Mkoa wa mara ni jimbo lililojitenga? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkoa wa mara ni jimbo lililojitenga?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Jumakidogo, Dec 30, 2010.

 1. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #1
  Dec 30, 2010
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Mkoa wa Mara, ni jimbo lililojitenga?


  Wiki chache zilizopita dunia nzima ilishuhudia unyama wa aina yake waliofanyiwa wasichana wadogo huko Mkoani Mara kwa kuwakeketa na kuwashuahia heshima pamoja na ubinadamu wao.
  Serikali ya Tanzania inapinga vikali vitendo vya ukeketaji, lakini hata hivyo hali hiyo imekuwa tofauti kidogo Mkoani Mara.
  Huko tumeshuhudia kwa macho yetu viongozi wa serikali kuanzia ngazi za chini mpaka zile za juu wakishangilia huku wakisindikiza kwa macho sherehe haramu za ukeketaji huko Mara.
  Je huko hakuna jeshi la polisi? Je wakati waandishi wa habari wakipiga picha na kuripoti matukio yale yaliyokuwa yakifanyika hadharani polisi hao walikuwa wapi? Hapa nashindwa kuelewa uzito wa makosa ambayo jeshi la polisi huwa likiyachukilia hatua kwa haraka ikiwa ni pamoja na kupiga watu mabomu ya machozi, kuwachapa virungu pamoja na kutumia nguvu nyingi na mabavu ya kila aina.
  Je kitendo cha wanachuo wa chuo kikuu wanapoandamana kwa kudai haki zao kina hatia gani zaidi ya wale wanaofanya vitendo vya kinyama kwa kuwakeketa watoto wao hadharani huku wanaume watu wazima vijana na, watoto wakishangilia?
  Je, jeshi la polisi linayo mafunzo ya kukabiliana na maandamano ya wakereketwa wa CUF tu wanaodai katiba mpya na halina ubavu wa kupambana na wabakaji wa haki za watoto?
  Nina wasiwasi, nina wasiwasi mkubwa siku moja huko mara watoto watabakwa mbele ya kituo cha polisi huku wanausalama hao wakishangilia.
  Tunajua na tunao uhakika kuwa mikoa mingi hapa nchini bado inaendeleza mira hiyo katili lakini wanafanya kwa uficho na usiri mkubwa kwa kuogopa vyombo vya usalama, kilichofanyika huko Mara ni dharau kubwa sana kwa serikali na aibu kwa Taifa. Huo ni unyama na ukatili mkubwa ambao serikali haikupaswa kabisa kuufumbia macho.
  Ni unyama ambao kamanda wa polisi wa mkoa wa Mara pamoja na viongozi wa Mkoa huo leo hii hawakutakiwa kuwepo madarakani.
  Hawa walitakiwa wajiuzulu kutoka katika nyadhifa zao ili wawachie watu wenye uwezo wa kuendeleza mapambano dhidi ya vitendo hivyo vya kinyama.
  Kwa mtazamo wangu naona kuwa Mkoa huo ni sawa na jimbo lililojitenga lenye katiba na sheria zake lenyewe.
  Pamoja na matukio hayo ya ukeketaji mkoa huo pia unavituko vingi vya kusisimua ikiwemo kilimo cha bangi kilichopindukia.
  Imefikia wakati sasa kwa serikali hii butu kujaribu kupeleka makucha yake hayo hata kwa kujilazimisha ili kumaliza matatizo mengi yanayouandama mkoa huo ikiwa ni pamoja na migogoro ya kikoo.
   
 2. spencer

  spencer JF-Expert Member

  #2
  Dec 30, 2010
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 2,791
  Likes Received: 1,337
  Trophy Points: 280
  UNAULIZA TENA??

  Polisi wenyewe wanapatia mafunzo kule sasa kama wao ndio walimu nani wa kuwagusa?

  Yaani Mara ni sawa na Amerika na IsraeL, Jeshi lote watuwa Mara kama Jeshi la America na IsraeL
   
 3. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #3
  Dec 30, 2010
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  crap
   
Loading...