Mkoa wa Kilimanjaro watangaza rasmi kuwa na uhaba mkubwa wa Chakula

Azarel

JF-Expert Member
Aug 25, 2016
28,410
39,480
Habarini Wakuu,

Muda si mrefu yaani hata nusu saa hazijapita nimesikia katika taarifa ya habari ya TV 1 kuwa uongozi wa mkoa wa Kilimanjaro umetangaza wilaya ya Hai kuwa na upungufu sana wa chakula.

Hali halisi ya mashambani imeoneshwa, ni mazao mengi sana yamekauka kwa kukosa mvua na walalamikaji ni wakulima wenyewe.

Imetangazwa kuwa Mkoa wa Kilimanjaro una uhitaji wa Tani 400 za chakula ili kukidhi mahitaji ya chakula kwa wananchi wa mkoa huo.

Huo ni mkoa ulioko kaskazini mwa Tanzania ambao mara nyingi unaexperience mvua mara kwa mara kwani ni eneo la kitropiki.

Sasa nikisikia kuna mikoa yenye njaa sanaa hasa mikoa ya kimediteranean kwa kukosa mvua ni kwanini nisiamini?

Tunaomba serikali iwakumbuke kwa chakula watu wa Kilimanjaro.

Nawasilisha.
 
Sinauhakika kwa Kilimanjaro wasiwasi wangu kunakina mbowe majimbo yote mh!!!!!
 
Habarini Wakuu,

Muda si mrefu yaani hata nusu saa hazijapita nimesikia katika taarifa ya habari ya TV 1 kuwa uongozi wa mkoa wa Kilimanjaro umetangaza wilaya ya Hai kuwa na upungufu sana wa chakula.

Hali halisi ya mashambani imeoneshwa, ni mazao mengi sana yamekauka kwa kukosa mvua na walalamikaji ni wakulima wenyewe.

Imetangazwa kuwa Mkoa wa Kilimanjaro una uhitaji wa Tani 40 za chakula ili kukidhi mahitaji ya chakula kwa wananchi wa mkoa huo.

Huo ni mkoa ulioko kaskazini mwa Tanzania ambao mara nyingi unaexperience mvua mara kwa mara kwani ni eneo la kitropiki.

Sasa nikisikia kuna mikoa yenye njaa sanaa hasa mikoa ya kimediteranean kwa kukosa mvua ni kwanini nisiamini?

Tunaomba serikali iwakumbuke kwa chakula watu wa Kilimanjaro.

Nawasilisha.
Jimbo la KUB
 
Kushindia uji na maembe kwenu ,haimanishi kuwa Tanzania kuna baa la njaa.

Kuna tofauti kubwa kati ya mtu fulani kuwa na njaa na nchi ya Tanzania kukumbwa na njaa.

Njooni Rukwa, Mbeya, Njombe, morogoro chakula kinaozea shambani

Nyumbu mlielewe hili.
Mbona miaka yote wasilalamike?

Sasa kama kuna mikoa ambayo chakula kinaozea shambani si serikali idistribute katika mikoa yenye njaa?
 
Mimi kipato changu haba Lakini hakuna siku nimeomba Msaada serikalini Zaidi ya kupigia akili nitatokaje?? Sasa nini tofauti ya mkulima Na mfanyakazi kiasi kwamba Mwingine ionekane ipo haja ya kumsaidia??
 
Hai jimbo la mbowe,watapelekewa kweli chakula cha msaada.I dont think so.
 
Back
Top Bottom