Mke wangu kaolewa

Dr leader

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2016
Posts
1,041
Reaction score
1,294
MKE WANGU KAOLEWA

Namuombea laana, yeye na kizazi chake
Asipate cha maana, yeye na wazazi wake
Naamba kwa maulana, kumhusu mja wake
Mke wangu kaolewa

Nilifanya kila hali, wao wapate amani
Haramu au halali, chakula kiwe tumboni
Kupata sio sahali, hakuridhika mwandani
Mke wangu kaolewa

Bora angeniarifu, taraka yake nimpe
Hilo ameligharifu, hata nguo nisimpe
Hatukuwa na khirafu, tuligandana ja kupe
Mke wangu kaolewa

Kanitumia barua, hana haja ya taraka
Mimi ndo nitaamua, taraka au baraka
Sisemi nitamuua, ila hatapata faka
Mke wangu kaolewa

Na yule Shekhe kuwadi , aliyepewa utamu
Ndoa yenye uhasidi, kawabiriki, karamu
kabla siku ya ahadi, nitamtia hatamu
Mke wangu kaolewa.

✍️Abuuabdillah

 
Jipe miaka 2 soma haya unayoandika utajua jinsi gani ulikuwa mpumbavu, wanawake hawana maana; Ishi nao kama unaishi na Jirani, akihama, wewe tafuta Nyumba ingine kama Kodi hutaiweza!
 
Weeeeeeee.... bado hatujasahau yalomkuta Penina wa Goba mshangazi nginjanginja komasava, alivyokula hela ya msukuma hadi akageuzwa bucha..🤣
 
Weeeeeeee.... bado hatujasahau yalomkuta Penina wa Goba mshangazi nginjanginja komasava, alivyokula hela ya msukuma hadi akageuzwa bucha..🤣
Hebu nielezee kidogo hiyo story
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…