Idd Ninga
JF-Expert Member
- Nov 18, 2012
- 5,205
- 4,403
UKIWAHISI WAPIGE.
1)mnamshangaa mwewe,kuku avyo watafuna.
Sema udakwe na wewe,cha moto utakiona
Usemwe na ushangawe,jama lazidi kutuna
Ukiwahisi wapige,hakimu akose kazi.
2)vipanga wanadonoa,tai alishakunena.
Vibeji atawagea,vinyota kubandikyana.
Mengi mtajionea,mtajuta kupeana.
Ukiwahisi wapige,hakimu hakose kazi.
3)nao watoa hukumu,mahakimu kubanana.
Jitu likaanga sumu,laanza kuchukizana.
Kifika kule na humu,wenzake watatengana.
Ukiwahisi wapige,hakimu akose kazi.
4)wala hawanyamazishi,ndivyo tulivyoagana ?
Majibu yasi uzushi,tukaja kutibuana.
Mdogo mdogo moshi,hauzimiki mchana.
Ukiwahisi wapige,hakimu akose kazi.
5)kwani kesho ipo mbali,na jana za karibyana.
Itawa kama ajali,kwa nguvu wataachana.
Hakuna atae jali,kama kwa kuumizana.
Ukiwahisi wapige,hakimu akose kazi.
Shairi:UKIWAHISI WAPIGE.
Mtunzi:Idd Ninga wa Tengeru Arusha.
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com
1)mnamshangaa mwewe,kuku avyo watafuna.
Sema udakwe na wewe,cha moto utakiona
Usemwe na ushangawe,jama lazidi kutuna
Ukiwahisi wapige,hakimu akose kazi.
2)vipanga wanadonoa,tai alishakunena.
Vibeji atawagea,vinyota kubandikyana.
Mengi mtajionea,mtajuta kupeana.
Ukiwahisi wapige,hakimu hakose kazi.
3)nao watoa hukumu,mahakimu kubanana.
Jitu likaanga sumu,laanza kuchukizana.
Kifika kule na humu,wenzake watatengana.
Ukiwahisi wapige,hakimu akose kazi.
4)wala hawanyamazishi,ndivyo tulivyoagana ?
Majibu yasi uzushi,tukaja kutibuana.
Mdogo mdogo moshi,hauzimiki mchana.
Ukiwahisi wapige,hakimu akose kazi.
5)kwani kesho ipo mbali,na jana za karibyana.
Itawa kama ajali,kwa nguvu wataachana.
Hakuna atae jali,kama kwa kuumizana.
Ukiwahisi wapige,hakimu akose kazi.
Shairi:UKIWAHISI WAPIGE.
Mtunzi:Idd Ninga wa Tengeru Arusha.
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com