Mkuchika Kikwazo cha maendeleo Kusini.

GAZETI

JF-Expert Member
Feb 24, 2011
5,200
6,383
Ili kuwasaidia wakulima (Kama ni kweli) Serikali ilianzisha mfumo
Wa uuzwaji wa mazao unaojulikana kama Stakabadhi ghalani. Ni
Mfumo maarufu ambao Chama cha ushirika kupitia kwa vyama
Vya msingi vya ushirika hukusanya mazao ya wakulima na kuyapeleka
Ghala kuu ambako huuzwa kwa mnada.

Tatizo lililopo ni kwamba mnada huo umekuwa ukiendeshwa kwa
Siri bila mkulima kufahamu mazao yake yamenunuliwa kwa bei gani
(Hapa nakusudia zaidi zao la korosho) Mwisho wa yote mkulima
Huambulia Tsh 800 mpaka 1000 tena siyo taslimu hulipwa kwa awamu
Tatu bila kuambiwa korosho zake zimenunuliwa kwa bei gani.

Baadhi ya wakulima wakaamua kuanzisha umoja wao wa wakulima wa
Korosho ili waweze kuuza wenyewe kwa mfumo huo huo ambao serikali
Inautaka. Umoja huo ukasajiliwa kwa Cert. no. S.A 16671. Umoja ukaanza
Kazi.

Jambo la kwanza lililofanywa na umoja huu ni kufichua bei ya zao hilo
Huko ghalani ambayo ilibainika wazi kuwa ni kubwa ukilinganisha na
Malipo yaliyokuwa yanamfikia mkulima. Kwa mara ya kwanza Mkulima
Ambaye ameuza kupitia umoja huo akalipwa pesa taslim Tsh. 1,800
Hapo ndipo miksukosuko ilipoanza. Serikali kama kawaida yake ikaanza
Kutumia mabavu kuuzuia umoja huu kufanya kazi hiyo. Baada ya
malumbano ya muda mrefu hatimaye umoja huo ukaruhusiwa kuuza
korosho zilizosalia.

Jambo la kushtusha ni barua ya hivi karibuni kutoka TAMISEMI ambayo
Inauzuia umoja huo kukusanya na kuuza korosho za wakulima wake.
Huu ni uonevu wa wazi ambao unanifanya mimi na wengine kuamini
Kuwa mkuchika na wote waliokuwa wanatajwa kunufaika na uuzwaji
Wa korosho kuwa Tuhuma hizo ni za kweli. Kwanini huu umoja unaandamwa
Kiasi hiki? Ni wazi kuwa serikali haina nia ya dhati ya kumtaka mkulima
Awe na maendeleo ya kweli.

Mkuchika tunaomba ujirekebishe, una tuhuma za mradi wa NDF, tunajua
Kuwa unapata fedha nyingi kutoka kwa wahisani kwa ajili ya maendeleo
Ya shule za sekondari zilizo chini ya NDF (Newala Development Foundation)
Tunajua kuwa fedha nyingi zinaingia mfukoni mwako. Hatutaki kukuumbua zaidi
Tunachotaka utuachie korosho zetu tufanye tunavyotaka la sivyo tutaanika
Uozo wako wote mpaka huko kwa wahisani wako.
 
Kimilidzo

JF-Expert Member
Jan 3, 2011
1,346
594
Hakuna mwana CCM anayependa maendeleo ya wakulima na wafanyakazi wa chini. So do Mkuchika... Mi nashangaa sana ilikuwaje mkampa hata ubunge kwani kauli zake zinajidhihirisha kila wakati kuwa ni mkuu wa vilaza wote nchini.
Poleni wana kusini, komaeni ili umoja wenu uwasaidie. Nadharia ya ushirika ni grassroot, yaani inaanzia kwa nyie wakulima wadogo kwenda juu, sio kuletewa na hao wezi akina mkuchika na kuwaamulia cha kufanya
 
GAZETI

JF-Expert Member
Feb 24, 2011
5,200
6,383
Kwa mambo wanayotufanyia hawa jamaa nimefikia kuwa na mawazo
ya Ajabu sana. Yaani natamani Mungu angefanya siku moja liwaangukie
jengo lao pale Kimwaga Dodoma, Wafutike wote tuanze moja!
 
GAZETI

JF-Expert Member
Feb 24, 2011
5,200
6,383
Hakuna mwana CCM anayependa maendeleo ya wakulima na wafanyakazi wa chini. So do Mkuchika... Mi nashangaa sana ilikuwaje mkampa hata ubunge kwani kauli zake zinajidhihirisha kila wakati kuwa ni mkuu wa vilaza wote nchini.
Poleni wana kusini, komaeni ili umoja wenu uwasaidie. Nadharia ya ushirika ni grassroot, yaani inaanzia kwa nyie wakulima wadogo kwenda juu, sio kuletewa na hao wezi akina mkuchika na kuwaamulia cha kufanya
Mbaya zaidi wanataka wakulima wauuze mazao yao kupitia
Chama cha TANECU ambacho kina sifa sawa kabisa na hiki
wanachokizuia tofauti ni kwamba hiki wanachokitaka kimejaa
makada wa CCM.
 
Nazjaz

JF-Expert Member
Jan 20, 2011
6,946
6,382
hiyo ndo faida ya kuipa kura zenu CCm. Ikataeni ccm maana ndio kikwazo cha maendeleo yenu
 
GAZETI

JF-Expert Member
Feb 24, 2011
5,200
6,383
hiyo ndo faida ya kuipa kura zenu CCm. Ikataeni ccm maana ndio kikwazo cha maendeleo yenu
Tuko Tandahimba Tuliikataa CCM bt wamechukua jimbo kwa nguvu
Huyo Mkuchika anatamba kote kote ili kuimiliki vizuri Wilaya ya Tandahimba
Ndio maana wameanzisha TANECU yaani TANDAHIMBA & NEWALA COP. SOC.
 
GAZETI

JF-Expert Member
Feb 24, 2011
5,200
6,383
Nini kilitokea kwa rail way kule Mtwara.
Hapo ndipo unapoweza kuifananisha serikali ya CCM na ile ya mfalme JUHA Reli
Imeng'olewa na vyuma vikatumika kujengea fensi na mageti hata huelewi walikuwa
na Lengo gani kuing'oa ile reli au ni mpango maalum wa kuididimiza kusini?
 
Freema Agyeman

JF-Expert Member
Mar 3, 2011
3,653
3,460
Hapo ndipo unapoweza kuifananisha serikali ya CCM na ile ya mfalme JUHA Reli
Imeng'olewa na vyuma vikatumika kujengea fensi na mageti hata huelewi walikuwa
na Lengo gani kuing'oa ile reli au ni mpango maalum wa kuididimiza kusini?

Juzi kati hapa nilikuwa nacheck NHC wakibomoa nyumba kwa kumtoa mpangaji anayedaiwa kodi ya millioni tatu.It was pathetic.
 
Rweye

JF-Expert Member
Mar 16, 2011
16,711
7,151
Mleta mada unataka kusema unazijua siri nyingi za Mkuchika na bado unazificha?unamfichia nani kwa nini usiweke uhozo huo hapa Jf ama na wewe unanufaika na uhozo huo?
 
GAZETI

JF-Expert Member
Feb 24, 2011
5,200
6,383
Mleta mada unataka kusema unazijua siri nyingi za Mkuchika na bado unazificha?unamfichia nani kwa nini usiweke uhozo huo hapa Jf ama na wewe unanufaika na uhozo huo?
Vuta subira mkuu najaribu kutafuta vielelezo nikivinasa nitamuanika hapa
tatizo ni hilo tu ilibaki kidogo nivinase unajua utamu wa mambo kama hayo uwe
na vielelezo kwani yanafahamika kwa wengi bt tatizo ni Evidence!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom