Mkoa wa Arusha hatuna deni na mama

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2012
Posts
20,668
Reaction score
42,712
Kwa ambaye hajafika Arusha kwa miaka mitatu iliyopita akienda kwa sasa lazima ashangae kila kitu. Hapa namaanisha mkoa mzima wa Arusha yaani kuanzia Arusha jiji hadi huko wilayani. Yaani mkoa mzima umechafuka maendeleo ndani ya miaka mitatu tu. Mimi hadi naandika huu uzi bado ninatafakari kwa kina hii kasi ya maendeleo mama kaiwezaje?

Kwa mfano Arusha mjini hadi 2020 sehemu nyingi hazikuwa na barabara za lami ila ghafla ndani ya miaka michache lami zimemwagwa hadi mitaa ya ndanindani huko Sokoni 1, Unga Ltd. Kwa sasa unapiga lami kutoka town (france corner) hadi huko Nadosoito wakati lami ilikuwa haifiki hara dampo. Kwa sasa shortcut zimekuwa mingi ile laana. Kikubwa zaidi zinapigwa njia nne town hadi Kisongo, yaani ni hekaheka, Mama anaupiga mwingi.

Huko wilayani Karatu nako sehemu iliyokuwa makao makuu ya vumbi kwa sasa zimetandazwa lami mitaa yote ya mjini. Vumbi imekuwa historia. Na kwa vile mama anaupambania utalii kwa sasa huo mji mdogo umekuwa na camps, lodges na hotel za hadhi ya juu. Wawekezaji wamefurika. Kimsingi ukiitoa Arusha inafuatia Karatu kwa shughuli nyingi za utalii. Huko kaskazini watu wanatajirika sana kwenye uongozi huu wa Dr Mama Samia.

Kwa mkoa wa Arusha mama kafanya makubwa mno. HATUMDAI. Mama Samia ni kiongozi mwema mwenye upendo na watanzania wote. Nilipita Lindi pia naona kwa sasa nao hawako nyuma. Nyumba za kisasa zimejengwa nyingi huko.
 
Kiwanda cha jenero taya wakifufue tu sasa.
 
Lukas mwasamba mwenzako yupo hoi ICU hao lumumba wa kizimkazi hatawajampa matibabu na alikuwa chawa humu
 
Lengo lenu Michadema
Watanzania wasijue maendeleo yanafanywa na Serikali yao chini ya Dk Samia Suluhu Hassan ✍️
 
Umeshinda 98% unalazimisha maridhiano .......na nani ? Kwani umewakosea nini ?
 
kazi na utu, tunasonga mbele pamoja 🤝
 
 

Attachments

  • VID-20260728-WA0031.mp4
    15.6 MB
Wale kenge hawataliona hili kamwe!..
 
Unaongea kama nani hapo arusha? Nani amekupa mamlaka hayo ya kuongelea watu wa arusha
 
Unaongea kama nani hapo arusha? Nani amekupa mamlaka hayo ya kuongelea watu wa arusha
Raia mwenye uoni angavu anayepima mambo kadri siku ziendavyo,tulipotoka na tulipo,wale huwa wana upofu,anaweza tembea kwenye lami nzuri,yeye akaona ni lami ya udongo!
 
Hiliii nalo poyoyo....
Ukiwa chadema be of this type!
*Barabara ya lami,ione ya udongo na mbovu
*Kitu kizuri,kione kibaya sana
*Kiongozi akifa kizuri,mwone hajafanya lolote
--Kwenye akili uone na ujijenge ya kuwa lissu na heche pekee ndiyo wanaweza kufanya vitu vizuri pekee,hata wewe punda yao huwezi kufanya kama wao,ni wao pekee ndiyo wenye uwezo,na watu wote ni lazima wawasikilize wao tu
#FOOLISHDUMBPOOO!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…