Mkopo wa viwanja + vifaa vya ujenzi

Mkopo wa viwanja + vifaa vya ujenzi

CCC LTD,inawakaribisha Watanzania wote kwenye mradi wa uwezeshaji ktk sekta ya Makazi. Sera yetu ni kufanikisha upatikanaji wa Makazi kwa njia rahisi kwa watu wengi wa kipato cha chini kati na hata wale wenye kipato cha juu.

Mpango wetu unawaalika wenye mahitaji yafuatayo:

*Wenye mipango ya kununua KIWANJA lakini wamekwama VIFAA VIA kuanzia ujenzi.( tutakuuzia KIWANJA na kukukopesha Matofali na cement).
* Wenye kuhitaji KIWANJA kwanza lakini hawana pesa ya kutosha( tutakukopesha KIWANJA na ukimaliza kulipa utakopeshwa VIFAA VYA ujenzi kwa awamu hadi utahamia kwako.

* Wenye ndoto ya kujenga nyumba ya aina Fulani lakini bajeti yao ni ndogo, tutatathimini jinsi ya kuwawezesha.

* Wenye kuhitaji kununua Viwanja kwa ajili ya akiba ya baadae ya watoto tunawakaribisha tutawashauri jinsi ya kuwekeza.

√÷+-*CCC LTD , Imekuja na mpango huu baada ya utafiti na kugundua vikwazo kadhaa vinavyo zikabili familia nyingi katika harakati ya kutafuta Makazi bora :

1. Watu wengi huwachukua zaidi ya miaka 5 kukamilisha ujenzi wa nyumba baada ya kununua KIWANJA.
2. Watu wengi huishia kutapeliwa wakati wa ununuzi wa Viwanja visivyopimwa.
3. Watu wengi hutumia gharama Mara mbili zaidi ya kawaida kwani huwalazimu kuishi miaka mingi kwenye nyumba za kupanga huku wakilipa pango ya nyumba na kodi ya ardhi wakati akisubiri majaliwa ya kujenga.
*Watu wengi hupoteza matumaini ya kujenga baada ya majukumu ya kifamilia kuwazidi na kufanya KIWANJA alichonunua kuvamiwa na kuanza kuleta migogoro isiyoisha mahakamani.
* Watu wengi hukosa sifa za kukopesheka ktk taasisi za fedha hivyo huishia kuishi katika Makazi duni.
* Familia nyingi zimeshindwa kudhibiti tabia za watoto baada ya kuishi maeneo yasiyopangiliwa kimakazi .
* Makazi duni huchochea hali ya umasikini,ujinga na maradhi.
* Sera za taasisi nyingi za fedha haziko rafiki na watu wenye kipato kidogo ,imekuwa vigumu kupata MIKOPO ya nyumba kama inavyonadiwa.

Hivyo basi CCC LTD, INAKUJA NA JAWABU LA MAKAZI BORA KWA NJIA RAHISI ,JIUNGE NA UWE MWANACHAMA WA WETU ,ILI UPATE KUINGIA KWENYE MKAKATI WETU WA KUWEZESHA WATANZANIA KUPATA MAKAZI BORA.

#* SIFA.
* Mtanzania miaka 18 na kuendelea,
* Mwenye kipato ( biashara, kilimo,Ajira)
* Nunua Viwanja katika maeneo tuliyotenga na kuyahakiki sisi( CCC LTD)

#* Viwanja vipo maeneo ma5 tofauti kigamboni.(Mwasonga,Mwembe mdogo,Amani Gonvu, Mbutu
Pia Mvuti(iko wilaya ya ilala,) Mbande karibu na Azam complex, nk.
*# Miradi inayotarajiwa: Dodoma, kibaha,na Mkuranga.

*Ukubwa kuanzia: mita 20*20( sqm 400)hadi 4200sqm

*Bei kuanzia mil 4.8

MAWASILIANO:
CCC LTD .
PO BOX 38509 DAR ES SALAAM.
Email: chadcreationtz gmail.com
0762781778/0674880470

Sasa mkuu.

Mimi nipo huku Mtwara,ni mmiliki wa kituo cha tiba nina kiwanja ambacho tayari nimeanza ujenzi wa kituo kingine cha kutolea Huduma za afya je naweza kupata msaada(mkopo) wenu kukamilisha ujenzi huo.

Nasubiri jibu
 
Sasa mkuu.

Mimi nipo huku Mtwara,ni mmiliki wa kituo cha tiba nina kiwanja ambacho tayari nimeanza ujenzi wa kituo kingine cha kutolea Huduma za afya je naweza kupata msaada(mkopo) wenu kukamilisha ujenzi huo.

Nasubiri jibu
Kwasasa jibu ni hapana Sera ni kuendeleza makazi
 
Mkuu nimeweza kuelewa nia yenu ni nzuri na bora kwa wanyonge hasa wasio na uwezo wa kupata pesa ya pamoja

Nisaidie kuweka sawa hii

Unatakiwa kuwa na 20%(ambayo ni 960,000/=TZS)ili uweze kukopeshwa 80%.
1.Mkopo wa muda gan?
2.Kuna interest kwenye mkopo?
3.Mtu akishindwa mwishoni kuleta marejesho mkataba unasema vipi?
Kwa wasio na Ajira rasmi tunawashauri kujiunga kwenye vikundi unaweza kunicheki kwa what's up tuweze kuona ni jinsi gani ya kuwawezesha, MIKOPO ni kwa mwaka mmoja kwa Viwanja, namba yetu kwa what's up 0762781778
 
Mkuu nimeweza kuelewa nia yenu ni nzuri na bora kwa wanyonge hasa wasio na uwezo wa kupata pesa ya pamoja

Nisaidie kuweka sawa hii

Unatakiwa kuwa na 20%(ambayo ni 960,000/=TZS)ili uweze kukopeshwa 80%.
1.Mkopo wa muda gan?
2.Kuna interest kwenye mkopo?
3.Mtu akishindwa mwishoni kuleta marejesho mkataba unasema vipi?
MTU akishindwa kulipa tutauza na kurejesha alichotoa
 
Kama kiwanja ninacho nanilisha anza kujenga inakuwaje?
Kwasasa tunawezesha wale Wateja wetu wa Viwanja , lakini tunakiri kupokea maombi mengi kama ya kwako _,tunayafanyia kazi
 
kwa hyo nikinunua kiwanja kwenu kwa bei hyo hapo,mnanijengea kama sina pesa then mnataka nilipe sh ngap kwa mwezi?
Lazima tukae kuona ni kiasi gani utahitaji ndipo tunaweza kujua ni kiasi gani utaweza kukopeshwa na jinsi ya kulipa
 
Umenena vema sana mkuu,lakini kuna maswali kadhaa nimeshindwa kuyapatia majibu;
1.Kwa kuwa malengo ni kuwasaidia wanyonge wa mikoa uliyoitaja (Dar na mengine tarajali) vipi kwa mikoa mingine kama Morogoro n.k

2.Mchanganuo wa namna mnavyowasaidia hao masikini,kwa mfano cement,mnakopesha kwa bei gani,na kwa muda gani?

3.Kwa upande wa wananchi wasio na ajira,mnawakopesha kwa vigezo gani!!?

Kwa sasa maswali yangu machache ni hayo,naendelea kutafakari wema wenu mkuu kuwasaidia raia wa Tanzania,MUNGU na awabariki sana kama nia yenu ni njema kwa masikini wa taifa letu.
Utafiti unaonyesha watu wengi hawakopesheki kwa kukosa dhamana,anuani na jinsi ya kuonyesha mapato yao kwa mfumo rasmi, hivyo basi watu wa kundi hili ngao yao kubwa ni umoja ,tunashauri watu waungane na kuja kutuona tuandae mfumo wa kuwasaidia .
 
Mpango Mzuri,
Hembu niambie yafuatayo
a)Mbande karibu na AZAM,bei ni kiasi gani
b)Mvuti nako bei ipoje?

Wazo:
Ofisi zenu zipo wapi?
Na mnaonaje mngetengeneza website ambapo mngekuwa wa kisasa zaidi kuliko mnavyofanya sasa,mnasimamia mradi mkubwa mnatumia GMAIL?
Kenyan wajasiriamali wanatupita mbali sana kwa ubunifu.
 
Mpango Mzuri,
Hembu niambie yafuatayo
a)Mbande karibu na AZAM,bei ni kiasi gani
b)Mvuti nako bei ipoje?

Wazo:
Ofisi zenu zipo wapi?
Na mnaonaje mngetengeneza website ambapo mngekuwa wa kisasa zaidi kuliko mnavyofanya sasa,mnasimamia mradi mkubwa mnatumia GMAIL?
Kenyan wajasiriamali wanatupita mbali sana kwa ubunifu.
1 km toka Azam complex ,mita 400 toka Rufu Mbande kuna eneo linaitwa Mlamleni hapo ndipo mradi ulipo , eneo hili kijografia linasomeka Wilaya ya Mkuranga ,ni mpakani mwa Temeke na Mkuranga ,eneo zuri lipo juu ,hewa ya kutosha sehemu kubwa ni tambarale.Miundo mbinu ya umeme ,Barabara tayari imefika. BEI ni kuanzia Mil 3, kulingana na ukubwa , ktk eneo hili Viwanja vichache vimeanzia ukubwa wa sqm 290 na vikubwa kabisa ni 1000sqm .

Kuhusu Mvuti vilivyopo sasa ni kuanzia sqm 1000 na bei ya sqm 1 ni tsh 12000.

WEBSITE YETU IPO UNDER CONSTRUCTION tumebadili mambo mengi kuhusu Sera zetu soon tatakuwa hewani.
Karibu , kwa ushauri what's up 0762781778
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom