Kwanza niharakishe kuandika kuwa mimi ni mfuasi wa Tundu Lissu, kuanzia jioni hadi asubuhi, siku saba za wiki. Lakini pili, kama mwanachama wa kawaida wa CDM, Lissu ni kiongozi wangu. Na ieleweke pia sifurahii mambo ya kijinga ya wenye dola dhidi ya Lissu, kiasi cha kumpunguzia muda wa kufanya shughuli zake za kichama na serikali. Kisha niseme tu kuwa andiko hili halina lengo lolote isipokuwa kutoa elimu ndogo tu lakini muhimu.
Kinachoitwa Uchochezi, (mahakama ndio inajua) ni ule ujasiri wa kusema kweli mbele ya domo la dubu (beast) asiyependa kusikia ukweli usiompa nafasi ya kupendwa. Ukweli unaomnyima nafasi ya kuchekewa na ya watu wasiofikiri. Ni ujasiri huo, ndio unafanywa wenye dola kufikiri mambo mengi mengi.
Katika moja ya mambo yanayoweza kumpa mtu ujasiri wa kutisha (kama wa Lissu) ni matumizi ya baadhi ya dawa, Mfano, Benzos, Met-amphetamine na heroine (ikitumiwa kwa kiasi kidogo).
Na marijuana bila shaka.
Sasa, dawa hizo na zingine zinapotumiwa na mtu, huzunguka kwenye damu hadi zinapofika kwenye ubongo a na kuleta athari zake, (kulewa, kuchamaka, nk). Dawa hizo zinharibiwa na/au kuchujwa kwenye Ini au Figo (inategemea aina ya dawa). Baada ya hapo, kinachopatikana hutolewa mwilini kama sumu kwa njia ya hewa, jasho au mkojo. Lakini mara nyingi na kwa kiasi kikubwa, mkojo!.
Kwa hiyo, naweza kusema kuwa waliompima Lissu mkojo walihisi ujasiri wake unatokana na matumizi ya dawa za kulevya. Na kwa hiyo wakataka uthibitisho. Baadhi ya dawa zinaweza kuonekana hata kama mtu amekaa miezi bila kutumia.
Nahisi nimeeleweka! Nimesubiri Lumumba wajitetee hadi nimechoka.
Elimu imekuwa bidhaa adimu siku hizi!
Sent using
Jamii Forums mobile app