Mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by CHITEMBEJA, May 10, 2012.

 1. C

  CHITEMBEJA Member

  #1
  May 10, 2012
  Joined: Apr 18, 2011
  Messages: 50
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Wadau jf hamjambo.

  Hakika Jeshi letu la polisi na baadhi ya vyombo vya habari visipoacha unafiki katika kazi zao zinaweza kushusha janga katika taifa hili.

  Hii inatokana na mtazamo wangu wa muda mrefu wa namna vyombo hivi viwili vinavyoyachulia masuala nyeti ya kitaifa hasa yanayohusu siasa na ambayo ndiyo yanayobeba mustakabali wa amani na utulivu wa nchi hii ikiwa pamoja na kudumisha umoja wetu

  Mifano miwili halisi ya matukio ya kisiasa na jinsi jeshi letu la polisi na baadhi ya vyombo vya habari yalivyoyachukulia ni yale ya Makada vijana wa CCM kufanya kikao pale Kibaha na kutoa Matamko mazito ya kuwagawa watu Kikanda kwa kutumia uongozi wa Nchi na lile la Mbunge Nassari la kutaka kanda yake kujitenga kwa kuhisi kuonewa na uongozi wa serikali uliyopo.

  Kwangu mimi ninaona ni hatari sana kwa sababu utendaji wa polisi na jinsi ulivyoyahandle masuala haya mawili tu na baadhi ya vyombo vya habari kuthibitisha bila shaka yo yote kuwa kuna upendeleo wa dhahiri kiasi kwamba ipo hatari ya yule anaejiona kuonewa kuamua maamuzi magumu kama ya Nassar na yule anaependelewa kuona kuwa ana haki ya kufanya atakavyo kama wanavyofanya viongozi wa CCM.

  Makada wa Chama Cha Mapinduzi Vijana kanda fulani walikaa pale Kibaha na kutoa matamko mazito akiwemo mtoto wa Rais ambayo yalikuwa dhahiri ya ubaguzi mbaya wa kikanda ubaguzi ambao Baba wa Taifa aliukemea sana wa kutaka Rais atoke kulingana na ukanda badala ya uwezo ubara au Uzanzibara.

  Cha ajabu Polisi hawakujihangaisha kwa namna yo yote na makada wale kwa kuona kuwa wanahatarisha amani ya nchi kwa kuigawa nvhi ki kanda wala gazeti la mwananchi halikuona umuhimu wa kukemea siasa kama zile uchwara na kutufahamisha adhari zake.

  Hakuna alieona awe Rais au Waziri ama Polisi kuwa kama hawa wakiachiwa madai yao haya ipo hatari ya kuamsha hisia ya kuonewa ki uongozi Kanda zingine lakini pia muungano wetu kuwa Wanzibari nao watajiuliza zamu yetu ipo lini tena Mashariki nao watakutana kama walivyokutana Kibaha na kudai kanda ya Kati nayo je?

  Hli polisi hawakuliona hatari yake uchochezi huu mbaya kwa mustakabali wa amani umoja wetu na utulivu wetu ama kweli Mkuki kwa Nguruwe binadamu mchungu.

  Gazeti la Mwananchi hili hawakuliona kama lina adhari yo yote lakini Mwalimu Nyerere aliliona kuwa na adhari kubwa kupita ukoma akakemea.

  Nassari juzi juzi kutokana na hali ya kujihisi kuonewa kutengwa kimatendo japo siyo kwa maneno akatoa matamshi hatari ya kuitahadharisha serikali kuhusu mwenendo wake kuwa utagawa nchi na yeye bila kutafuna akasema kama itaendelea hivi wao watajitenga au hawatakuwa radhi kumpokea Rais ambaye hakemei matendo haya ya uvunjifu wa amani utulivu na siasa za kistarabu.

  Huyu ameonekana mchochezi Polisi wamekuja Juu hawakamatiki, Gazeti la Mwananchi limeibuka na maoni ya mhariri kukemea kauli hizi maoni ambayo yanaonyesha wazi kuwachochea polisi wachukuwe hatua kutokana na ukweli kuwa watu wanaamini maoni ya mhariri ni msimamo wa gazeti siyo ya mtu binasfi nai maoni ya UMMAi!!!

  KWELI MKUKI KWA NGURUWE BINADAMU MCHUNGU NDIVYO TAFSIRI HALI INAYOONYESHA KUFANYWA NA VYOMBO HIVI LINAPOJITOKEZA SUALA LA VYAMA HIVI VIWILI AU PANDE HIZI MBILI ZA CHAMA TAWALA NA UPINZANI AU CCM NA CHADEMA .

  Uchochezi na ubaguzi na siasa za matusi zinazohatarisha amani utulivu na umoja wetu kwa jeshi letu la polisi na Mwananchi gazeti zinatoka upande mmoja tu wa upinzani ama Chadema Lusinde akitukana Polisi wanaona halali ingekuwa Chadema wangekuwa wametinga mahakamani na Mwananchi angeibuka na mhariri ambAayo dhahiri yangekuwa uchochezi kwa polisi wawakamate Chadema Makada wa CCM wakikutana kusema Urais uwe wa mgao hao siyo ubaguzi ni siasa hakuna hatari hapo ya uchochezi wa kikanda.

  AA HAKIKA TUNAKOELEKEA KUBAYA.
   
 2. m

  mbwago2007 Member

  #2
  May 10, 2012
  Joined: Oct 19, 2009
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Polisi pia wamedhihirisha kuwa wanawanwanyanyasa wapinzani. Kauli ya Bw. Mngulu ni ushahiddi tosha. Mungulu alisema bila ya kutafuna maneno kuwa kama MHE. NASSARI hatajisalimisha mwenyewe jeshi lake litamzalilisha. Je kauli hii ina maana gani!!!!!!!!!!!!!!!
   
Loading...