Hiyo laki sita ni baada ya makato au ndo mshahara wote? Kwa maelezo ya uhakika niliyoyapata NMB nilipoitembelea wiki hii, hesabu rahisi ya kujua kiasi gani unachoweza kukopa mkopo wa mshahara ni sawa x20 take-home yako (+/- kidogo sana).
Masharti muhimu ni kupeleka barua ya kuajiriwa, barua kutoka kwa mwajiri wako (bosi wa kituo chako cha kazi; sio barua ya uthibitisho kazini) na salary slips za miezi mi3 ya karibuni!!
Nikiangalia masharti japo mepesi kabisa sioni ni jinsi gani utayatimiza...ndio kwanza una miezi miwili, slips za miezi mitatu utazitoa wapi?
Ushauri wa bure:
Kaa chini utafakari mara ya pili kama una hitaji la gari kiasi hicho. Ongea na seniors wako ofisini wenye magari upate picha ya kuhudumia gari pale utakapokua umeanza makato! Nina hakika kuna jambo zuri zaidi ya gari. Kuchukua mkopo na ukafanyia jambo la kuzalisha utaona uzuri wa kazi, upande wa pili itakua majuto mpaka makato yaishe (3, 4 hadi miaka 5). Kaa tafakari vizuri.