Wakuu,
Mkoa wetu wa Kagera umekutana na majanga mazito kuliko mkoa wowote Tanzania. Pengine kila Rais aliyetawala Taifa hili kakutana na hayo mapigo ya mkoa wa Kagera!
Mwl Nyerere alipigana vita kuukomboa mkoa wetu mikononi mwa Idd Amin! Mh Mwinyi yeye akakumbana na pigo la ugonjwa wa ukimwi kuteketeza wananchi na kuacha miji ya watu ikijaa makaburi na yatima wengi.
Mh Ben Mkapa yeye akakutana na ajali nzito ya Mv Bukoba iliyoua watu zaidi ya 800 wengi wakiwa wakazi wa huko. Mh Kikwete akakutana na ugonjwa wa mnyauko ulioteketeza migomba kama ugonjwa wa ukimwi ulivyotekeza watu! Mpaka leo bado kuna athari za ugonjwa huo wa Mnyauko.
Mh JPM yeye akakutana na tetemeko la ardhi lililoacha uharibifu mkubwa kuwahi kutokea. Sasa Mh Rais Samia tayari nae amekutana na ajali mbaya ya ndege!
Nafikiri mkoa wetu unahitaji maombi ya kipekee sana! Imekuwa ardhi inayokumbana na kila janga baya linaloibuka. Inawezekana kwenye ulimwengu wa kiroho mkoa huu una potential nzito ndio maana umejaa mashambulizi ya kila aina.
Kama Taifa upo umuhimu wa kufikiria mkoa huu kimkakati kutokana na historia hizi zinazojirudia!
Upuuzi mwingine wa kidini,maombi Tena!!majanga unayoyataja si ya kwanza kutokea,duniani,Kuna nchi zinakumbwa na matetemeko ya ardhi,mafuriko,
Hii ajari imesababishwa na uzembe wa wamiriki wa Ndege,maana naambiwa hawafati kabisa misingi ya matengenezo.
Kuhusu vita ya Kagera,ni kwa sababu Idi amini alitaka kukata mkoa wa Kagera,
Hata kule Mtwara,alshababy walivamia,sasa na penyewe tupige magoti tuombe!!Afrika ina makanisa Mengi na misikiti kuliko sehemu nyingine duniani,na watu wanakesha wakiomba!!ila matatizo hayaishi!!,jibu sio maombi!jibu ni kutumia mbongo na tekinolojia!!
China,Japan hawaabudu huyu Mungu wetu,kimwamposa!!Ulaya makanisa yanabadilishwa kuwa baa,na madanguro!!lakini hawana shida kama hizi za kwetu,
Huu upuuzi wa kutaka kila kitu kitatuliwe kwa kupiga magoti na kuomba,ni upuuzi mtupu,sasa kijana wako amemaliza chuo,unataka mkopo wa bodi akasome Elimu ya juu,sasa maombi yatakusaidia nini hapo!!.?Acha ujinga,Kuna Ndege ya Ukraine ilipigwa kombora ikiwa na watu 850!!
Vipi kuhusu Ukraine inayotwangwa kwa zaidi ya miezi SITA!,na wao wapige magoti waombe!!