Mke wangu amegundua baba yangu alimuua baba yake

Mke wangu amegundua baba yangu alimuua baba yake

Dr.

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2014
Posts
217
Reaction score
193
Mimi ni Mtanzania, mzaliwa wa Kanda ya Ziwa umri wangu ni miaka sasa. Namshukuru Mungu nimebahatika kupata elimu japo kwa taabu sana na sasa nafanya kazi hospitali moja ya umma hapa Dar na huu ni mwaka wangu wa tano kazini maisha yanaenda.Nimeoa na nina watoto 2 mapacha wa kiume.

Nakumbuka nilikua darasa la sita,ulizuka ugomvi mkubwa kati ya mzee wangu na jirani yetu ambae ndie baba wa huyu mke wangu kipenzi. Katika huo ugomvi ambao chanzo chake ni mipaka ya mashamba bahati mbaya sana mzee ambae ni baba wa mke wangu alifariki katika mazingira ya kutatanisha kwani alichinjwa na watu wsiojulikana tena mchana akiwa shambani na mkewe pamoja na huyu mke wangu ambae kwa kipindi hicho alikua mdogo sana. Mzee wangu ndie aliehusishwa na kifo hicho kutokana na ugomvi na marehem na baadae akaja kufariki mahabusu kabla hata hukumu haijatoka.

Kutokana na uhasama huo hawa jirani zetu walihama na kwenda kuishi kijiji jirani maana hali haikua nzuri na huu ugomvi ulianza kua wa kiukoo.Wao walizaliwa wawili yeye na dada yake ambae nilikua nimetangulia darasa moja.Mgogoro huo uliniathiri sana kama mtoto na hasa kifo cha mzee ambae nilimpenda sana, zaidi kilichagiza umasikini wa kupindukia hapo nyumbani.

Hata ivo nilisoma kwa bidii na katika mtihani wa darasa la saba nilifanya vizuri na kuchaguliwa kujiunga shule ya sekondari Ihungo iliyoko manispaa ya Bukoba.Kutokana na umbali pia umaskini sikurudi nyumbani hadi nilipomaliza kidato cha nne.Niliumia sana nilipofika na kuambiwa mama amefariki dunia ni miezi mitatu iliyopita.

Nilikaa kijijini hadi matokeo ya kidato cha nne yalipotoka, nilichaguliwa kujiunga kidato cha 5 shule ya sekondari Ndanda iliyoko wilaya ya Masasi mkoani Mtwara ambapo nilihitimu kidato cha sita mwaka.Nilifanya vizuri na kubahatika kujiunga chuo kikuu nikisomea masuala ya afya miaka miwili baadae yaan 2002.

TULIPOTOKA
: Nakumbuka nilikua mwaka wa mwisho wa masomo yangu nilitumiwa shilingi laki nane na rafiki yangu ambae tulikutana kipindi tuko advance alitaka nimnunulie madawa kwenye maduka ya madawa kisha nimtumie huko Dodoma ambako ndiko anafanyia biashara zake.Baada ya kuchukua ile pesa benki niliiweka kwenye begi ambalo ndani yake pia kulikua na laptop yangu nilipanda daladala ambayo ilijaza sana abiria,nilipanga niende nyumbani kisha kesho yake niende madukani kununua mzigo wa jamaa.

Sjui nini kilitokea nilichukua begi langu na kumkabidhi binti ambae alivalia sare za shule anishikie,yeye alikalia siti.Baadae kidogo abiria walipungua nikapata siti na kukaa, kutokana na uchovu nilipitiwa na kausingizi nilikurukupuka niliposkia konda anataja kitua ambapo natakiwa kushuka,niliteremka haraka, ile navuka barabara nakumbuka sina begi. Nilihisi kuchanganikiwa, kibaya zaidi laptop yangu ilikua na documents zangu muhimu ili nihitimu.Nilikaa chini machozi yakawa yananilengalenga sikujua pesa ya jamaa ningeipataje.

Nilirudi nyumani maeneo ya Magomeni ambapo nilikua napanga.Ilipita wiki nzima siendi chuo huku nikimdanganya rafki angu kua nimeshanunua mzigo nitamtumia. Katika kueleza huo mkasa wangu kwa rafiki yangu mmoja aliniuliza unakumbuka huyo binti alivaa sare za rangi gani, nilimtajia japo sikuwa na uhakika sana akanambia huyo atakuwa mwanafunzi wa Jangwani kesho twende. Kesho yake saa kumi na mbili asubuhi tulikua maeneo ya shule tukimwangalia kila mwanafunzi wa kike anaeingia na kutoka ila hatukuambulia kitu, kibaya zaidi nilkua sina uhakika na sura ya binti mwenyewe.

Tulikata tamaa maana tulirudia zoezi kwa siku mbili bila mafanikio. Wiki ya pili tangu begi lipotee nilipigiwa simu na yule rafiki yangu akanambia ana mshikaji waka ni mwalimu pale Jangwani ameongea nae anasema kesho twende atatangaza parade kama tuna uhakika ni mwanafunzi wao ndie aliondoka na begi.Tulifika, kweli wanafunzi wengi walikuepo walitangaziwa kisha sisi tukaondoka.

Siku ya tatu nikiwa chuo nilipigiwa simu na yule mwalimu akanambia niende shuleni.Nilifika hapo shuleni nikakutanishwa na mwalimu wa zamu na wa nidham ambao walinambaia kuna mwanafunzi anao huo mzigo.Aliitwa, akanambia begi analo ila amemwachia mjomba wake amba anishi nae, kwakweli sikuamini macho yamgu nilibaki namtazama yule binti ambae kwa wakati huo alikua kidato cha nne nilijikuta namkubatia bila kujali walimu wake. Nilikabidhiwa kwa mwalimu wa zamu ambae tuliambatana na huyu binti hadi kwao, alikuwa anaishi Gongo la Mboto.

Mjomba wake alinikabidhi begi na pesa yote ikiwemo,alikua ni mzee sana ila mwenye busara nyingi, nyumba iliyochoka isiyo hata na umeme. Nilishangaa sana. Kuanzia siku hiyo nilijikuta nimetokea kumpenda sana yule binti lakini kitu nilichogundua haraka sana alikua ni mtoto wa jirani yetu ambae alikua na mgogoro na marehemu baba kabla hajafariki.

Hili nililigundua kutokana na yeye kufanana na dada yake ambae tulisoma wote primary ingawa sasa nilikuja kujua kua nae alishafariki, pia mama yake alishafariki.Kiukweli alikua binti mmoja mzuri sana yaan mrembo hasw japo maisha magum yalificha yote. Nilibahatika kumaliza chuo mwaka 2008 na yeye akamaliza kidato cha nne. Bahati mbaya hakufaulu vizuri. Nilishampenda sana mwaka 2010 tulifunga ndoa takatifu.

MADA KUU:
Tumeishi kwa amani, furaha na upendo wa hali ya juu huku kipato nacho kikizidi, ila kwa vile nilimpenda sana na kwa kuhofia asije kujua historia halisi ya maisha nilimwambia kwetu ni hapahapa Dar na kumtambulisha mzee mwenye nyumba Magomeni nilipokua naishi kipindi nasoma kama baba yangu na aliamini hivo, nae huyo mzee amefariki mwaka juzi. Nimekua nikiishi ndugu zangu halisi kiujanjaujanja na nilipotaka kwenda kwetu ilibidi niende kwa kujificha sikuwahi kuambatana na mke wangu.

Sasa mwezi huu mwanzoni alifariki yule mjomba wake ambae alikuwa akiishi naye. Kwa kweli nimekuwa sijihusishi na mikusanyiko yoyote ambayo inanikutanisha mimi na familia yake na mara nyingi natoa sababu au nasafiri ghafla; Kwenye huu msiba ndipo yalipoibuka yote na yeye akafahamu kila kitu. Alilia sana, nilibembeleza lakini wapi.

Ni wiki sasa tangu atoweke nyumbani na mwanangu mmoja. Nimemtafuta kila mahari simpati. Maisha yamevurugika mtoto anauliza alipo mama mama mi namwangalia tu.

Hata siku moja hatukuwahi kukwaruzana nampa kila anachotaka, ni mwanamke mkimya sana na mwenye upendo wa kweli sijui kwa hili itakuaje.
 
Duh pole sana mkuu. Kama ni ukweli kuwa mlikuwa na amani na upendo katika maisha yenu ya ndoa like you said, i'm pretty confident atarudi tu muendelee kutunza familia na maisha. Right now she needs time to come to terms with what transpired, that's all (especially the fact that you kept such a huge secret). Ila I'm sure after digesting everything she will realize that you are both victims of the situation so hakuna faida kulaumiana.
 
Duuuuh!Hii imenisikitisha sana.
Pole sana mkuu.
 
Pore bro hayo matatizo yapo sana hasa kwenye jamii hii ya kibongo. Bifu kwa wazazi mpaka kwa watoto. Kikweli sipendi hiI tabia
 
Kwa hiyo mtot akilia na wewe unalia au unamwangalia tu
 
Pole sana,
hata mimi ninaimani atarudi mpe mda huku ukiendelea kumtafuta na kumshawishi
 
Kula matunda ya uongo wako. Mijitu mmezoea kuishi kwa uongo wakati mnaambiwa KWELI ITAKUWEKA HURU. sikupi hata pole maana mdomo wako ndo umetengeneza haya yote.
 
Traditionally hii hali inaweza ikarudi kivingine baadae ikaathiri kizazi chenu but all in all ungekuwa mkweli ingesaidia na sijui ungeendelea kuishi kama digi digi mpaka lini na huyo ni mke wa ndoa
 
Alitakiwa umweleze ukweli tangu siku ya kwanza, tena ungeanza na "kama nakufananisha vile wewe mtoto wa Fulani?" Baadaye ndio ungemweleza ukweli angekuelewa Ila hata hivyo ni ngumu kidogo kila akifikiria 1. Matatizo yote aliyoyapata yamesababishwa na baba yako 2. Kumbe wewe ulijua hilo ndio maana ukamficha ukweli. Hapo Mkuu sikufichi tegemea msamaha kwa mbali sana tena labda kwa ajili ya watoto na si kwa ajili yako,
 
Pole sana kijana.duuuh omba mungu yote kwake yanawezekana
 
Yaani wewe ungekuwa bongo muvi na ela ya kampeni ya ccm ungekula kama Wema sepetu kwa story zako tena wewe ni wale Wa story hii ni ya kweli maana aitakuwa na jini anatokea kwenye pembe
 
Kikubwa Mungu kapanga mue pamoja,tokea hyo stoli ulivyoisema,maake ni vigum mtu kulala na kumuachia mtu mzigo wako mzito tena uliekua nae na stori nyuma tena nzito kama hyo
Bro huyo ndo mke Mungu aliekupatia na inatakiwa umtafte na ukae nae,kwanza upole na utulivu wake ni kwa sabab ya vifo vya nduguye na kila mtu wa karb yake,kingine akifikilia we ndo the only hope she had na pia familia yako ndo imefanya mpaka sahv ukoo wao uko hvyo tena ukiangalia mjomba wake nae kafa,Mungu anamaana yake kuwakutanisha
Cha msingi mtafte kwa bidii na kumuonesha unampenda maana sahv kilio cha moyo wake kimeanza upya,na cha sahv ni kikubwa kuliko asikwambie mtu,mtafte umtulize mwenyewe na umwambie ukwel kabisa kua ulijua mapema
Mr weka mambo sawa maana adi kaskia imeongelewa sana uko msiban,na cha msingi we ndo umtulize maake kilio cha mtu kama hyo Mungu nae huskitishwa na kilio chake
Jinsi ya kumpata
~tafta marafiki zake,either shulen au kazini,na wabembeleze wajue kwel unania ya kumpata,ata ikiwa kwa ndugu we wafate tu,ili wote wajue unampenda,wasije wakafikilia unaweza kumdhuru maake ishajulikana
Usitegemee aje2,ila mtafte na kila mtu ajue unampenda na halikua kosa lako
 
Back
Top Bottom