuwa na wagombea wa Ubunge ambapo Chama cha ACT-Wazalendo kilipata Kura 8, Chama cha ADC Kura 42, Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kura 4860, CHAUMA Kura 10, Chama Cha Wananchi CUF Kura 1234, Chama cha DP Kura 8.

Vingine ni Chama cha NRA kura 1, SAU Kura 4, TLP kura 2, Chama Cha UMD Kura 2 na Chama Cha UPDP Kura 1 na kufanya jumla ya Kura za Vyama vyote kuwa 6172.
 
Kidumu Chama cha Mapinduzi
Idumu Serikali ya Mapinduzi Zanzibar

Mapinduzi Daima!
 
kuelekea 2020 tunaitaji TUME HURU YA UCHAGUZI. Maana yangu ni nini??
kwa mfano Ramadhani Kailima ni nani !!! ana sifa gani za kusimamia uchaguzi!!
nafasi yake aliyonayo ilitangazwa lini kwy Govt gazette!!
nani alimfanyia veting/uhakiki wa background kujua km ana uwezo!!!
je Ramadhani na wenzake kwy tume Mkiti wa CCM anao uwezo wa
kuwatimua wakati wowote!! kwa maana are they serving for interest
of the people or for someone who appointed them!!
swali muhimu can the people hold the tume accountable for mishandling
the presidential election??? how about the court?? je mahakama kama msimamizi mkuu wa haki inao uwezo kwa niaba ya wananchi kuangalia kilichofanywa na Tume ili kuakikisha haki imetendeka!!????? kama si umma wala mahakama
inao uwezo wa kuangalia matendo ya Tume basi kuna haja ya kupigania
tume HURU. kama uundwaji wa chombo chenyewe siyo wa uwazi na wala
wausika wala stakeholders kwa maana ya wapiga kura na vyama vya siasa
havijui wakina Ramadhani na wenzake wamechaguliwa vipi na wamepatikanaje
kwa maana ya sifa na nafasi zao zilitangazwa lini ukiwemo uzoefu na elimu zao
basi hujue kuna umhimu wa kuwa na tume huru iliyopatikana kwa njia za wazi
ikiwashirikisha stake holders na taasisi zake. bila hivyo kushiriki kwy uchaguzi
especially wa Urais ni kupoteza muda kwani hata km mtu aliyewachagua akipata
kura mbili atatangazwa kwani amewaweka pale kulinda maslahi yake na si vinginevyo na pia power ya Rais kuweza kuwachagua na kuwatimua wkt wowote kinafanya chombo kizima kutokuwa huru kwani watawajibika kwa yule aliyewaweka
na siyo umma wala wapiga kura wala wagombea na wala mahakama ambayo imenyanganywa uwezo wa kuoji kinacofanywa na Tume kwahiyo Tume inayowajibika kwa mtu mmoja siyo huru na haiwezi kuwa huru milele
 
Mkuu unataka Tume Huru kama ya Kenya au nyingine?
 
Back
Top Bottom