Mkurugenzi wa halmashauri afungwa jela miaka miwili

jamadari

JF-Expert Member
Feb 13, 2010
295
92
ALIYEKUWA Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Kigoma, Mohamed Masha amehukumiwa kifungo cha miaka miwili gerezani kwa kosa la kutoroka chini ya ulinzi halali wa serikali huku mashtaka mengine hususan shitaka la uhujumu uchumi wa Sh 77 milioni likisubiri.

Mkurugenzi huiyo alipata pigo hilo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa Kigoma iliyokuwa chini ya hakimu wa mahakama hiyo Emanuel Mrangu.

Hakimu huyo alisema alitoa adhabu hiyo ili iwe fundisho kwa watu wengine na viongozi waliopewa dhamana kama Masha kutenda mambomkinyume na maadili yake na uongozi kwa ujumla.

Pamoja na Mkurugenzi huyo, Mahakama hiyo pia ilimuhuku kifungo cha miaka mitatu gerezani polisi Nelson Mwaja ambaye alihusika katika tukio zima la kuhakikisha Masha anafanikiwa kutoroka.

Aidha hakimu Mrangu katika hukumu yake alimuachia huru aliyekuwa Meneja wa benki ya CRDB tawi la Kigoma, Mcharo Ngereja na polisi David Lorra baada ya kutokuwepo ushahidi wa kuthibitisha ushiriki wao katika kumtorosha mkurugenzi huyo.

Mrangu alisema hakuna mahali popote ambapo ushahidi unathibitisha kwamba Meneja huyo alishiriki kutoa fedha kwa polisi ili kumtorosha mshitakiwa wala kuruhusu kutoa gari lililombeba mtuhuhumiwa kuweza kutoroka.

Ilidaiwa kuwa ushahidi wa maneno uliotolewa kwamba dereva wa gari lililombeba Masha ndiye aliyepewa maagizo na Meneja huyo wa CRDB hayana uzito kutokana na upande wa mashitaka kushindwa kuwasilisha mazungumzo hayo ya simu baina ya watu hao wawili.

Katika hukumu hiyo pia hakimu Mrangu aliiambia mahakama kuwa kwa upande wa polisi Lorra hakuna sehemu yoyote ya ushahidi inayomtaja kuhusika katika tukio zima la kumhusisha na kadhia nzima ya kutoroka kwa mkurugenzi huyo.

Mkurugenzi Masha alikuwa akikabiliwa nan shtaka la kutaka kutoroka ambapo alikamatiwa uwanja wa ndege kutokana na kuwepo tuhuma za ubadhilifu wa fedha nyingi kwenye halmashauri yake ambazo ziligunduliwa na vyombo vya dola.

CHANZO MWANANCHI
 
Nafikiri papa hawakamatiki kwa sababu wanaiba hela nyingi hawa wa pesa ndogo ndio tatizo kwa viongozi wetu.
 
Bado wale wa Bagamoyo na Mhasibu wao; tusubiri tuone maana huko kuna tetesi za vigogo kuhusika!

Hata hivyo nitoe pongezi kwa wote waliofanikisha hili hata kama ni dogo katika makubwa lakini bado ni hatua!
 
Mfano mzuri wa kuigwa na mahakimu wengine nchini; lakini tunangojea hao wa Bagamoyo tuone kama huyo kigogo aliyehusiswa katika matumizi mabaya ya fedha za umma nae atapata adhabu stahiki!! Justice has to be metted across the board!
 
Back
Top Bottom