Jembe Jembe
JF-Expert Member
- Jun 9, 2016
- 757
- 1,822
Mkurugenzi wa jiji la Arusha ,Dkt Maulid Madeni amekata pongezi za kumsifia baadabya jiji lake kuibuka kidedea kwa kuvuka makusanyo ya ndani kwa majiji yote nchini akidai kuwa sifa hizo hazimsaidii iwapo kama hajafikia malengo aliyojiwekea .
Akiongea na vyombo vya habari ofisini kwake Mkurugenzi wa jiji hilo,Dkt Maulid Madeni amesema kuwa licha ya jiji hilo kuvuka malengo ya makusanyo mwaka wa fedha 2019/20 kutoka bilioni 15.7 na kufikia bilioni 16.4 na kushika Namba moja kwa majiji yote nchini,amesema mpango wa jiji hilo ni kufikia makusanyo yanayozidi sh, bilioni 30 kwa mwaka .
Dkt Madeni amesema kuwa pamoja na pongezi nyingi alizopata za kuvuka makusanyo ya ndani, amesema kipaumbele chake si kusifiwa na wala hapokei pongezi hizo bali ni kufikia malengo ya makusanyo aliyojiwekea na kulihakikishia maendeleo jiji la Arusha .
Hata hivyo amesema Jiji lake limepanga kukusanya mapato ya ndani kiasi cha shilingi bilioni 20.7 katika bajeti ya mwaka wa fedha 2019/20 kupitia vyanzo vyake mbalimbali vya ndani.
"Mimi si mtu wa kusifiwa na wala sikubali pongezi hizo ninachotaka bado hakijafikiwa, lengo langu ni kufikia makusanyo ya bilioni 30 " Amesema Madeni.
Katika hatua nyingine Dkt Madeni amesema kuwa jiji la Arusha limetenga bajeti ya kiasi cha shilingi bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la ofisi na ukumbi wa Mkutano.
Dkt Madeni amesema ujenzi wa jengo hilo unatarajia kuanza mapema mwaka wa fedha 2919/20 na litajengwa jirani na ofisi za sasa za halmashauri hiyo.
Pia Mkurugenzi huyo amedai kuwa jiji la Arusha limetoa kiasi cha shilingi milioni 140 kwa wakala wa barabara za mijini na vijiiini Tarura kwa ajali ya kuzifanyia ukarabati barabara zote za jiji hilo zilizoharibiwa na mvua kipindi cha masika.
Amesema barabara hizo zitafanyiwa matengenezo na kuondoa malalamiko yanayojitokeza kwa watumiaji wa barabara wakiwemo watumiaji wa vyombo vya moto ambao wamekuwa wakilalamika kuharibika kwa magari yao kutokana na mashimo yaliyopo.
Wakati huo huo jiji hilo limesaini mkataba wa ujenzi wa barabara yenye urefu wa kilometa 3.5 itakayojengwa kwa kiwango cha Lami kwa thamani ya shilingi bilioni 4.1.
Akiongea wakati wa kusaini mkataba huo baina ya jiji hilo na kampuni ya ujenzi ya Sinohydro kutoka nchini china Meya wa jiji la Arusha, Kalist Lazaro alisema kuwa mradio huo ni kazi ya nyongeza ya ujenzi wa mradi wa barabara ya Kisongo Bypass inayotoka Olasiti jijini hapa.
Meya alisema kuwa mkandarasi huyo atafanyakazi yenye ubora kwa muda wa miezi minne kuanzia September 11/2019/hadi January 11/2020 atakapokabidhi mradi huo.
Ends.....