chizcom
JF-Expert Member
- Jul 31, 2016
- 7,581
- 15,721
Daaah salama Wananzengo
Huyu mke wangu kila siku anazidi kunenepeana na kutoka kitambi
Baada ya kuzaa mtoto wa pili ndo imekua balaa kila siku anazidi kufumuka tu
Tumbo limekua kubwa yani ana kitambi kumzidi hata Lugola
Wife yeye ni mwendo wa kula kuku na mapocho pocho ,huko kazini anakaa tu kwenye kiti cha kuzunguka yani hana habari, kabweteka jimwili linakuja kasi hadi kero
Nimemshauri atumie tiba mbadala apunguze kitambi au afanya mazoezi apunguze kitambi hataki yani kila siku ananipiga sound tu
Ebu niambieni wana Nzengo njia gani nzuri niitumie huyu mwanamke apunguze mwili awe kimbau mbau manake hata ninapompiga mkuyati kuna baadhi ya style anashindwa kuzichakata vyema.
hapo kwenye tumbo kama wizara ya mambo ya ndani na disco