Tetesi: Mkoa wa Mara kugawanywa

Brigedia Chan-ocha

JF-Expert Member
Mar 7, 2014
1,353
2,846
Kuna taarifa ambazo bado ni tetesi kuwa Mkoa wa Mara unategemea kugawanywa na kuwa mikoa miwili, Taarifa zinasema, kutakuwa na Mkoa wa Mara kaskazini na Mara kusini, hali kadhalika, wilaya kadhaa zitaongezeka ili kukidhi mahitaji ya kimkoa.

Taarifa zinadai kuwa, Makao makuu wa Mkoa mpya wa Mara kaskazini yatakuwa UTEGI ambapo kutakuwa na wilaya kama RORYA, SHIRATI, TARIME, SIRALI na Nyamongo, hivo hivo, Mkoa mpya wa Mara kusini utabaki na wilaya zake kama Msoma mjini, Butiama, Serengeti, na wilaya zingine.

Haijafahamika mara moja nia na dhumuni la kuugawa huu mkoa, ila kwa maoni yangu, sioni sababu ya kuugawa huu mkoa.
 
Kama ni kweli, upande wa north Mara wamechemka. Utegi ipo pembeni mno na hizo wilaya tajwa bora yangekuwa Tarime mjini
 
dhana ya kubana matumizi imesimamia nn hasa...

Afu pia kugawanya mkoa wa Mara ni mkurupuko wa kiwango cha juu.

Namna mkoa wa Mara ulivyo kaa kama si sababu za kisiasa tu haufai kugawanywa.

Kama itakuwa ndivyo Mara kusini itakuwa na viazi vingi kwa swala la uchaguzi.
 
Mkuu, yaan mimi sijapenda kabisa huu mkoa ugawanywe, wauache hivo hivo, mimi ni wa huko, ila hili swala la kuugawa silipendi kabisa,
 
Kama ni kweli, upande wa north Mara wamechemka. Utegi ipo pembeni mno na hizo wilaya tajwa bora yangekuwa Tarime mjini

Labda wewe ni mgeni wa maeneo husika, kutoka tarime mjini kwenda utegi ni km 23, kutoka sirari kwenda tarime mjini ni chini ya 10 km, huu ni umbali mfupi sana kuliko anayetoka Kinesi kwenda utegi au Kogaja au Masonga/Bubombi. Kwahiyo kama hoja ni kuwa katikati basi UTEGI ndiyo mahali sahihi, kwani hapo atakayekuwa mbali kidogo ni wa Nyamongo lakini pia huyu atatumia barabara ya lami kwa sehemu kubwa. Lakini kama ni kweli basi hata makao makuu ya mkoa wangeweka pale Ingri juu walikoweka makao makuu ya wilaya ya Rorya maana huko fidia itakuwa ndogo kuliko UTEGI au kama ni utegi basi wakajenge kule HBU au FARM (KIWANDANI).
Nimefanya kazi huko mpaka nikatoka na mutoto wa kijaluo ,nikawa mwenyeji sana. wajaluo ni wakarimu sana aisee.
 
Kama ni kweli Mara Kusini utakuwa mkoa masikini zaidi kanda ya ziwa
 
Kama ni kweli, upande wa north Mara wamechemka. Utegi ipo pembeni mno na hizo wilaya tajwa bora yangekuwa Tarime mjini

Hahahaaa aisee nilikuwa sijaona avator yako kumbe ni NYAUCHO wewe lazima upendekeze makao makuu yawe tarime maana unajua SHIRATI SI RAHISI (kwa sababu ni pembezoni sana) na utegi pia huwezi support kwasababu mnazozijua toka issue ya wilaya ianze. By the way msalime sana ndg mheshimiwa Mabere Marando Nyaucho, hv si wewe uliyemkashifu enzi zile za kampeni kati yake na sarungi mwaka 2000 japo ndiye aliyekusomesha?. Aisee binadamu wabaya sana (Utani tu mkuu)
 
Magu alishaweka wazi kuwa kwenye kipindi chake hakutakuwa na migawanyo mpya sababu za gharama kubwa
 
Mara nzima ina watu laki nane kwahiyo kila mkoa utakua na watu laki nne nne oky sio mbaya
 
Kuna taarifa ambazo bado ni tetesi kuwa Mkoa wa Mara unategemea kugawanywa na kuwa mikoa miwili, Taarifa zinasema, kutakuwa na Mkoa wa Mara kaskazini na Mara kusini, hali kadhalika, wilaya kadhaa zitaongezeka ili kukidhi mahitaji ya kimkoa.

Taarifa zinadai kuwa, Makao makuu wa Mkoa mpya wa Mara kaskazini yatakuwa UTEGI ambapo kutakuwa na wilaya kama RORYA, SHIRATI, TARIME, SIRALI na Nyamongo, hivo hivo, Mkoa mpya wa Mara kusini utabaki na wilaya zake kama Msoma mjini, Butiama, Serengeti, na wilaya zingine.

Haijafahamika mara moja nia na dhumuni la kuugawa huu mkoa, ila kwa maoni yangu, sioni sababu ya kuugawa huu mkoa.

Deutoronomy 27:17 : Curse be unto him who removes the mark of the ancient land
 
hamna kitu kama hicho kamkoa kenyewe kadogo sana ,hakana sifa
utegi kuwa makao makuu ya mkoa ni ndoto wanazoota mchana tu ukoo wa sarungi
 
Back
Top Bottom