Mke wangu amehamishia upendo wote kwa watoto. Je, ndio uhalisia wa ndoa zote?

Wandugu poleni na majukumu ya kila siku bhana nisikuchoshe nianze moja kwa moja

Wapwa niko kwenye ndoa mwaka Watano sasa nashindwa kuelewa haya maisha ya ndoa yana uhusiano gani na ya mahusiano kipindi bado hatuna watoto..

Kweli kipindi sina mtoto niko kwenye mahusiano mwenzangu alinipenda sana tofauti na sasa tuna watoto yeye hataki kusikia stori zangu n yeye na wanae swali kwa wanawake ,je ni kweli anapokuwa umezaa upendo wote huelekezwa kwa watoto?

Kama ndio vepe kuhusu mumeo alikuzalisha hastahili upendo au ndo tuwe busy kuijenga familia bila upendo pande zote ...!!!

Dondosha comment yako

Sent using Jamii Forums mobile app

Mueleweshe kwamba watoto ni wapita njia, hawatakiwi kuchukua nafasi yako wala hawatakiwi kuwavurugia mipango yenu.

Asipoelewa, mchukue nenda nae kwenu au kwao, akawaone wazazi wake walivyobaki peke yao, bila shaka ataelewa watoto sio ndugu ni wapita njia tu!
 
Ulikuwa unamnyonya mkeo ila sasa watoto wanamnyonya vema hadi maziwa yanamtoka, una nini cha ziada..?

Mke: “Jitahidi utujengee nyumba ili ukifa mimi na watoto tusihangaike”.

Dadadadeekii.
 
kawaida hiyo vumilia kaka me ilikua hivyo ilanshazoea yaaan unaweza mpelekea mayai tray nzima ile ameyapokea tu anaanza kusema haya ya kwangu na mtoto na ni kweli hupati hata 1 ila mwisho wa siku nlimchana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu iko ivo, nadhani mzee wangu alianza kumzingua Bi mkubwa aisee Upendo wote maza ilibidi auelekezee kwangu na hivo ndo nilikuwa mtoto wake pekee wakiume.

Aisee! sijawahi pata upendo wa kweli kama ule umeni-affect sasa hivi nimekuwa na niko mbali na mama ila kwa siku lazima nimpigie Simu au anipigie zaidi ya mara moja asububi na jioni haiwezi kupita siku sijaongea nae kwa simu na naweza piga nae story hata nusu saa kwa simu.
 
kawaida hiyo vumilia kaka me ilikua hivyo ilanshazoea yaaan unaweza mpelekea mayai tray nzima ile ameyapokea tu anaanza kusema haya ya kwangu na mtoto na ni kweli hupati hata 1 ila mwisho wa siku nlimchana

Sent using Jamii Forums mobile app
Ha ha ha!!

Mimi nilikua naleta maziwa mtindi dumu la litre 5, aisee sipati hata kikombe cha chai mpaka yanaisha. Naambiwa yote ya mtoto.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo mkuu inamcost mzee wako sana maana anaweza asione kama anapata support yeyote kutoka kwako ama ndugu kwasababu alichokianzisha ndicho kinachomgeuka tena aise omba yasikukute
Mkuu iko ivo nadhani mzee wangu alianza kumzingua Bi mkubwa aisee Upendo wote maza ilibidi auelekezee kwangu na ivo ndo nilikuwa mtoto wake pekee wakiume Aisee sijawahi pata upendo wa kweli kama ule umeni affect saivi nimekuwa na niko mbali na mama ila kwa siku lazima nimpigie Simu au anipigie zaidi ya mara moja asububi na jioni haiwezi kupita siku sijaongea nae kwa simu na naweza piga nae story hata nusu saa kwa simu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo n majukumu natimiza daily so kama n kawaida na mm n take ma time kwngne sio

Sent using Jamii Forums mobile app

Mkuu kuna mambo inabidi uelewe na ukubaliane nayo.

Swala la mwanamke kuhamishia mapenzi kwa mtoto hiyo ni nature na kamwe huwezi kuizuia wala kupambana nayo. Kumbuka mtoto anapozaliwa anakua helpless kwahiyo lazima kuwe na mtu wa kumuangalia, na ndio nature ikampa jukumu hilo mwanamke. Sisi wanaume hua hatuko attached saana na watoto zaidi zaidi ni kuleta matumizi tu.

Mistake kubwa tunayofanya waswahili ni kutokupangilia swala la lini tunapata watoto. Watu mkishaoana tu, mnafikiri kwamba ni lazima mpate mtoto as soon as possible! Wengine mnaoana na mimba tayari.

Wenzetu wazungu wanalielewa sana hili na ndio maana wao wanaweza kuoana na wakakubaliana kwamba mtoto wa kwanza tutapata baada ya miaka mitano. Hii inawapa nafasi kubwa ya kujivinjari bila bugudha na kufurahia mapenzi mpaka pale watakapoona sasa imetosha. Pia inawasaidia endapo wataachana hapo katikati kunakua hakuna watoto watakaodhurika kwani kisayansi ndoa nyingi huvunjika katika miaka michache ya mwanzo.

Kiuhalisia ni kwamba wakati wa kuenjoy mapenzi ni wakati mkiwa hamna watoto. Watoto wakishaingia, sahau habari ya mapenzi! By the time watoto wanawaacha nyie mmeshajizeekea wala hamna mzuka tena.
 
Au mkeo anachepuka? Embu anza kuchelewa kuingia ndani, uone kama atashuka? Na ukifika home usiwe na time nae, wewe kuwa busy na siku yako ingia Jf, asipokuuliza juwa hiyo mchepukaji. Na umwambie ukweli na kuwa asije kulaumu Siku ukilaala kwa mariam.😀😀
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom