Mke wa rafiki yangu

manuu

JF-Expert Member
Apr 23, 2009
4,064
10,731
Wamekuwa kwenye ndoa kwa miaka 8 na wana watoto 2...Ilitokea mtafaruku baina yao uliyopelekea mke kuondoka nyumbani kwa mume wake na kwenda kwao kupumzika...

Taratibu za mazungumzo ya kuwasuluhisha zimeshaanza na mda si mrefu mke atarudi kwake..Mke akiwa kwao akapata kazi kwenye shirika lingine tofauti na lile alilokuwa akifnyia kazi...
Kufika kule kwenye lile shirika kuna rafiki yangu na yeye anafanya kazi kule ,yule mke wa jamaa hajui kama yule jamaa anamfahamu..Jmaa akaja akaniambia nimemuona mke wa rafiki yako kaingia kwenye shirka letu kama mhasibu muhasibu pale.

.Kwenye shirika lile kuna jamaa ambaye yeye ni muathirika wa virusi vya ukimwi ambaye mke wake alishafariki sasa huwa anafanya kama makusudi kuambukiza na huwa anatangaza kuwa mwanamke akaijichanganya anampa jamaa aliethirika ni financial controller hivyo wapo ofisi moja na huyo mke wa rafik angu ..

Sasa jamaa amekuja kaniambia huyo Financial kamwambia na kwa ushahidi wa picha kwamba last wkend toka ijumaa alikuwa na yule mke wa jamaa angu kwake na kapiga bila hata kinga..
.Na kuanzia jtatu jamaa anasema wanaenda lunch pamoja kwa kutumia gari la huyo FC anaacha lake prking...Nataka nimweleze rafiki yangu kuna tetesi wife wako ana uhusiano na jamaa ambaye kuna uwalakini kwenye afya yake hivyo hata mkirudiana hakikisha mnaenda pima afya kwanza kabla hamjafanya chochote..

Na tafakari sijui huyo rafiki angu atapokeaje swala hili ila nimeamua kwa namna atakayopokea mimi nitamweleza tu..
 
Tafuta mtu mwingine wanaofahamiana amweleze.Ukimweleza wewe atakushangaa kwa nini unafuatilia nyendo na maisha ya mkewe.Si ajabu mkakosana.
 
katika suluhu ya kurudiana mwambie tu rafiki yako ni bora mkapima kwanza kabla ya kuanza kufanya tendo si lazima umweleze kuwa mkeo ametembea na mwathirika ..... ila kama akitia ngumu mwambie pia wanawake wa siku hizi si wale wa zamani ambao ni wavumilivu wengi wanagawa tu bila aibu.. jamaa yako ajiongeze apime asipo fanya hivyo shauri yake
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom