Mkurugenzi wa jiji la Arusha akataa kamati ya usuluhishi aliyounda Meya

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,296
MKURUGENZI Mtendaji wa Jiji la Arusha, Athumani Kihamia amekataa kamati ya watu wanne iliyoundwa na Meya wa Jiji la Arusha, Calist Lazaro kutatua mgogoro wa maduka eneo la Stendi Ndogo jijini hapa.

Amesema kukataa kuundwa kwa kamati hiyo kunatokana na kamati nyingi kuundwa bila kuleta mafanikio na fedha za umma kupotea pasipo kutumia busara katika maamuzi. Kihamia alikataa Kamati hiyo iliyotaka kuundwa mwishoni mwa wiki kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa Jiji la Arusha, na kuongeza kuwa wananchi wanawatuhumu madiwani hao kuwa ndio chanzo cha mgogoro wa maduka katika Stendi Ndogo.

Alisema ni vema madiwani hao wakaacha masuala ya siasa katika kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo kwani sasa Jiji hilo linakosa mapato takribani Sh bilioni 1.2 kwa mwaka na kuambulia takriban asilimia 30 kwa mwaka kutokana na changamoto za migogoro ya maduka eneo hilo na maeneo mengine ya Kilombero, Soko Kuu na Kijenge.

“Nyie madiwani mnatuhumiwa kuwa ndio chanzo cha mgogoro huu, sasa acheni siasa badala yake fanyeni kazi maana maneno ni mengi na mmeshaunda kamati mbalimbali kabla hazijatoa majibu mnakuja tena na nyingine, hapana. Mjue fedha za wananchi mnatumia halafu faida hakuna, sitaki tume nyingine na siku nyingine kabla hamjaleta maazimio yenu muwasiliane na mimi ili nijue inawezekana au la, ila kwa hili sasa basi,” alisema mkurugenzi huyo wa jiji.

Alisema katika Stendi Ndogo maduka yenye mgogoro ni zaidi ya 396 na hivi sasa kuna kesi katika Mahakama ya Ardhi imefunguliwa ikisubiri maamuzi, hivyo hakuna busara ya kuunda kamati wakati kuna kesi mahakamani. Awali, Diwani wa Kata ya Olasiti, Alex Marti aliomba busara zaidi itumike kutatua mgogoro huo na viongozi waacha siasa pembeni ili kupata suluhu ya suala hilo.

KIHAMIA.jpg
 
Nionavyo Mimi mkirugenzi yupo sahihi. Suala LA usuluhishi halitakiwi kufanikishwa kwa nguvu ya fedha bali maridhiano, hao wote wanao hitilafiana ni watu wazima na wenye akili timamu, waitane wakae chini waondoe kasoro zilizopo au hao wanakamati kama ni vipi wajitolee tu
 
Back
Top Bottom