Somo zuri ila ukumbuke pesa haitoshi
Wengi wanavyo anza kuchukua mikopo huwa na mawazo kama yako ila baada ya kuchukua na kulipa hujikuta wakibaki katika kutafuta mkopo mkubwa zaidi
Sababu ni za wengi
Baada ya kuwa na pesa hujiingiza katika uwekezaji wa miradi mingi ambayo huwa haiwezi kurudisha hela kwa haraka kwa mfano watu hujikuta wanajenga nyumba za kupangisha ambazo haziwezi kukupa matokeo ya haraka na ukawa na mtaji tena
Wengi hujikuta wako katika kutafuta sifa kwa kuwa na biashara kubwa sasa ukimwambia abaki na mtaji wake halisi baada ya kulipa mkopo atajikuta amerudi nyuma km za kutosha hivyo itamlazimu kutafuta mkopo ili kubaki juu kibiashara
Lakin pia wapo wanao uza dhamana kwa lengo la kuhamisha makazi maana najua akiuza nyumba haiwezi kufika uhitaji wa pesa anayo taka hivyo anaingia benk na kuchukua mkopo mkubwa na kutelekeza dhamana wewe unao kafilisika kumbe kauza kwa njia nyingne
Pia wapo ambao kazi yao ni kuhamisha madeni hawa hujikuta hawapati hata faida zaidi hufaidisha benk na hawa ndio hufirisika kabisa
Kwa Leo nifikie hapa