Tanzania Railways Corp
JF-Expert Member
- Mar 23, 2018
- 274
- 646
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Mhandisi Machibya Masanja ametembelea banda TRC katika maonesho ya kimataifa ya biashara (Sabasaba) yanayoendelea katika viwanja vya Mwl. J.K Nyerere jijini Dar es Salaam muda mfupi baada ya maonesho hayo kufunguliwa rasmi Julai 7, 2025 na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi.
Mkurugenzi Mkuu TRC, akiwa bandani hapo amesema kuwa ushiriki wa TRC katika maonesho hayo ni muhimu kwa kutoa elimu kwa wananchi kuhusu miradi, huduma na mipango ya TRC siku za baadaye katika kuboresha huduma za usafiri wa reli nchini.