Mke wangu ni HIV Positive

ishi nae tu ila mkapate ushauri nasaha. pia ukimuacha huyo mkeo utamuongezea stress
 
Mkuu mengi yamesemwa lakini kumbuka ule UPENDO wa awali! We huna uhakika kama hujaambukizwa! na yeye hakujua hata ni lini na nani aliyempa. nenda kwa washauri nasaha/wataalam upate jinsi ya kuishi na VVU! Ila kumwacha ucfikirie! nafahamu watu walikuwa na case kama yako na wana miaka 8 sasa ktk ndoa yao na watoto 2!
 
Habari zenu wana JF.

Poleni na mihangaiko ya wiki nzima na leo hatimaye mmerejea kulijenga taifa. Jamani nimejitokeza leo kuwaeleza true story ya maisha yangu na kama kuna ushauri basi nitaupokea. Mimi nilioa kwa ndoa takatifu mwez Sept 2012. Ilipofika Nov 2012 Mke wangu alipata ujauzito na kila m2 kati yetu akawa na furaha.

Sasa ilipofikia muda wa kwenda clinic kama ilivyo ada mnatakiwa kuwa wote ili kuweza kupata nasaha na hatimaye kupima maambukizo ya HIV. Baada ya yote tukapima na yeye Mke wangu akakutwa anaishi na virus va UKIMWI na mimi niko salama kabisa. Kwel alilia sana na Nurse akapata shida sana ya kumbembeleza hatimaye akatulia na tukatoka akwa na uso wa tabasamu bandia.

Tulipofika nyumban kilio kilianza upya na mimi nikionekana usoni sina hata lepe la hofu wakati moyoni nilikuwa naumia sana. Baadae ucku akaniomba kuwa kwa sababu Kanisani tulifundishwa kuwa ndoa yaweza vunjwa kama mmoja wapo akionekana ni malaya. Ki ukwel mimi nilimkatalia nikamwambia Mi ni wake mpaka kifo kitakapo tutenganisha, wala hakuamini macho yake.

Kwa sasa anaonekana yuko at least normal ki akili na leo ameenda kazini. Yeye binafsi ni muumini mzuri na anapenda kwel kuimba na kumsifu Mungu. Naomba ushauri wenu tafadhali.

Ushauriwangu ni hapo kwenye blue line brother.
 

Du nimesoma ushauri wako hadi chozi limenitoka.ushauri mzuri sana.big up
 
KAka ukimwi usiwe sababu ya kumuacha mke wako,ukifanya hivyo utamuua mapema. pia tambua wapo wenye ukimwi na hadi leo wanadunda na wanazaidi ya miaka 27 wakiwa wanaumwa. kaka kaa na daktari akushauri namana ya kufanya mapenzi na mkeo na namna ya kumfariji. binafsi nakuombea na tambua ukimwi hupo kila nyumba!!!!!!!!!!!!!! kaka bado yapo maisha na mafanikio mbele yenu
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…