Mkoa Mpya wa Songwe na Wilaya mpya zaanzishwa

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
tmp_22312-simbachawene.JPG-2107216549.jpeg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.John Pombe Joseph Magufuli ameidhinisha kuanzishwa kwa mkoa mpya wa Songwe na wilaya nyingine mpya nchini.

Akitoa tamko hilo kwa niaba ya Rais Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Mhe George Simbachawene amesema kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 imempa Mamlaka Rais ya kugawa Nchi kwa kadri ambavyo atakapoona inafaa.

Mhe George Simachawene amesema kutokana na mamlaka hayo aliyopewa Rais jumla ya Wilaya sita na Mkoa mmoja wa Songwe umeanzishwa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na Mkoa mpya wa Songwe umeanzishwa kutoka Mkoa wa Mbeya.

Amezitaja Wilaya mpya zilizoanzishwa kuwa ni Wilaya ya Songwe Mkoa wa Songwe,Wilaya ya Ubungo Mkoa wa Dar es salaam, Wilaya ya Kibiti Mkoa wa Pwani, Wilaya ya Kigamboni Dar es salaam, Wilaya ya Mlanyi Mkoa wa Morogoro na Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi

“ Nichukue fursa hii kuwaagiza Wakuu wa Mikoa wote ambao Wilaya mpya zimeanzishwa kufanya maandalizi rasmi ili Mkoa na Wilaya hizo ziweze kuanza kufanya kazi,aidha mkazo uwekwe kwenye upatikanaji wa Ofisi na huduma zote muhimu kupatikana kwa urahisi katika Mkoa naWilaya hizo mpya” Alisema Mhe Simbachawene.
 
Hapo matumizi yanabanwa kwa kusogeza huduma karibu zaidi kwa wananchi,mbn kwa akili ya darasa la pili tu unapata jibu mkuu??
Swali lako jepesi sana,ingawa limekaa kimajungu.
Mimi sijasoma mkuu, hebu nifafanulie vizuri....hapa unaongeza matumizi au unabana matumizi...nijuavyo unavyoongeza idadi ya Watoto ndivyo na matumizi ya pesa yanaongezeka..
 
Hii ni moja ya namna za kupunguza au kubana matumizi.

Go magu go!!!!

Ni vema tu
Ndiyo maana nafikiri priorities za magu ziko upside down. Kama mkakati unahusisha kubana matumizi then kuongeza government expenditure si namna. Ngoja tuone mambo yatakuwaje mwishoni!

Huduma za msingi na za umma hutolewa kwa urahisi zaidi zikiwa karibu na wanajamii. Aidha kinachoshajihisha ugawaji wa naeneo kiutawala ni pamoja na kuwajengea uwezo zaidi wanajamii wa kuzalisha ili kukuza uchumi kupitia miundo mbinu inayosindikiza uanzishaji wa maeneo hayo mapya. Suala la msingi ni kuhakikikisha makao makuu ya wilya na mikoa hiyo ipo mahali muafaka?
 
Pamoja na maelezo marefu uliyo toa hakuna kitu kinacho itwa kubana matumizi hapo, matumizi yanaongezeka ila ufanisi wa kutoa huduma kwa jamii husika ndio unaboreshwa
 
Mzee WARIOBA, H, POLEPOLE, JONSON MBWAMBO, wanaweza kulamba ukuu wa mkoa au wilaya.
 
naikumbuka ile mikoa niliyojifunza drs la 3 mikoa 21 bara visiwani5...ilikuwa mikoa kweli ukifika iringa ,mbeya,kagera,shy,dsm,tanga..unaona ni mikoa kweli makao makuu mipango miji..huduma ..hii mipya kama manyara...Dhu pamoja nakujengwa bado hadhi inabakia ile ile wilaya tu...
 
View attachment 320990

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.John Pombe Joseph Magufuli ameidhinisha kuanzishwa kwa mkoa mpya wa Songwe na wilaya nyingine mpya nchini.

Akitoa tamko hilo kwa niaba ya Rais Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Mhe George Simbachawene amesema kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 imempa Mamlaka Rais ya kugawa Nchi kwa kadri ambavyo atakapoona inafaa.

Mhe George Simachawene amesema kutokana na mamlaka hayo aliyopewa Rais jumla ya Wilaya sita na Mkoa mmoja wa Songwe umeanzishwa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na Mkoa mpya wa Songwe umeanzishwa kutoka Mkoa wa Mbeya.

Amezitaja Wilaya mpya zilizoanzishwa kuwa ni Wilaya ya Songwe Mkoa wa Songwe,Wilaya ya Ubungo Mkoa wa Dar es salaam, Wilaya ya Kibiti Mkoa wa Pwani, Wilaya ya Kigamboni Dar es salaam, Wilaya ya Mlanyi Mkoa wa Morogoro na Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi

“ Nichukue fursa hii kuwaagiza Wakuu wa Mikoa wote ambao Wilaya mpya zimeanzishwa kufanya maandalizi rasmi ili Mkoa na Wilaya hizo ziweze kuanza kufanya kazi,aidha mkazo uwekwe kwenye upatikanaji wa Ofisi na huduma zote muhimu kupatikana kwa urahisi katika Mkoa naWilaya hizo mpya” Alisema Mhe Simbachawene.
Duh wilaya ya mtama haipo mbona tulichagua kwa wingi ccm tukitegemea mtama kupata wilaya kila kitu tunacho kwa nini magu ametubania
 
Wilaya sita na Mkoa mmoja wa Songwe umeanzishwa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na Mkoa mpya wa Songwe umeanzishwa kutoka Mkoa wa Mbeya.

Amezitaja Wilaya mpya zilizoanzishwa kuwa ni Wilaya ya Songwe Mkoa wa Songwe,Wilaya ya Ubungo Mkoa wa Dar es salaam, Wilaya ya Kibiti Mkoa wa Pwani, Wilaya ya Kigamboni Dar es salaam, Wilaya ya Mlanyi Mkoa wa Morogoro na Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi

Hayo makusanyo ya mapato sasa si ndiyo yataishia kulipa wakuu wa hizo wilaya na wakurugenzi, ndiyo maana culture ya watanzania kuongeza walaji baada ya vipato kuongezeka haiishi, kila laki inayoongezeka kwenye mshahara inavuta bibi mpya
 
Back
Top Bottom