Mke wangu kanihamishia familia yake yote kwangu

kingdon

Senior Member
Feb 15, 2012
121
61
Mimi nina mke wangu tuna miaka kama nimetoka tuoane ndoa ya kanisani, mwanzoni mke wangu alikuwa mtulivu sana ila baada ya kupata mtoto visa vikaanza nilikuwa nakaa na mtoto wa dada yangu akamfukuza kisa eti anamdharau, mimi nikanyamaza maana ni mtu wa safari za kikazi sana.

Akaanza akamleta mdogo wake akaniambia nimtafutie chuo nikatafuta akaanza kusoma, kukaa kidogo akamleta mama ake mdogo nyumbani bila kunipa taarifa akakaa, aichukua mda akamleta kijana bila kuniambia eti ni mfanyakazi kwenye biahara zake ameona akae pale nyumbani.

Nikawa natafakali ila nikaa kaa kimya,kuna siku nimemuomba simu yake kuna namba nilikuwa nachukua nikakuta katumiana sms na mama ake mdogo ambaye yuko apa nyumban kwamba sisi wababe tumemleta uyu kijana bila kumtaarifu jamaa na kaka bila shida,.

Sasa cha ajabu kawaleta tena wadogo zake wawili bila taarifa narudi kutoka kazini nawakuta, sasa najiuliza huyu mke anamatatizo gani au ananidharau au kuna kitu anatafuta? Sikatai kukaa na ndugu zake lakini si tuna discuss sasa yeye anawaleta bila kuniambia na wakifika hasemi kitu na mimi namnyamzia.

Ila kwasababu ana biashara nilimfungulia nataka kuacha kutoa matumizi na kusitisha kutoa ada kwa mdogo wake, maana kuna siku nilimkuta mdogo wake nyumbani katoka chuo alikuwa anadaiwa ada nikampa pesa akalipe ada, dada mtu kujua nilimpa pesa ya ada anasema uyo mdogo wake ni hawara yangu kwanini nimpe pesa ya ada na nisimpe yeye mke wangu ampe.

Naombeni ushauri seriously
 
me nina mke wangu tuna miaka kama mine toka tuoane ndoa ya kanisan,mwanzon mke wangu alikuwa mtulivu sana ila baada ya kupata mtoto visa vikaanza nilikuwa nakaa na mtoto wa dada angu akamfukuza kisa eti anamdharau me nikanyamaza maana ni mtu wa safari za kikaz sana,akaanza akamleta mdogo wake akaniambia nimtafutie chuo nikatafuta akaanza kusoma,kukaa kidogo akamleta mama ake mdogo nyumban bila kunipa taarifa akakaa,aikuchukua mda akamleta kijana bila kuniambia eti ni mfanya kaz kwenye biahara zake ameona akae pale nyumban,nikawa natafakali ila nikaa kaa kimya,kuna siku nimemuomba simu yake kuna namba nilikuwa nachukua nikakuta katumiana sms na mama ake mdogo ambaye yuko apa nyumban kwamba sisi wababe tumemleta uyu kijana bila kumtaarifu jamaa na kaka bila shida,sasa cha ajabu kawaleta tena wadogo zake wawili bila taarifa narud kutoka kazin nawakuta sasa najiuliza uyu mke anamatatizo gan au ananidharau au kuna kitu anatafuta?,sikatai kukaa na ndugu zake lakin si tuna discuss sasa yeye anawaleta bila kuniambia na wakifika hasemi kitu na mimi namnyamzia ila kwa sababu ana biashara nilimfungulia nataka kuacha kutoa matumiz na kusitisha kutoa ada kwa mdogo wake,maana kuna siku nilimkuta mdogo wake nyumban katoka chuo alikuwa anadaiwa ada nikampa pesa akalipe ada,dada mtu kujua nilimpa pesa ya ada anasema uyo mdogo wake ni hawala yangu kwann nimpe pesa ya ada na nisimpe ye mke wangu ampe?,naombeni ushauri seriously

Hama na wewe mwambie unawapa nafasi utarudi watakapoondoka
 
me nina mke wangu tuna miaka kama mine toka tuoane ndoa ya kanisan,mwanzon mke wangu alikuwa mtulivu sana ila baada ya kupata mtoto visa vikaanza nilikuwa nakaa na mtoto wa dada angu akamfukuza kisa eti anamdharau me nikanyamaza maana ni mtu wa safari za kikaz sana,akaanza akamleta mdogo wake akaniambia nimtafutie chuo nikatafuta akaanza kusoma,kukaa kidogo akamleta mama ake mdogo nyumban bila kunipa taarifa akakaa.

Haikuchukua mda akamleta kijana bila kuniambia eti ni mfanya kaz kwenye biahara zake ameona akae pale nyumban,nikawa natafakali ila nikaa kaa kimya,kuna siku nimemuomba simu yake kuna namba nilikuwa nachukua nikakuta katumiana sms na mama ake mdogo ambaye yuko apa nyumban kwamba sisi wababe tumemleta uyu kijana bila kumtaarifu jamaa na kaka bila shida,sasa cha ajabu kawaleta tena wadogo zake wawili bila taarifa narud kutoka kazin nawakuta sasa najiuliza uyu mke anamatatizo gan au ananidharau au kuna kitu anatafuta?

Sikatai kukaa na ndugu zake lakin si tuna discuss sasa yeye anawaleta bila kuniambia na wakifika hasemi kitu na mimi namnyamzia ila kwa sababu ana biashara nilimfungulia nataka kuacha kutoa matumiz na kusitisha kutoa ada kwa mdogo wake,maana kuna siku nilimkuta mdogo wake nyumban katoka chuo alikuwa anadaiwa ada nikampa pesa akalipe ada,dada mtu kujua nilimpa pesa ya ada anasema uyo mdogo wake ni hawala yangu kwann nimpe pesa ya ada na nisimpe ye mke wangu ampe?.

Naombeni ushauri seriously.
Pole sana, ila inabidi ukae nae chini umueleze haya yoote uliyosema hapa halafu umsikie atasemaje. Ndoa inahitaji kuwekana wazi ili maumivu ya moyo yasitokee. Sasa we mwambie kua hukupenda alivyochukua maamuzi bila kukutaarifu na labda wewe ungependa afanyaje? Apunguze ndugu hapo home au awatoe kabisa mbaki wenyewe. Ndugu wasiwagombanishe.
 
Kwa NDOA ya kanisani (KIKRISTO) familia ya mkeo ni familia yako pia. Nafikiri ushauri unaoweza kukusaidia ni wa wewe kurudi tena na kupata mafundisho ya NDOA upya ....
sikatai familia yake ni yangu si kama kuna ktu anataka kuja kwanza tunadiscuss?,sasa yeye anawaleta bila taarifa nakitu kilichonifanya nione ni makusudi zile sms alizotumiana na mama ake mdogo kwamba wao ni wababe wanaleta mtu na anakaa sisemi kitu
 
Kunakokuponza ni huko kukaa kaa kimya kwako...

Washakuona boya, ipo siku watataka uwapishe walale kitandani kwako wenyewe, wewe ukalale na wanaume wenzio chumba kingine huko.....

Timua wote aiseeeeee, life ya mjini na kurundikiana ndugu wapi na wapi.

Walioweka option ya kuformat flash disk ikiingia virus usifikiri ni wajinga aiseee.
 
Umepanga hiyo nyumba au mmejenga? Nataka kujua ili uangalie option ya kutafutaKwa mtindo huo, kwanini mtu asichepuke au asianzishe nyumba ndogo? Hapo ili usiumie anza kujipanga. Ongea naye, kama hawezi kukusikiliza kuhusu kuipunguza hiyo familia basi hapo inabidi wewe ufanye maamuzi magumu.
 
Kwa NDOA ya kanisani (KIKRISTO) familia ya mkeo ni familia yako pia. Nafikiri ushauri unaoweza kukusaidia ni wa wewe kurudi tena na kupata mafundisho ya NDOA upya ....

Sawa, familia yake ni yangu, lakini kila mtu akae kwake. Ingekuwa ni mimi mbaya zaidi hiyo msg wanaambiana wao wababe, ningewaita wote sebuleni na kuwatimulia mbali Point Blank, na mke naye kama angeleta ubishi ningemtimua vile vile, ili next time awe na akili.
 
Nakupa huu ushauri nikiwa nikijiaminisha kweli kwamba umeoa na siyo story za JF.

Ulishakosea toka mwanzo kuruhusu ugeni bila kujadili, ilitakiwa yule mtu wa kwanza kabisa kufika mjadili na mkubaliane kwamba kwa mwingine atakayefata utaratibu ni huo.

Mpaka sasa inaonekana huyo mama yake mdogo kaja kukuharibieni ndoa na atafanikiwa kwa kiasi kikubwa, kwa sababu mpaka sasa anaonekana amemshika masikio wife wako kwa kiasi kikubwa, na wife anafikia kujisifu kwa kukufanya Bushoke.

Usije kushangaa hata mama yake mdogo huyo wakawa na ushirika kwenye maswala ya michepuko (nawaza hivi kwa sababu wanadhani wamefanikiwa kukufanya Bushoke).

Nini kifanyike?

1. Weka kikao na wife, mwambie unataka huyo mama yake mdogo na kijana waondoke mara moja, kama amewaleta wadogo zake na hawana kazi ya kufanya basi wasaidiane naye kwenye hiyo biashara yake. Kama wadogo zake anataka kuwasomesha awasomeshe na wewe usijihusishe na ulipaji wowote wa ada kwa yeyote;

2. Ni marufuku mtu kuja kuishi bila wewe kutoa idhini;

3. Yule mdogo wake aliye shule akimaliza shule straight arudi nyumbani, kama kuna msaada wowote anaweza kupewa akiwa nyumbani, katika kipindi anachosoma anaweza kukaa hapo kwenu; na

4. Kama kuna chochote unachangia kwenye hiyo biashara yake basi sitisha mara moja, mwache aendeshe biashara yake kutoka mfukoni kwake.

NOTE: Kama hayo yakishindikana jua huna mke, ndoa iko ukingoni, mtakuwa mnahitaji msaada wa wakubwa zaidi kuweza kulitatua hilo, wazazi wa pande zote wanahusika, huku maombi yakiwa ni muhimu zaidi kwa sababu tayari kuna doa kwenye ndoa yenu.

Kila la kheri mkuu na hongera kwa busara za kuweza kumvumilia mpaka sasa, ninaamini kama unaipenda familia yako hili utalitatua.
 
Stage ya kwanza: Mtafune huyo mdogo wake.

Stage ya pili: Mtafune mama yake mdogo.

Stage ya tatu: Nunua uwanja bila yeye kujua anza kujenga (na uhakika hata yeye ameanza bila wewe kujua)

Stage ya nne: Sitisha kutoa misaada nyumbani ikiwemo kununua vitu nyumbani

Stage ya tano: Fanya juu chini hakikisha hiyo biashara yake inafirisika na usimuongezee mtaji hao vijana wataondoka wenyewe.

Stage ya sita: Anza kuwaleta ndugu zako hapo kwako.

Stage ya saba: Rudia tabia yako ya uzinzi, ulevi na uvutaji, kila siku rudi usiku sana na weekend geuka popo, akikuuliza unakuwa mkali kama mbogo
 
Umepanga hiyo nyumba au mmejenga? Nataka kujua ili uangalie option ya kutafutaKwa mtindo huo, kwanini mtu asichepuke au asianzishe nyumba ndogo? Hapo ili usiumie anza kujipanga. Ongea naye, kama hawezi kukusikiliza kuhusu kuipunguza hiyo familia basi hapo inabidi wewe ufanye maamuzi magumu.
tumepanga mkuu yetu iko kwenye finishing maana siku wale wawili walivyofika usiku nikamsikia anasema wakakae kwenye nyumba yetu wailinde maana iko kwenye finishing tu ila wapo tu home
 
Back
Top Bottom