ndayilagije
JF-Expert Member
- Nov 7, 2016
- 7,490
- 8,305
Mpenzi Mwantumu,mke nikupendaye sana.
Pole kwa yaliyokupata.Ni miezi 5 tangu uondoke nyumbani,nyumba imezubaa sana natamani kelele na kero zako kwani zilishakuwa sehemu ya familia yetu.
Nilikuoa 2015 mbele ya makasisi na mashehe, mchana wa jua kali baada ya kutimiza masharti yote ya mila na desturi.
Tangu nikuoe hujawahi kuwa mke mwema!mara uniite majina ya kuudhi,nikisema unasema,mpaka watoto umewafundisha kutoniheshimu. Nilikuonya hukusikia,ukaanza kuwa na mahusiano yanayotia shaka na wanaume lukuki,ukiniambia utahakikisha wananikomesha.!eti wataninyoa bila maji!nikavumilia.
Sina hakika kama uliwagonganisha lakini nikasikia wamekupiga.Nikataka kukupeleka hospitali ukasema huhitaji msaada wangu.Ukaondoka na kwenda kutibiwa na pedeshee wako.
Juzi nimesikia wamekuhamishia huko mbali zaidi. Lakini unataka nigharimie matibabu yako huko.
Mwantumu mpenzi,watoto wananisumbua sana,nikiwapiga wananiita dikiteta eti. Kwa kuwa mimi ni mzazi siwezi kuwaacha wafanye kila wanalotaka,napambana nao.
Upatapo salaamu zangu darling juwa wewe ni mke halali na bado nakusubiri turekebishe tofauti zetu,uniambie nani aliyekudhuru na ikiwezekana sheria ifate mkondo wake,ya nini kuwafichaficha? hata kama walikufumania hawakupaswa kukuvunja miguu,kwanza na wao ni wezi tu.
Ugua pole baby,ila kumbuka kiapo cha ndoa yetu pale uwanja wa taifa.
Nitabaki kuwa mume wako mpaka hapo 2025.