Mke wangu anathamini sana kazi kuliko familia

Samahani sijakufahamu uliposema anathamini sana kazi unamaanisha hana mda na watoto wala na wewe au? hiyo kazi ameajiriwa au amejiajiri?
 
ameajiriwa, tuna mtoto mmoja, mara nyingi anasahau vitu vya muhimu kuhusu mtoto na familia, kwa kifupi ni mtumwa wa kazi aliyoajiriwa (mwalimu wa primary)
 
Naanza kupata picha ya jinsi ulivyo na mkeooo... Haya endelea kushusha matusi zaidi
nimekujibu kulingana na ulichoeleza, hilo sio tusi ila ni ukweli. Na kama ungekuwa na busara usingekurupuka kuandika kitu husichokielewa.
 
Kwa namna hii ya uandishi na mpangilio wa fikra inawezekana mkeo hakuelewi.
Boresha uwezo wako wa kuwasiliana ( communication skills)
 
Ndoa nyingi ambazo wanandoa wote wanafanya kazi hazina furaha kabisa....sema ndio hivyo tu kuta zinaficha mambo mengi kweli......
 
Kwa namna hii ya uandishi na mpangilio wa fikra inawezekana mkeo hakuelewi.
Boresha uwezo wako wa kuwasiliana ( communication skills)
wewe unashauri niandikeje, mpangilio wa fikra ukaeje na niboreshe vipi mawasiliano?
 
Ndoa nyingi ambazo wanandoa wote wanafanya kazi hazina furaha kabisa....sema ndio hivyo tu kuta zinaficha mambo mengi kweli......
Wengine hufikia kiasi cha kusema "KAZI YAKE NDO KILA KITU KWAKE" hayo mengine yapo tu ila Mwanaume inabidi uplay part kama kichwa cha House
 
Wengine hufikia kiasi cha kusema "KAZI YAKE NDO KILA KITU KWAKE" hayo mengine yapo tu ila Mwanaume inabidi uplay part kama kichwa cha House
ila kwani maana ya kuwa wawili ndani ya nyumba ni kusaidiana asee

wanawake tuna majukumu mengi kuzidi uwezo wetu sometimes
 
ila kwani maana ya kuwa wawili ndani ya nyumba ni kusaidiana asee

wanawake tuna majukumu mengi kuzidi uwezo wetu sometimes
Sikatai mkuu na kwa kweli mwanamke anaejishughulisha ni mzuri ila isifikie kiasi cha kuisahau au kusahau majukumu yake kama MAMA na mwanaume asisahau majukumu yake kama BABA
 
Back
Top Bottom