Mkenya kortini kwa makosa 58 ikiwemo utakatishaji wa fedha

Zurie

JF-Expert Member
Jul 6, 2014
2,002
5,534
Stanley Murithi Mwauru (38), Raia wa Kenya, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam akikabiliwa na makosa 58 likiwemo la utakatishaji wa fedha Sh. Milioni 800.

Inadaiwa kuwa mnamo tarehe 7 mwezi Mei mwaka jana Stanley aliighushi nyaraka kwa lengo la kujipatia fedha kupitia hundi feki na kujipatia Sh.9,800,750 kwa lengo la kuonesha zimesainiwa na Ahmad Zacharia na Vida Zacharia na alijipatia pesa hizo katika benki ya Azania.

Katika shitaka la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, inadaiwa alilitenda kati ya Januari mosi 2013 na Mei 31 mwaka huu jijini Dar es Salaam katika benki ya Azania na kujipatia Sh. Milioni 805.3.

Katika shitaka la utakatishaji fedha inadaiwa alilitenda kati ya Januari mosi 2013 na Mei 31 mwaka huu jijini Dar es Salaam ambapo alidai amejipatia Milioni 805.3 ikionesha imesimamiwa na Kituo cha Professional Paint katika Benki ya Azania, huku akijua kuwa fedha hizo zimepatikana kwa makosa.

Mshitakiwa alikana tuhuma hizo na kesi iliahirishwa na Hakimu hadi Juni 20, mwaka huu na mshtakiwa amekosa dhamana kutokana na kosa la utakatishaji fedha linalomkabili.
 
Ilikuwaje sijaelewa vizuri,izo pesa alipiga kwa mkupuo mmoja?
 
Kama alipiga kidogo kidogo kuna watu azania bank wanahusika
 
Back
Top Bottom