Mkurugenzi (H) Monduli Mtendaji huyu anakutega

MLIMAU

Member
Feb 2, 2017
17
2
Mimi ni mkazi wa Kjiji cha Makuyuni wilaya ya Monduli naomba kumweleza Mkurugenzi wa Wilay ya Monduli kuwa Mtendaji wa Kijiji cha Makuyuni Mzee Mwenda anatuvuruga na amekuwa chanzzo cha vurugu eneo la Makuyuni kwa sababu amesahau wajibu wake.

Mzee Mwenda amefanya mambo ya kusikitisha baada ya kusimamisha wajumbe wa serikali ya Kijiji walipwe fidia na TANESCO kwenye eneo la Kanisa Katoliki na eneo la chuo cha VETA ambacho ni mali ya Halmashauri ya Monduli.

Fidia hii ni ile inayotolewa na TANESCO kupitia kupitisha msongo mkubwa wa umeme yalipo mashamba ya taasisi za dini, serikali na mashamba ya watu binafsi.

Bila aibu Mwenda badala ya kuwataarifu wahusika kuja kusimama wakati wa tathmini aliamua kufanya wizi wa mchana kwa kuwasimamisha marafiki zake ili wakishalipwa fidia wagawane.

Cha kusikitisha hata lililokuwa eneo la Halmashauri ya Monduli kilipo chuo cha VETA Makuyuni amesimamisha mtu binafsi ili achukue fidia ambayo kuhalali ni ya Halmashauri. Hapa ameamua kupanga na kuiibia Halmashauri wazi wazi ambayo kimsingi ndiyo iliyomwajiri.

Ni ushahidi gani tena Mkurugenzi wa Halmashauri ya monduli anautafuta ili kumwajibisha huyu Mtendaji mwovu wa Kijiji . Lichofanya Mwenda ni hujuma dhidi ya mwajiri wake na sioni kama ana sifa ya kuendelea kuwepo Makuyuni.

Sijui kwa nini Mkurugenzi anasita kumchukulia hatua kali wakati malalamiko yanayomlenga ni mengi haswa kuhusu udanganyifu wa fidia alioufanya pale Makuyuni akishirikiana na serikali ya Kijiji haswa Mwenyekiti mzee Sulle.

Mtendaji amekuwa hafuati tena taratibu za serikali na sheria za nchi na badala yake anaongozwa na Mwenyekiti mzee Sulle.

Mwenyekiti wa kijiji cha makuyuni amemfanya Mwenda kuwa kama msukule wake kwani hawezi tena kufanya maamuzi kama yanapingana na mawazo ya mwenyekiti wa kijij. Kuna ombwe la uongozi Makuyuni na ndiyo maana vutrugu zinazoepukika za ardhi zimekuwa nyingi.

Namshauri Mkurugenzi amchukulie hatua la sivyo hizo hela za Halmashauri zikiondoka DED utakuwa ktk wakati mgumu. Tunakuangalia kwa karibu tuone busara na hekima zako zikifanya kazi baba.
 
Mi ni mdau wa Monduli ni kama ardhi yake ina laana. Kwani kule halmashauri ndio kabisaa
 
Mtu anasimamia wezi kuiba mali za mwajiri wake ili akatiwe ka percent na shahidi ni yeye? hapa isisikike upelelezi unaendelea tena ni mtu kukamatwa na kusekwa ndani
 
Msiogope tuko hapa na Mkuu wa Wilaya tunaangalia jinsi atakavyoshughulikia hili jambo
 
Natamani mkuu wa wilaya akiondoka hapa Makuyuni leo aondoke na mtu wake na si vingivyo
 
Mkuu wa Wilaya najua hakuja hapa kupoza wala kupindisha mambo kwani malalamiko ni mengi kwa serikali ya mwenda na mwenyekiti Sule. anatakiwa afanye mambo kwa kunyoosha kamba
 
Mwana kwetu nashukuru upo hapo Makuyuni kufuatilia kikao cha mkuu wa wilaya na hao wezi
 
Nadhani namfahamu huyu mzee, kuna kipindi alikuwa anaishi Arusha kwenye magorofa ya NHC karibu na hospitali ya kaloleni,
 
Naamini utatupa taarifa zote na harufu utakayo detect itatusaidia kwani hiyo serikali ni ovu na haimtaki mtendaji wa kata kwa sababu yeye anasimama palipo na ukweli
 
Kuna ka msemo kanasema "ukicheza na mpumbavu atakupaka mavi" sasa huyu Mkurugenzi inawezekana ni mwadilifu sana ila anachenza na mpumbavu.
 
Back
Top Bottom