Mkurugenzi wa Break Point afikishwa mahakamani kwa kutotumia mashine ya EFD

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
6,042
10,787
Mkurugenzi wa Hotel ya Break Point, David Machumu amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya Kinondoni akituhumiwa kwa mashtaka matatu likiwemo la kushindwa kutoa risiti katika mashine za elektroniki (EFDs).

Akisoma hati ya mashtaka Wakili wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) wa Wilaya ya Kinondoni, Juliana Ezekiel amedai kuwa tukio hilo lilitokea Oktoba 8, mwaka 2016 katika hoteli hiyo iliyopo Kinondoni.

Wakili Ezekiel amedai kuwa mtuhumiwa kwa makusudi na bila sababu alipokea Sh12,000 kutoka kwa mteja ajili ya vinywaji bila ya kutumia mashine za EFDs ambapo kufanya hivyo ni kosa kinyume cha sheria ya kodi.


Chanzo: Mwananchi
 
Mmh aisee..hivi yale mapato yao ya kila mwezi mbona siyasikii hizi siku mbili tatu hapa
 
Wanamsumbua tu huyo.. Waende kariakoo mchana kweupeeew.
Wata enjoy wenyewe
 
Sitetei kukwepa kodi, ila kama wameamua kuendesha zoezi la kulipa kodi, lisiende kibaguzi. Lifanyike sawa kwa wote.
 
Ndio unajua hilo Leo ? Machine ilikua mbovu na alishatoa taarifa na kuipeleka hao Tra. Km ni hilo basi kuna ziada. Hio issue naijua nilishuhudia yakitokea. Asimame kuuza chskula kisa efd ? Hio hasara italipwa na nani.
 
Hivi maduka gani hasa yanatakiwa kutumia hizi EFDs maana maduka mengi mtaani ambayo kwa hadhi yake yanatakiwa yawe na hizo EFD unapewa jibu raisi "tumeomba hatujapata", sasa utafanyaje? Kibaya zaidi nimeshuhudia kwamba watu wengi sana hawana hata muda kudai risiti wakilipa wakapewa kitu walichonunua haooo!. Kiasi mimi ninapodai risiti ya EFDs wananiona msumbufu, ukikomaa hasa Kaliakoo utaona mtu anajivuta anaingia chemba anakuletea. Wala mashine haipo hapo hapo kaunta kwa maduka mengi. TRA ongezeni awareness Watanzania suala la risiti bado kabisa.
 
Ndio unajua hilo Leo ? Machine ilikua mbovu na alishatoa taarifa na kuipeleka hao Tra. Km ni hilo basi kuna ziada. Hio issue naijua nilishuhudia yakitokea. Asimame kuuza chskula kisa efd ? Hio hasara italipwa na nani.
Siyo mara ya kwanza kwa TRA kutia timu kwa huyu jamaa, wanaenda wamapata lager kisha wamakataa kulipa, wanalao Jambo
 
TRA wafanye kazi kwa ufanisi waache mitego, haiwezekani club kubwa na maarufu kama ile ikose EFD !!
 
Back
Top Bottom